Bwana Mungu, nashangaa kabisa, nikitazama kama vilivyo,
nyota, ngurumo, vitu vingi vyote, viumbwavyo kwa uwezo wako.
Roho yangu na ikuimbie, jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie, jinsi wewe ulivyo mkuu.
Nikitembea pote duniani, ndege huimba nawasikia,
milima hupendeza macho sana, upepo nao nafurahia.
Nikikumbuka kama wewe Mungu, ulivyompleleka mwanao,
afe azichukue dhambi zetu, kuyatambua ni vigumu mno.
Yesu mwokozi utakaporudi, kunichukua kwenda mbinguni,
nitashukuru na kwimba milele, wote wajue jinsi ulivyo.
Roho yangu na ikuimbie, jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie, jinsi wewe ulivyo mkuu…
Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Damu yake na sadaka, nategemea daima
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele yake
Kwake Yesu nasimama, ndiye Mwamba ni salama
Ndiye Mwamba ni salama, ndiye Mwamba ni salama
Yesu ndiye kiongozi wangu…kumfuata yeye ni furaha…ajuaye kuongoza vyema…
anilinda nisione shida…analeta raho moyoni…
Mwimbieni Bwana hii…
Naupenda ndio maana nimeuweka hapa
Tenzi za Rohoni… zina ushuhuda mkubwa sana…
Nyimbo za tenzi nzuri sana haswa ukiziimba kutoka ktk vilindi vya nafsi na roho yako hujisikia kuhuishwa
Twende kwa Yesu mimi nawe,
Njia atwonya tuijue
Imo Chuoni; na Mwenyewe,
Hapa asema, Njoo!
Na furaha tutaiona,
Mioyo ikitakata sana,
Kwako, Mwokozi, kuonona,
Na milele kukaa.
“Wana na waje,” atwambia.
Furahini mkisikia;
Ndiye mfalme wetu pia,
Na tumtii, Njoo.
Wangojeani? Leo yupo;
Sikiza sana asemapo;
Huruma zake zikwitapo,
Ewe kijana, Njoo.
LIKO LANGO MOJA WAZI
1.Liko lango moja wazi, Ni
lango la mbinguni; Na wote
waingiao Watapata nafasi.
%Lango ndiye Yesu Bwana
Wote waingie kwake,
Lango! Lango La Mbinguni
ni wazi.
2.Yesu ndiye lango hili, Hata
sasa ni wazi, Kwa wakubwa
na wadogo, Tajiri na maskini.
3.Hili ni lango la raha, Ni lango
la rehema; Kila mtu apitaye
Hana majonzi tena.
4.Tukipita lango hili Tutatua
mizigo, Tuliochukua kwanza,
Tutavikwa uzima.
5.Hima ndugu tuingie Lango
halijafungwa, Likifungwa mara
moja Halitafunguliwa.
AKIFA YESU NIKAFA NAYE
1.Akifa Yesu nikafa naye
Uzima upya huishi naye;
Humtazama mpaka nje:
Nyakati zote ni wake yeye.
%Nyakati zote nimo
pendoni, Nyakati zote ni
uzimani, Humtazama hata
atokee, Nyakati zote mimi
ni wake.
-
Vita sipigi visivyo haki, Na
Bwana wangu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki, Napo
po pote hila sitaki.
-
Sina mashaka, akawa
mbali; Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Imanweli, Nyakati
zote mimi husali.
-
Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi chozi, wala siguni;
Sikuti afa, ila kitini Daima
hunifikiri mimi.
-
Kila unyonge huusikia; Kila
ugonjwa kwake hupoa; Yesu
ni mwenye kuniokoa Nyakati
zote hunijalia.
Mungu ni pendo apenda watu,
Mungu ni pendo anipenda
Sikilizeni furaha yangu,
Mungu ni pendo, anipenda
Nilipotea katika dhambi,
nikawa mtumwa wa shetani
Akaja Yesu kuniokoa,
yeye kanipa kuwa huru
Sababu hii namtumikia,
namsifu yeye siku zote.
paap
14
N
natafuta hiyo audio ya huu wimbo OG
Unaweza pata google,u tube hata playstore zitakuwepo application zenye audio
paap
16
Kote sijafanikiwa nimeutafuta sana