TUCHEKE, TUVUNJE MBAVU, TUONDOE STRESS

#2
TOFAUTI YA UKOPAJI WA MZUNGU NA MSWAHILI:

Mzungu : Hi I need $ 100 will pay back on Monday.

Mswahili : Kaka vipi. Shwari ? Dah....hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini ? Juzi nimekuona kwa mbaali...mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, alafu misiba mingi, wife nae kajifungua ghafla, sasa kuna check naisubiri haijatoka hadi leo,wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata "laki moja" ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi....?
 
#5
*Ila jamani wanawake wa zamani walikuwa waelewa ,ebu chukulia mfano Yona alivyopotea zile siku ngapi halafu akarudi kwa mkewe akamwambia kwamba alimezwa na samaki na mkewe akakubali , ebu potea hata siku moja kwa mwanamke wa kisasa halafu mwambie hata ulimezwa na chatu uone kama atakuelewa!*
 
#6
*Uchawi Wa Kweli Ni Pale Unaposubiri Baba Yako Ambaye Ni Dereva Bodaboda Aende Kazini, Halafu Wewe Unampigia Simu Demu Wako Aje Nyumbani. Bahati Mbaya Inalalia Kwako, Kwani Baba Yako Ndiye Anayemleta Demu Wako. Na Kufanya Bahati Mbaya Iwe Mbaya Zaidi, Demu Baada ya Kufika Nje Ya Nyumba Yenu Anakupigia Simu Ili Uje Kulipia Usafiri.*

*_Kaka Yangu, Amini Nakwambia, Uchawi Upo_*
 
#8
*KWANINI UFE MASIKINI*?

BEI YA FIGO NI MILIONI 500-900
UZA FIGO MOJA KWA MILIONI 700
CHUKUA MILIONI 500 KABETI MECHI 2 ZA ODDS 2.4 MFANO MPE BAYERN WIN NA BARCA WIN
UTAPATA KAMA BILION 2.1
CHUKUA MILIONI 700 KANUNUE FIGO URUDISHIE
UTABAKIWA NA BILIONI 1.4 JUMLISHA NA ZILE MILIONI200 ZILIZOBAKI BAADA YA KUBETI INAKUWA BILIONI 1.6*
FANYA MIPANGO YA MAISHA
 
#9
*Hakuna mtu makini kama sisi walevi....wakati wa kuvuka barabara,kwanza tunaangalia kushoto na kulia kama kuna magari au pikipiki,*
*Tuangalia juu kama kuna ndege, tunaangalia chini kama kuna mabomu yametegwa, tunaangalia nyuma kama kuna mtu anataka kutukaba , tunashikilia bia kwa umakini kisha tunavuka barabara kwa zig zag kukwepa risasi.....*
 
#10
*Isaya:4.1*

*Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.*

Hiv hii siku inakuja Lin?
 
#13
*Hakuna mtu makini kama sisi walevi....wakati wa kuvuka barabara,kwanza tunaangalia kushoto na kulia kama kuna magari au pikipiki,*
*Tuangalia juu kama kuna ndege, tunaangalia chini kama kuna mabomu yametegwa, tunaangalia nyuma kama kuna mtu anataka kutukaba , tunashikilia bia kwa umakini kisha tunavuka barabara kwa zig zag kukwepa risasi.....*
Nimecheka sanaaa
 
#18
*Hivi ushawahi penda msichana hadi mkiwa church unamlipia sadaka...unaweka kwa kikapu alafu unamwambia mchungaji kwa ishara ya vidole kuwa sadaka uliyotoa ni."Ya wawili?* ".. ✌

ikifikia hatua hii basi ujue kazi ya moyo ni kusukuma CHAPATI
 
#20
Wapendwa leo kuna tukio la kuhuzunisha limenitokea. Nilikuwa nimesimama maeneo ya Retco nikisubiri gari, ghafla nikamuona mama mtu mzima analia kwa sauti kubwa, mda huo huo nilikuwa nimeshika simu yangu nachati na mtu. Ikanibidi nisogee karibu ili nijue ni nini kimemtokea yule mama, kumbe yule mama ameibiwa simu yake basi aliponiona mimi akasema simu yake aliyoibiwa mimi ndo nimeishikilia. Watu wakaanza kunipiga kwa silaha mbalimbali na kuniumiza vibaya sana lakini nashukuru Mungu askari walikuwa karibu na walifika eneo la tukio na kunichukua mimi pamoja na yule mama na kutupeleka kituoni. Baada ya kufika kituoni yule mama akapewa simu na afande ili apige kwenye ile simu yangu wahakikishe kama simu niya yule mama au lah!. Basi akapiga simu yake haikuita kwenye ile simu yangu aliyodai ni yake, bali iliita huko kwake na kupokelewa na dada wa kazi. Kumbe yule mama alidhani mimi nimemuibia simu yake maana ilifanana na yake.
Polisi wakashauri tuelewane pale pale, huwezi amini yule mama alitaka kunipa Milioni 40 cash kama fidia.
Bahati mbaya mkojo ukanibana ikabidi niamke kwenye hii ndoto na kwenda kukujoa chooni. Hili liwe fundisho kwa watu wote, kabla hujalala msinywe maji mengi ili msije mkakosa dili la hela kama hili.
 

Top