Uzi wa kusimulia matukio ya kuwakimbia wanaume wanaotisha baada ya kumkuta ndivyo sivyo!

Demiss

Senior Villager
#1
Nimeamua nihamishie huku huu uzi kutoka jf.
Haya tuende kwenye tukio lenyewe lililonikuta Demiss miye.
Huyu ni mkaka wa IG huko ameweka picha zake za self tu ni handsome balaa sijapata kuona nakwambia alianza kwa kulike na kucomment picha zangu mwisho wake akahamia DM.
Hili tukio lilitokea mwaka jana kabla sjapata kuwa na mahusiano na Mganga.
Tukabadilishana mawasiliano tukawa tunawasiliana akafunga safari ya kutoka Dar kuja Dom tukutane.


Mtoto wa kike nikaupara vya kutosha jaman naenda kukutana na handsome wa ukweli.
Akaniambia amefikia royal village hotel basi nikachukua kibajaji mpaka royal hotel nikaenda kukaa pale ngalawa nikisubiri handsome ajee tukutane.


Ghafla akaja mkaka mfupi anafika kiunoni kwangu ana mikono mirefuu na miguu mirefuu jaman lakini ni yule wa kwenye picha alafu ana kibiyongo eeeh mungu nisamehe Demiss miye.
Nikainuka nikaanza kuondoka nikasikia nyuma ananiita Demiss nilijua tu utanikimbia tafadhali rudi basi hata tuongee tu mimi wallah sikugeuka nyuma nikasema mungu nisamehe sijui nilitendalooo.
Baada ya hapo nilitumiwa sms za laaana sijapata kuona jamani.


Nisingeweza mimi jamani uwiiii eeh mungu unisamehe nilikuwa sijui nilitendalo nina dhambi mimi jamani.

Demiss Malaikaa.
 

Mtu chake

Senior Villager
#15
Hizo laana hazijawahi kukurudia?!
Binafsi siwezi mkimbia mtu hata aweje, ameshafika ndo huyo ni kubadilishana mawili matatu tuu kwani atakubakaaa???

Huwa inaumiza sana jamani, kwa nini ukimbie???
Kukimbiwa au kuoneshwa dharau kuwa wewe ni taka taka,huna hadhi ya kuongea nae ,huwa inauma sana
 

Top