TBT: Pwaguzi kapata pwagu

kush yule mnono

Retired Hekaya Master
#1
These were the early days when kuwa na mobile ilikuwa ni priviledge. You could literally count the chosen few. Hii ilikuwa time bado ukauzi mob ya tao haikuwa. Hizo days nlikuwaga kamjuaji fulani hapo CBD. Had just been employed na ka salary ka 12 thao.

So end month kufika nkaamua kupiga mwenda pale Luthuli ncheki ka tifi ka coloured kazuri kale ntarudi kubuy once shande imeingia kwa mfuko. Nkavaa tisho ju ya coverall ya job ndo isijulikane, then crossing Moi avenue pale Archives nikavuka Tom mboya street pia na kuingia Luthuli avenue.

Went straight kwa shop ya muindi and after kuchat na bro ya @vunja deki , salesman pale akanisho teli kathaa and I finally settled on one Sony trinitron 14 inch at 10k. Tukabonga na muindi ikabaki ntarudi kesho yake. On my way out nkapata ma hawkers wametandaza bidhaa zao pale wanaimba bei. Nkashika ngepa moja and then I was on my way back to the work location.

While waiting for ma threes kupita ndo nivuke Tom mboya kurudi ki Moi avenue, ka @Chokoste fulani hivi hivi kaka kwom hapo kando nkama pia kanataka kuvuka rodi. Akani gotea nka goteka alafu akanichekeshea tenje moja swafi. By then nokia ndo zilikuwa kusema.

Akaona amekwachu attention yangu so akasogea karibu akaitoa yote nkaicheki. Akaipitisha akanisho ncheki kama iko sawa alaf nkijiskia nayo tunaweza chapa biz. Nka confirm kabisa adi ilikuwa na line ya kencell, tenje inawak poa. Nkaulizia bei akadai ni thao ngovo, hapo nkaingiza mguu moja kwa box yake. Hio bargain ilikuwa vv tempting so nka cancel ku cross road and made 2 steps backward ndo tujadiliane zaidi. Akadai tenje kwanza nkamrudishia alafu tukaanza kutembea tukienda ki fire station nkiendelea ku bargain. Finally tuka agree on thao moja. Hapo nkaingiza mguu ya pili kwa box.

Kijana alikuwa steps ka tatu mbele yangu akadai tuchape biz chap chap tukiendaga kabla ma ponyi wasome rada yetu. Biz ikachezwa ni kama majamaa wa ma dre. Mi nkatoa niadu nkampitishia na yeye akapitisha mali na bila kwaheri kila mtu akachora kiviake. Mimi huyo nkavuka Tom mboya hapo karibu na Imenti house mbio sana karibu nchotwe na moti. Nkatokelezea Moi avenue hizo area za nairobi sports house and ran all the way adi Kenya cinema plaza where I was working.

Nkaingia base na pupa ata nkashtua maboy wangu wa waks. Not able to hold the joy no more I broke the good news to them boys. Ikawa .... "mabuda mnajua niaje, nmeangukia tenje moja ya power sana at a v throw away price na ni nokia latest model". Nokia 5210 was the bomb then, if you know you know.

Wafula, mluya moja kumbaff wa Ungwaro huko gatina akaingilia story na kudai ... "muchamaa wekelea hako kasimu hapa tukaone ama pia uwaje".

Yours trully akatoa simu and decided to switch it on ndo niwasho uzuri wa kuwa mjanjes. Kujaribu kufinya the end call button which doubled up as the on/off switch, nkapata resistance. Kujaribu tena hai cooperate. Nka decide kuitoa cover ndo ncheki battery. Hapo ndo "nlioneko maachap" in Wafula's words. We all couldn't believe what we were seeing na sana sana mimi, being one of the kimenyis kwa hio base, a born tao, msomi wa Jamhu. It was a hard one to swallow. Nli buy ordinary mud kwanza ile ya red, stuffed inside covers ya mobile and made to look like a genuine phone. I became the talk of the base for the right reasons.

What a funda I was kuingizwa box mzima mzima na nkatoshea. Nlihapa huyo boy mahali ntapatane naye, liwe liwalo lazima ataona moshi. Hio shift nliimada bila kuroga na anyone, tukaitwa kwa office mmoja mmoja na kuhesabiwa, kiasi tu, tukafunga works.

Bado nkiwa na hasira zangu, nkateremka same luthuli avenue, kwenda pale down karibu na apple bees kwa ka kichorochoro ma vaite huuza veve. Nkakuta murume wangu and while bado tunabadilishana mawazo as to sharba gani poa, saitan ikajileta. I guess hio masaa kathaa ilikuwa imepita hakuwa ata anakumbuka watu ameosha.

Akajidunga kibanda next na kuanza kuchagua masharba. Without mambo mob nlimkuta huko na before ajue anajuwa alikuwa chini. Nlimpiga hedi moja swafi and watched as the nundu on his forehead grew bigger rapidly. Kuamka nka adisia kahasho, yeye kuinama mimi huyo nkampatia avunja kwa shavu akatema mate. Me being an ordinary pale, ma vaite wakafika kujua ndiambo ni gani.

Nkawachapia hio story ikabidi boy arudishe maganji zangu hio noma ikatike. Alinichota 1k lakini mimi nkadai thao sita and luckily alikuwa na more than that kwa mfuko plus ile tenje moja aliniweka nayo box. Kiroho safi hio pia nlimuosha. Ma vaite wakampapasa tena kiasi na kumtoa kijiko.

Mi naye nkalipa mbachu chap chap na kudandia mat ya namba tisa hapo luthuli nijitoe kwa hio scene upesi kabla mboys arudi na geri yake. Nlidondokea pale juu kariokor nkavuka roady na kuingia kbs namba 46 adi Ungwaro mtaani. Nlijipatia likizo for sometime ya kutofika hizo ma area za tom mboya kurudi na huko chini. Ata teli sikurudi ku kwachu tena.
 

Top