Ujambazi Mlimani City

Wadau, habari;

Hapa maeneo yetu kuna msiba umetokea. Marehemu ameuwawa na majambazi. Alichukua fedha (milioni 10) kutoka Benki mojawapo hapa Mlimani City na kuanza safari ya kuelekea huko Salasala ambako alikuwa na shughuli ya ujenzi inayoendelea. Majambazi walimfuata kwa nyuma, walimpita na kumzuia kwa mbele. Majambazi walimtaka atoe 10M aliyochukua Benki kabla ya kumpiga risasi. Walikuwa wanafahamu kiasi halisi kilichochukuliwa!

Siku kama 5 kabla ya tukio hili, tukio lingine lilitokea eneo la Bamaga (mkabala na Hongera bar). Mtu na mke wake walichukua fedha toka benki hapo Mlimani City (13m). Majambazi walimfuata kuanzia hapo Mlimani city hadi huko Bamaga na kumtaka awape fedha. Kumbe alikuwa amezitenganisha; aliwapa laki 5 lakini walipatwa na hasira na kuhoji fedha nyingine ilikuwa wapi. Walimpiga risasi begani. Mke wake akawaongezea laki 1; naye alijeruhiwa kwa risasi wakidai “tunataka milioni 13 zote”. Pona yao ni kuwa fedha walikuwa wameificha kwenye booth. Baada ya kuona muda unapita majambazi wakaondoka. Na kwa bahati nzuri majeruhi walipona. Cha kushangaza ni kuwa majambazi hawakujifunika nyuso zao wala hawakuwa na wasiwasi wa kujificha hata kidogo.

Huko nyuma, jirani yetu mmoja (Mama-Joshua) alichukua milioni 4 hapo hapo Mlimani City. Baada ya kufika kwa Kakobe, majambazi walimpita na kumsimamisha baada ya kujifanya kuwa wanamjua. Baada ya kusimama walimtaka awape “awape mzigo aliochukua benki”. Hivyo:

  1. Mlimani city ni eneo hatari sana kwa ujambazi; kuwa makini unavyokwenda kuchukua pesa hapo.

  2. Inaelekea wafanyakazi wa Benki wanashirikiana na majambazi. Hivyo, kitendo cha wewe kwenda kuchukulia fedha ndani ya benki (bulk cash room) hakiwezi kuwa ni cha siri;

  3. Epuka kuchukua fedha nyingi benki. Fanya malipo kupitia benki au njia nyingine mbadala;

  4. Kama una ujenzi, ni hatari kuwa na kawaida kuwapelekea mafundi fedha kwenye site; tumia M-pesa, tigopesa, nk.

  5. Kama umechukua fedha, usikubali kusimamishwa na mtu usiyemjua njiani isipokuwa kama wameku-block na huna jinsi ya kukwepa.

Mjulishe rafiki, ndugu na jamaa kuhusu changamoto hii ya kiusalama.

(Sent as received from another person).

Du hatari sana, milioni kumi tu inamtoa mtu roho…anaacha familia ikihangaika…ndio maana sinaga huruma na majambazi

Duh!..

Hii hatari

Namba mbili ni kweli kabisa kama baadhi ya polisi wanavyoshirikiana na majambazi kuibia watu.

Ok ila hii habari ni ya Mwaka 2015 December Mkuu.

wasiumize kichwa wachunguze hao wafanyakazi watataja hao majambaz

hela ya kumtoa mwenzio uhai Haina mwisho mwema Wala haikusaidii

Rip marehemu

mil 10 tu kweli unaua mtu?

Asante…

Nadhani hata kwa sasa inafanya kazi pia maana haya mambo ya kibenki yanatisha sana aisee

Hatare

Hii ni lazima CRDB BANK

Wambie wanaume wa dar,wanasubiri mini kuwawekea mtego?

CRDB ndio wanahusika na michezo hii. Kuna tawi lao pale Mbezi mwisho ambapo ukitoa mzigo wa maaana lazima majambazi yale kichwa!

Inasikitisha sana…

Hizo dili mara nyingi hufanywa na watu wa maBank humo humo ndani…

Ila siku hizi Bank nyingi zina utaratibu mzuri kidogo… ukiingia Bank ukishanga shanga askari anakufuata na kukuliza… ukikaa muda mrefu bila kueleweka askari anakufuata kuuliza tatizo ni nini…

Tofauti na zamani mtu anaweza ingia Bank akakaa tuu na kuzuga bila kuulizwa chochote…

Ila linapokuja suala la fedha kuna changamoto nyingi sana kwenye usalama…

Cc: @Mahondaw

Its so sad kwakweli

Huduma za kibenki ya malipo ya kimtandao yamerahisishwa sana siku hizi sasa sijui kwanini mtu ana risk kwa kubeba cash kiasi kikubwa hivyo