Tetesi za soka 23 Juni 2018

Real Madrid wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Lyon Nabil Fekir, huku Liverpool ikiwa katika hatari ya kumkosa mchezajihuyo mwenye umri wa miaka 24 mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa.

Arsenal imefanya mazungumzo na mchezaji wa Sevilla na timu ya taifa ya Argentina Ever Banega, kuhusu uhamisho kuelekea Emirates.

Manchester City na Paris St-Germain wana hamu ya kumsajili mchezaji wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 29 kiungo cha ulinzi - Jerome Boateng.

Chelsea wanaelekea kupunguza malipo kwa kumfuta meneja Antonio Conte kwa kutuhumu kwamba hakushughulikia vizur kuuzwa kwa Diego Costa.

Manchester City wanaelekea kukaribia ufanisi wa usajili wake wa kwanza wa msimu wa joto baada ya mzungumzo mazuri kuhusu mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho, 26.

Manchester City inajitayarisha kuidhinisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya mchezaji wa kiungo cha kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, ambaye pia amehusishwana uhamisho kwenda Barcelona.

Meneja wa Rangers Steven Gerrard ana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria anayeichezea Roma Umar Sadiq, mwenye umri wa miaka 21.

Tottenham wamehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa wa timu ya Nice Alassane Plea, mwenye umri wa miaka 25, huku meneja wa Spurs Mauricio Pochettino akionekana kumpa ushindani Harry Kane.

Liverpool wamedokezewa kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City na Switzerland Xherdan Shaqiri.

Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Jack Wilshere, ataamua kuhusu mustakabali wake akiwa mapumzikoni baada ya kuondoka Arsenal.

Mesut Ozil wa Arsenal ataomba kuvaa kazi nambari 10 baada ya Wilshere kuondoka.

Pablo Zabaleta, wa Argentina anasema timu ya taifa hilo katika kombe la dunia inaonekana ‘imevunjika moyo’

Meneja wa Ubelgiji Roberto Martinez anasema mshambuliaji Romelu Lukaku, wa miaka 25, hana lengo la kushinda tuzo la the Golden Boot katika Kombe la dunia, badala yake anataka kuisaidia timu hiyo.

swadakta