Umewahi kupiga mpenzi au kumtukana?

Je, umewahi kupiga mupenzi au kumtukana? alikufanya nini hadi ukaamua kumpiga au kumtukana au vyote? Mie sijawahi kumtukana mpenzi wala kumpiga. Ukitokea ugomvi huwa nachagua maneno ya kusema very careful ili baadaye nisije kujutia kile nilichosema. Kupiga mpenzi pia sijawahi sipendi mambo ya kumdhalilisha KE kiasi hicho hata kama kanikosea ni bora penzi lifikie ukomo kuliko kuanza tabia ya kumpa kipigo cha mbwa koko. Pia huwa nahofia kwamba unaweza kusema ngoja nimnase kibao kimoja cha uhakika hadi aone nyota. Pwaaaaa! kaanguka! inuka inuka na wewe! Labda kapata mshtuko hadi kufariki. Umeshajiharibia maisha yako kwa kuua bila kukusudia hivyo lupango inakusubiri.
[SIZE=5][FONT=times new roman]
Hebu shuka kwenye uzi huu utwambie kama uliwahi kumpiga/kumtukana (au vyote) mpenzi ME/KE na alikukosea nini hadi ukaamua hivyo[/FONT][/SIZE]

Kumpiga sio Mara moja.

What was the reason behind your decision Mkuu?

Kila nikinyanyua mkono wangu kutaka kumpiga huwa nasita kutimiza azma yangu, maana najiuliza akipanchi au kunirudishia nini kitafuata? Hapo ndo unapoweza kujikuta ukimharibu sura yake…

Naam Mkuu hapo ndiyo unaona umuhimu wa kufikiri kwa kina kabla ya kutenda maana mwisho wa siku unaweza kujikuta unajilaumu mwenyewe for the rest of your life kwa nini uliamua kunyanyua mkono wako.

Nimewahi tukanwa ila yaliisha kabla hatujatawanyika, na nilifanya kosa kweli hata wakati ananitukana nilikuwa mpole sana, na tulikuwa wawili tu chumbani, kupigwa Niliwahi kofi moja tu halafu sikuumia, sema mie mpole siwezagi kuongea mtu akiniudhi au nikimuudhi

Ati sio mara moja?! Nini inafanya umpige?!

Kitu ambacho sijawahi waza ni kumtukana mwanaume wangu, kwanza ni kujishushia heshima! Matusi karibu yoote ni kumdhalilisha mwanamke halafu mie mwanamke niyaseme tena!

Huwa nina tabia ya kuuliza kama kweli kosa ni lake, nimekosa mie naomba msamaha! Bahati na yeye akianza ugomvi huwa nanyamaza kwanza, mwanzo huona namdharau ila hasira zikiisha ndo naanza kumuuliza kulikoni?!

You’re one of the kind Sakayo. You’ very special in so many ways. Hata kule JF nilikuwa nakuangalia kwenye uzi wa ukakasi hujiondokea kimya kimya bila kutia neno na mara nyingi umefanya hivyo. Hongera sana kwa mrembo.

Thanks BAK
Hakuna kitu naogopa kama ugomvi!
Huwa naumia sana nikigundua nimemkwaza mtu sababu huwa najua maumivu ya kukwazwa! Kinachonisaidia huwa ni mwepesi mnoo wa kuomba msamaha jamani, hilo tuu!

Hongera sana. Ni nadra sana katika dunia ya leo kukutana na binadamu mwenye mtazamo huu. Wengi hukimbilia kutoa matusi ili kuridhisha nafsi zao. Nashukuru sana kutowahi kumtusi mpenzi wangu hata mmoja nilikuwa sioni umuhimu wa kutamka hata mshenzi au mpumbavu achilia mbali matusi ya nguoni.

Hongera mnoo jamani
Wanaume wa miaka ya leo matusi yako mkononi!

Ngoja niwe msomaji

Aisee

Bado

Ndiwooooo

Polee

Naogopa sana ugomvi sitaki hata kuusikia.

Funguka dadaake acha hizo!

Nimewahi kupigwa jamani kumtukana mwanaume hapana nikiwa na hasira huwa nalia tu mm