Tukomae na Professor ASAD amejipambanua ni mwana demokrasia. Ndugai &Jiwe wanataka kutufilisi

Profesa Assad anajua…tena anajua sana serikali ya Awamu ya 5 isivyo na discipline na matumizi ya fedha za umma ndo maana akiwa mcha Mungu wa kweli ameamua kusema ukweli anaoujua japo anazunguka sana - Prof Assad anahofia hawa watu wanaoongoza serikali kwa sasa kwa jinsi wasivyo na discipline wakiachwa hivi wataiingiza nchi katika ufisadi wa kutisha na pengine hata machafuko huko mbele ya safari, ndo maana anaonya na kuonya kila wakati na wala siyo mara moja…

Kwa hivyo anapoonya, anaomba umma tumsaidie - hakika atakuwa anatishwa na uchafu unaoendelea serikalini na kufumbiwa macho na Bunge chini ya Spika Ndugai - sote tunafahamu jinsi ambavyo report za kamati maalumu za bunge siku hizi haziwasilishwi zijadiliwe bungeni bali Spika Ndugai hukimbia kiguu na njia kwenda Dar es Salaam kuzikabidhi Ikulu…

Prof. Assad amewahi kuonya kuhusu alichokiita “Political Entrepreneurship” na akatolea mfano wa Uuzwaji wa Nyumba za serikali uliosimamiwa na Rais Magufuli enzi hizo akiwa Waziri wa Ujenzi…

Baada ya muda akasema nchi za Africa ikiwemo Tanzania hazipaswi kuwa na “strong men” bali zinapaswa kuwa na “strong institutions”…

Mwaka jana akatueleza Trilioni 1.5 zilikuwa zimepigwa kutoka makusanyo ya serikali…

Amewahi kuonya pia juu ya uchafu wa kivuko cha MV Bagamoyo…baadaye mtuhumiwa alitutangazia kuwa amekikabidhi jeshini na akatuonya ole wetu tuendelee kukijadili maana hicho sasa ni kifaa cha jeshi…

So, Prof.Assad ni wazi anatilia mashaka uadilifu wa uongozi ama kiongozi wa sasa katika kusimamia fedha za umma lakini anashindwa kusema kila kitu kwa uwazi - anatamani bunge litimize wajibu wake japo kidogo ili labda kupunguza ubadhirifu unaoendelea, lakini hasikilizwi…

TUMSAIDIE…Ndugai na JPM watakuwa wamezungumza namna ya kumtisha hata juu ya uhai wake, lakini TUMSAIDIE Prof. Assad…huyu ndo mtu wa KUOMBEA siyo yule alazimishaye aombewe!

Hakika

Time will tell…

Sio mwanademokrasia ni Mkaguzi.