kuna thead moja wakati ule wa uhai wa jf, iliyokua inaelezea jamaa alivyotembelea drc congo, na namna tunavyochukuliwa wabongo huko congo. Ktk maelezo yake alisema wacongo ni watu poa na wanatupenda na kututhamini sana wa tz kuliko nchi nyengine. Katika comment za “villager” wengi walisurpot tathimini yake na kuongeza nchi zengine zinazotuthamini na kutukubali wabongo, wakiitaja kenya. Yani mjadala ulikua nani namba moja kati ya mkenya na mcongomani kwa kutujali pindi tunapokutana viwanja nje na aridhi ya nyumbani. Sasa ninachoshangaa, au hoja yangu, tangia tumekuja huku kt ugenini, comment za wakenya ni tofauti na tulivyoaminishwa kwamba wakenya ni ndugu zetu na hawana chuki au kuonyesha chuki kabisa baina yetu. Mbona comment za wakenya wanaonekana kuchukia wa tz sana.
Mbona sija muona mkenya hata mmoja ameongea hovyo juu ya mtanzania?wa tz msiwe na hio roho bana.
Kama una sema kuna chuki dhidi ya wa tz ni vyema kusema mkenya ali fanya hiki ama lile kudhalilisha mtz.
Bila evidence ni projo na maneno ya uchochezi tu kutafuta likes tu.