TBT moja Safiiiii

Mama has always been a thorough woman since way back in the days,especially with the house chores.
Countless times nimeosha vyombo na machozi.
Hio ni after uliambiwa uzioshe saa nane, lakini we ni nani, umejiona time keeper ati,“acha nikacheze chobo ua 1hr alafu ntarudi nizifanyie justice matime”.

Venye saa mbili inafikanga haujuangi,unaonanga tu ka giza flani kametokea pwaaa out of nowhere. Hapo ndo unakumbuka venye ulisign memorandum with your old man juzi amidst tears, akakushow Swaleh Mdoe asiwai anza kuchachisha habari za saa moja Nation tv kama hauko kwa hio nyumba(unless umetumwa).
Saa hizo ndo unaskia gang ikikushow ati kuna venye na vile waliona mzae wako akiingia.
Unatoka siaka destination kejani.

Unafika kwa mlango kitu ya kwanza ata kabla uknock unachungulia kwa hako ka space kadogo curtain inawachanga.
Chenye umeona ishakumaliza nguvu tayari, juu kuna vile miguu zako zishaanza kutetemeka ni ka uko na rickets alafu ka moyo kanaanza kupiga 90 hadi shati umevaa inaanza kuvibrate.
Hapo sasa inabidi utafute support na hizo chuma za stairs kabla mans acollapse ama arelapse juu enyewe umeona wall clock inadai ni 8:30 na pia umeona man of the house akiwa comfortably tucked in his couch.
Sijui hio combi ilikuwa inamaanisha nini kwenu,lakini mtaani hii ilikuwa lethal yaani bio hazardous juu enyewe unapiga hesabu ile beating unaenda kupokea hadi unaanza ku rehearse venye utalia dramatically ndio session isiende sana.

Sasa bado ukiwa hio harakati ya kujiprepare pschologically kamlango kanafunguka fwaaa(sistako anaenda kwa duka)
Nakushow boychild unashtuka hadi kidogo unadai kutoka mbio,lakini hauezi juu kale ka mwangaza ka sito kamekumulika mbayaa
Hapo tena unagundua kumbe umeparara, unakaa ni ka umetoka excursion pale Sahara desert
Juu after chobo ua, uliendesha tyre, ukacheza bano,ukaenda duf mpararo alafu ukamaliza na brikich
Sai wewe na chokosh tofauti tu ni hauna gum kwa mdomo.Kuzidisha vyombo za matha haukuosha.
Masibling saizo wamenice yao yote wanajua tu leo lazima kanuke, mjunior kwanza amengoja niaje atumwe hio rod.
Sasa hapo ndo ile spirit ya Koitalel Arap Samoei inakupanda unapata courage ya kuingia…Alaaaaaaafu

The rest of the stori ni histori, yaani imekataa kutoka huko TBT.