Usafiri ulisumbua njiani ila nimefika salama

Habari wakuu
Nimefika salama katika safari yangu yakutokea JF hadi hapa Kenya talk ila usafiri ulinisumbua sana pia walinzi wa mipakani nao walinidokezea rushwa lakini niliwapiga Chenga kwakuwapa pesa bandia
Na vile vile nikawapoteza ninakoelekea hawawezi kunikuta maana sijaacha footprints

Hongera na karibu sana mkuu.

Ni mimi ndugu yako,
Mtoto wa soda

Nilianza safari 5 days ago lakini jana ndio nimefika sasa

Karibu mkuu,
Ulipitia wapi? siku 5 nyingi

Nashukuru sana ndugu yangu shangazi yako anakusalimia sana

Nashukuru ndugu, mwambie Shangazi salamu zimefika. Usisahau kumwambia mjomba JF imehamia Kenya.

Pole kwa uchovu wa safari. Ya ugenini ni shwari

Nilishampa taarifa kabla sijaanza safari yangu na yeye ndie aliniwekea vitu vyangu kwa ajili ya safari na akanitakia safari njema pia kazi njema kwa sehem yangu mpya ya kazi ila alisihi sana niwe makini zaidi ya kiwango

Shukrani sana mkuu

Karibu sana Mzee Baba

Mie kidogo nirudie njiani maana lile li “ROBOT” kila nikichagua picha lina zengua zengua

Lile linazingua sana