USIKUBALI KUGEUZWA FURSA MDEBWEDO

Mtu ‘akikuvamia’ na kukuaminisha kwamba kuna fursa imetokea Mjini ambayo inatajirisha fasta, na kwamba ukiikosa tu basi ndio umepotea kiuchumi, uwe na hakika umekutana na mtu ambaye aidha hajui anacho kisema au kaamua tu kukudanganya. Kwa usalama wako tu, timua mbio zisizo za hapa, ikibidi hata viatu vyako abaki navyo!!!
Hapo kilichopo ni yeye kutaka ‘kukupiga’ kwa kukugeuza wewe ‘fursa mdebwedo’.

Kimsingi, hakuna kitu kilicho kingi duniani kama fursa, kwa sababu fursa za kiuchumi zinatokana na kutatua matatizo ya watu. Na matatizo hayataisha maadamu mwanadamu anaishi. Tafuta tatizo unalo weza kutatua kwa ufanisi, nasi hatutafanya hiyana, tutakulipa ‘mapene’ yako kiroho safi!!!
Akili za kuambiwa, changanya na zako.

[SIZE=5]pumbavu kabisa, mjinga wewe.
Uoga wako ndio umasikini wako.
Unajua Qnet??? Uliisikia D9 club???
Watu walioingia mwanzoni wamepiga mpunga wa kutosha wamejenga majumba na kununua magari (nina Rafiki zangu wawili walianza Qnet kimasihara kubabake sasa hivi nawatamania kinyama)[/SIZE]

[SIZE=5]Uoga wako umasikini wako.
If you don’t take risk, poverty will there with you till we dump you under your grave.[/SIZE]

Take risk,cha msingi kujiongeza…akizubaa unampiga ata uyo uyo anaetaka kukufanya fursa

Nimekumbuka kitu…huu ndo muda mzuri wa kuwafundisha wakenya Forex :):slight_smile:

The higher the risk the higher the profit and viceversa.

For sure

Hahaaa changamkia fursa mkuu.

Kule home tulikuwa tunaambiwa kuna mentor wanatoka Kenya ila nimepita kwenye majukwaa yao hakuna kabisaa story za Forex ngoja nichangamkie fursa.

Hahaha Forex na Ontario labda mentor wa Kenya ni @mk254.

W

Walianza mapema zaidi yetu…unaambiwa hata kubet wako mbali sana na betting kwao imekuwa kama addition kwa vijana na watoto.

Ontario na kina Cre walishaenda kenya walialikwa na willy tuva aka mzazi wa citizen radio yule wa mseto ea…wakakuta kona zote wanaijua forex wakarudi kapa.

Na wewe si ungejiunga ujenge hayo majumba…

[SIZE=5]ndio nishajiunga, na mafanikio nayaona.
Umesikia wewe fukara wa pesa na mawazo???[/SIZE]

Daaaaaaa

pambaneni, mie ngoja nifuge na kuuza nyie endeleen huko ntakapofikia mtanijuza

Ukiona unaitwa kwenye fursa jua wewe ndio fursa

Kila member wa hizo kitu Huwa anasema rafiki yangu katoka,yaani hizo fursa anatoka rafiki yako we kutoka ni ngumu

Wengi mlioingia huko Mna stress sana naweza soma hapa jinsi unavowajibu watu

Pesa nyepesi nyepesi zina uongo ndani yake msidanganyike sijui bitcoin pambana na kilimo chako tu

Tunataka reference ya uaself sio rafiki yako ili tusione nawewe ni fursa mdebwedo

Risk una take kwa kitu ambacho umbo sure nacho then faida na hasara zitakuja on process sio ku take Risk wakati unajua kabisa unatapeliwa

Akili za kimasikini ni kuaminishwa kitu na mtu na kutaka hela kirahisi bila kufikiria.

“If you think small, you will remain small for a life”.