Huku kwetu Kwamtogole kuna binadamu wawili waliojaliwa kupata watoto. Binadamu hawa wanaishi kwa ndoa zetu hizi za mjini mradi vijijoleo vyenu vimegusana basi ndoa tayari.
Tusiwahukumu kwa hilo, lilikonifanya niandike hapa ni hili ka malezi ya watoto wao. Binadamu hawa hawapitwi na sherehe mjini hapa. Iwe ubatizo, maulidi, kipaimara, kumtoa mwari, kitchen party, send off, you name it.
Watoto hawa huachwa kila nyumba mradi tu wazazi wapate nafasi ya kufakamia bila na chakula cha bure. Wako radhi kubadili mabasi matatu mpaka Keko bwana akiwa amebeba wa kwake na bibi wa kwake. Na wakirudi Jumamosi au Jumapili walale kwanza mpaka pombe ziwatoke ndiyo wakachukue watoto wao.
Sasa huyu mtoto wa kiume ambae ana miaka saba sasa, juzi anamwabia mama yake kuwa shule hataki kheri atafutiwe bwana aolewe. Bibi yule chozi linamtoka hajui mwanae alianza lini kuingiliwa na wanaume wenzake.