UFISADI MKURUGENZI MANISPAA UBUNGO

#1
MALIPO HEWA YA KODI YA NYUMBA YA MKURUGENZI
Huyu mama amelipa Tsh 14milioni kama malipo ya pango ya kuishi mkurugenzi yaani nyumba ya kupanga kwa sababu Manispaa ya Ubungo haimiliki nyumba . Kilichofanyika huyu mama akatengeneza mazingira ya kutafuta hiyo nyumba yeye mwenyewe na mwenye nyumba kulipwa. Ufisadi upo kwasababu hiyo nyumba iliyolipwa Kunduchi bado inakaliwa na mwenye nyumba na huyu mama yeye anaishi kwenye nyumba yake Maramba Mawili Mbezi. Kifupi mama ametakatisha fedha.

KUGAWANA MAPATO KWA % NA KIWANDA CHA URAFIKI (SOKO LA MABIBO

Ufisadi wa pili ni kuwa Manispaa ya Ubungo wamepanga eneo la soko la Mabibo kiwanda cha urafiki. Baadaa ya majadiliano ya muda mrefu (kabla yeye hajaamia Ubungo) makubaliano ilikuwa manispaa iwe inalipa pango la upangaji (rent) kwa kiwanda cha urafiki. Lakini huyu mama anachofanya ni kuwa yale mapato ya serikali yanayotokana na tozo mbalimbali katika soko la Mabibo anagawana kwa asilimia na kiwanda cha urafiki. Baraza la madiwani hatuna taarifa juu ya huo utaratibu, wala hatukushirikishwa kuamua % ya mgawanyo wa mapato. Wapi uliwahi kusikia serikali inagawana mapato na taasisi nyingine. Huo ni ufisadi mkubwa maana hakuna anayejua hizo asilimia zilifikiwaje.

MAHUSIANO MABAYA NA WATENDAJI WAKE
Kwa muda mfupi aliofika hapa tayari ameshagombana na DT kijana mweledi na anayeijua vizuri kazi yake hadi ameamua kukimbilia Manispaa ya Temeke. Issue ni kuwa mama anataka kupanga timu yake ya kufanya ufisadi sasa alishaona kwa huyu kijana na wengine atakwama. Kagombana na kila mtu hapo ofisini kuanzia wafanyakazi wa kawaida hadi wakuu wa Idara, lugha yake ni matusi tena ya nguoni na kujisifia kufahamiana na Waziri mmoja Mwandamizi.

Serikali hebu fuatilieni mwenendo wa huyu mama. Safari ijayo tutaeleza hujuma zake katika ngazi ya kisiasa, na jinsi asivyoheshimu vikao vyetu madiwani kwa kufanya maamuzi yeye binfasi bila kushirikisha Council.

TAKUKURU, vipi lile suala la Mkataba hewa wa ofisi, mmeamua kulifukia?
 
Top