Trevor Noah vs Trump.

Stewie

Senior Villager
#1
"Wakuu mumeona vile Trevor Noah ana muharass D.Trump kwa Tivii?":D. Kwa mbongo ambaye nina uhuru kidogo wa kujieleza sometimes huwa nahisi kavuka mipaka, lakini ukweli uhuru wa kujieleza unatakiwa ufike huko.

Nilikuwa naona pia jinsi anamnanga Jacob Zuma. kumbe South nao wako mbali sana kwenye hii ishu ya Uhuru wa kujieleza!!.

Hivi kwa nini nchi maskini zinachukulia uhuru wa kujieleza kama ni kikwazo cha maendeleo na wakati zilizo tajiri zinachukulia kuwa ni chachu ya maendeleo na wote tunaona ni kweli!?. Je kupinga na kuminya uhuru wa kujieleza ni kwa maslahi ya nchi hizo au ya viongozi wao?.

Kwakweli ukiona Jinsi Trevor Noah msouth Africa akimnanga Trump ndani ya ardhi ya Marekani na ukileta hiyo Scenario Tz unapata picha nyekundu na matobo ya risasi na maneno "anatumiwa na maadui wetu". inabidi tupambane tuwe na uhuru kama ule, tusisettle for less.
 

Top