UTARATIBU WA KUAGIZA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI

Salamu wakuu.

Naomba kujua procedures za kufuata ili kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi (Importation). Nimesajili company tayari, bidhaa zangu nyingi nategemea kununua kutoka nje ya nchi hasa SA, China na nchi nyingine. Naomba kujua A,B,C’s za kufuata…natakiwa kuwa na nini na mahitaji hayo nayapata wapi.

Natanguliza shukrani.

Yaani wewe “President Of The United States” haya huyajui? Ha ha ha haaa ngoja waje!!

Hahaha, Mr President hajui kila kitu mkuu. Nahitaji sana msaada wa hiyo kitu.

Ni kweli mkuu, hata jiwe anajidai kujua kila kitu lakini holaaaa!! Watakuja mkuu ingawa wengi tumewaacha home hawajafika huku Kakuma refugee camp!!

Wakuu mbona uzi muhimu ka huu hatumwagi mambinu ya kuagiza? wanaojua tafadhali saidieni

Mim najua jinsi ya kuagiza vitu vdgo vdogo tu kutoka aliexpress,ebay,amazon

binafsi najua hivyo hivyo ila najua kuna watu wengi wanajua namna ya kuagiza vitu vya kibiashara ila wamekuwa kimya dah,

Unataka kuagiza nini? Nadhani kila bidhaa zina taratibu sake hapo Tanzania, mfano bidhaa za matumizi ya binadamu kama chakula,mafuta ,dawa na vifaa tiba lazima usajili TFDA kwanza. Utapeleka sample zikiwa na documents au vyeti vya usajili toka kwao ili TFDA wapime kisha watakupa cheti cha usajili wa bidhaa yako.Baada ya hapo unawe kuleta mzigo.

Ahsante Sana mkuu

Watanzania wengi hatupendi kupeana michongo ya bihashara, hata apa kariakoo, ukimuulizia MTU ishu ya bihashara lazima udhurumiwe. Hakuna agents wa kueleweka apa Tanzania wengi wapo kiwiziwizi tuu na kutapeli,
Labda kwa wenzetu Wa mataifa yaliyoendelea

HILI SWALI BILA SHAKA LIMEMLENGA MFANYA BIASHARA TENA MKUBWA(JUMLA/AGENT) AMBAO WAKO BIZE SIZAN KAMA WAKO HUKU KUKUJIBIA KIUFASAHA…MIMI NIKUTAKIE TU KILA LA KHERI NAMI NI MHANGA WA ILO TATIZO WABONGO KUPEANA MCHONGO YAN NDIO TUMESHINDWAGA HAPO

Sio sema unataka kuingiza Nini ili upewe elimu nzima maana kila bidhaa INA utaratibu wake kuna bidhaa zenye kuhitaji leseni na zenye uhitaji vibali na document