Ulizaliwa USHINDE...

#1
Kuna wakati utakutana na kila dalili inayoonesha kuwa unatakiwa kukata tamaa; Huu ndiyo ule wakati unajiuliza hivi "niendelee ama niache?"

Ukifika kwenye hali hii inabidi ujilazimishe kujiambia kuwa: "Nakataa kukata tamaa"

Usiruhusu hisia za kushindwa zikufanye uanze kupoteza matumaini ya kule unakoelekea. Kumbuka kila lengo kubwa huwa lazima likutane na changamoto kubwa kabla halijafanikiwa. Siku zote Kumbuka washindi huwa wachache, kwa sababu watu wengi hukata tamaa mapema.

Ulizaliwa USHINDE na siyo USHINDWE...
 

Top