Tetesi: Jamiiforums kutorejea hewani kabisa

Kuna taarifa nimezipata kwa mtu mmoja mkubwa tu na yupo pale tcra na anajuana na wakubwa mno

Kanitonya kuwa jamiiforums kurudi hewani mapema ni ndoto na akasema hata ikija kurudi itachukua miaka mingi sana

Unaambiwa usimuamini mtu yoyote hao wenye jf wenyewe wanapoozwa na mkwanja

Hivi mnakumbuka ile issue ya kabla ya maandamano ya tarehe 26?

Mnakumbuka jf ilipotea ghafla??Basi unaambiwa ni jf wenyewe waliamua kwa amri kutoka juu

Hongera kenyatalks kwa kutukaribisha
Cha msingi tufanye hivi kama ulikua na marafiki mnaojuana kule jf ni muhimu kuwajulisha waje humu wahamie huku ili tuendelee kuwa wengi
Kila mtu amuinvite kila mwenzake anayemfahamu ahamie huku

Maana jf ndo basi tena

mtoa mada wewe ni lumumba, mimi kumwamin mwana lumumba Ni pale akifa na kweli nikamkuta au akanikuta ahela, lakn hata nimwone anaingzwa kaburn siamin

@Lizaboni wa Jf ni CCM damu kwahiyo apuuzwe.

Tutasikia mengi

Mpuuzi katika upuuzi

Huyu siyo @Lizaboni orijino!!

@Lizaboni wa kweli hafanani na mtoa mada hata kwa maandishi

nilichofurahia ni kwamba jf kufungiwa wote tunaisoma namba

Lumumba hata nyie kwa kupigia propaganda hakuna …naona wote tunabanana huku huku KenyaTalk

Huu mwandiko umeukopa kwa dada flani hivi!

Sawa tu, chamsingi tupo JF kupitia KT

Za kuambiwa changanya na za kwako…

Usiwapangie watu cha kufanya…

Cc: @Mahondaw

Kumbe hili limewakumba mpaka nyie Ccm? Nilitegemea mtakua na furaha kwa JF kutokua hewani, kumbe na nyie mnaumia.

Aiseee

tetesi zako zishindwe na zilegee, nimepakumbuka nyumbani

Ingekuwa kupozwa na mkwanja wangoleshapozwa siku nyingi kwenye zile kesi zao ili wamtaje muanzisha zile nyuzi za ukwepaji kodi wa oilcom

Melo na wengine mnaopambana JF irudi, please prove this guy wrong. Natamani sana amezeshwe maneno yake. Long live JF og.

Mkuu @reyzzap hawa ndio wale ambao tukikutana nao huko mbele baada ya kufa lazima tuchochee kuni sana.

Sie kabisa.

hahaaa pale jehanam, mkuu kuliko kumwamin mwana lumumba au tbc bora uingze vocha ya halotel kwenye voda yaweza ikakubali kuliko hawa viumbe, sina uhakika hata na mpira wanao onesha tbc yaweza hata iwe wanatuchezeshea PS fifa 2018