TCRA Msishindane na teknolojia, kaeni na bloggers wa Tanzania tuyajenge

Habarini za leo, napenda kuwapa pole ndugu zangu Watanzania kwa yaliyotupata. Kwakweli usajili kama usajili ni jambo jema sana kwasababu linafanya blog zetu zitambulike rasmi kama vyombo vya habari na pia tungepata fursa ya kulipa kodi nchini, tatizo ni namna mlivyolileta kwa haraka na kulipitisha bila kutushirikisha, naamini mngekaa nasisi tungejadiliana mengi na pengine tungetoka na muafaka bora zaidi.
Sasa haraka zenu zimefanya blog nyingi za Tanzania kusitisha huduma (japo zipo nyingi zilizoendelea leo japo hazijasajiliwa), matokeo yake ndiyo haya sasa, mmetuzimia JamiiForums, tumehamia KenyaTalk na faida kubwa haitakuwa kwa vijana wetu bali itakuwa kwa vijana wa Kenya wanaomiliki jukwaa hili, naomba mfahamu kuwa jambo pekee mnaloweza kufanya kutuzuia kabisa ni kuzima huduma za internet vinginevyo hamtaweza kutuzuia maana tutaendelea kupitia majukwaa ya nchi nyingine kama hili.
Mheshimiwa Mwakyembe tafadhali hebu ingilia kati, tukae pamoja, tujadiliane, tutoke na maazimio, tupewe muda wakutosha kujisajili, na ada zisiwe za kutukomoa.
Ahsanteni KenyaTalk kwa kutupatia jukwaa.

Poleni kwa yaliompata. Ila kuna kamsemo huenda hivi…

Kufa kufaana

Hahahaa, thanks @4makind nikweli, hii imekuwa fursa kwenu!

@Sijuti Sio kwamba www.jamiiforums.com imefungwa kabisa, forum kubwa kama ile haiwezi kufungwa kirahisi vile. Wanavuta kasi kwani kuna shida ya faragha za watumiaji wakiweka mambo sawa watarudi kwani hawashindwi kulipia 100,000/= na kulipia ada ya mwaka ya 1,000,000/= shida ni sheria kutaka kila anayepost wamjue ni nani. Hawataki anonymous.

tooba!

Hiyo ndo nimesema kuwa wangetuita bloggers na online forums administrators tungeyajenga na kufikia muafaka tu

Huh??? Hiyo jina ni ile yetu Kenya?? Ama ina maana pole tiizedi?

Mtakaa sawa lakini wao wanataka wanaopost wote wawe uchi ili hata kama kuna cha kusema ukiwa umejificha kisionekane hasa zile siri zao kubwa kubwa kama ufisadi pia makampuni makubwa na vigogo wenye kashfa mbali mbali. Hata mkikutana ni ngumu ngoja tuone watafanyaje hawawezi kupoteza empire kubwa kama ile na walikuwa wananufaika na matangazo mengi.

Hadi wafungue Jamiiforums tutadumu huku kwa majirani.

Tunataradari uhamishoni two five four …

Ada ya forums?

tcra tcra tcra

jiwe haambiliki jamani dahh… tunakolekea siyooo

Hahahaaaa

Yap

Kuna Nyumbu yeyote wa kijani humu?

Nipo nipo nipo mkuuu, hahahahaa, mzee wa buku 7 - Lumumba camp

bavicha mna sheeedaaaah!

Honestly tumejikuta tunaitwa Diaspora via TECHNOLOGY.
JPM falasi sana

Kweli hujutii mkuu