UFISADI MANISPAA UBUNGO

Inasikitisha wiki iliyopita iliwekwa post hapa kuhusu tuhuma za unadhirifu zinazomkabili Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ndugu Beatrice Dominic Kwai na watendaji wake. Huyu mama anatuhumiwa kuidhinisha malipo hewa kwa ajili ya malipo ya pango la ofisi za halmashauri licha ya kufahamu malipo hayo yana uvundo wa ufisadi.
Manispaa imepanga jengo moja kwa mkataba lakini majengo mawili hayana mkataba hivyo serikali imekuwa ikilipa fedha nyingi na bila shaka ‘’cha juu’’ kimekuwa kikichukuliwa na waidhinisha malipo. JF wamepigiwa simu wameondoa hiyo post bila shaka kwa shinikizo la huyo mama au TAKUKRU maana huu ufisadi uko peupe mno unahitaji dakika 10 tu kuuthibitisha

Suala hili jalada liko TAKUKURU cha kushangaza TAKUKURU wamekalia hizi tuhuma na huyu mama kwa kiburi, ujeuri na ufisadi na watumishi wenzie wameamua kulipa malipo hayo bila shaka kwa kugawana cha juu. Huyu mama haogopi kutumbuliwa kwa vile pale Ubungo ameletwa na waziri mwandamizi ambaye abna uhusiano na mume wa huyo mkurugenzi. Mara nyingi amekuwa akijitapa kuwa hakuna wa kumtoa hapo labda serikali ibadilike.

Bila shaka kinga hiyo ndio inampa jeuri ya kufanya ufisadi mchana kweupe huku umma ukishuhudia. TAKUKURU mko wapi kwanini mmepiga simu JF waondoe hiyo post?

Duh…!

Time will tell…

Uongozi unabadilika soon…

Cc: @Mahondaw