Vituo vya Polisi Hasa Mwanza ni Tishio kwa Rushwa

Hakika sasa ni aibu tupu katika hivi vituo vya Polisi jijini Mwanza. Sasa hivi watu kubambikwa kesi na kukaa lock up za Nyamagana na Kirumba kwa siku hata 20 ni jambo la kawaida na kinachotakiwa ni fedha tuu ili upewe dhamana.
Ni jambo la ajabu kuwa hali hiyo anaifahamu RPC Msangi, RCO, ma OCD wote na hata wakuu wa vituo na hakuna wanachojali nadhani kwa vile Rais alitoa tamko kuwa Polisi fanyeni muwezalo yeye anaunga mkono.
Nimefanya utafiti na kuona hali ni mbaya sana na hawaoni aibu kutaka chochote huku wakisema toa za kutosha tuwatoe na wazee pia. Jee hivi ndivyo nchi ilipofikia? Rushwa nje nje kuliko wakati mwingine wowote na bado kuna watu wanasema eti Magufuli anapambana na rushwa nchini? au kwa jeshi la Polisi ni halali kama alivyosema fela za kubrash viatu? lakini mbona wamepitiliza?
Nitawauliza wenyeji wa Mwanza wanipatie majina ya hawa maofisa wa polisi wala rushwa ya vitisho na kuyaweka hapa labda itasaidia kabla sijarudi zangu Dar. Hasa idara ya CID

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Tatizo Jiwe huwa anatoa kauli bila kupima madhara yake baadae yatakuwaje.

Huwezi kuwaambia polisi fanyeni lolote nitawaunga mkono, haya ndio matokeo yake ya kupewa kiburi na Jiwe ambapo yanakuwa ni mateso kwa wanyonge, kwa hali hii tusipopanza sauti tutaumia sana.

Tangu lini mla rushwa akapiga vita rushwa? Moja ya dalili na viashiria vya mla rushwa ni kukiuka sheria zote zinazohusiana na uwazi na uwajibikaji. Anaepiga vita rushwa hawezi kujitoa kwenye mikataba inayohusiana na good governance na transparency. Anaepiga vita rushwa hawezi kufanya manunuzi bila kuheshimu public procurement act.

Aibariki kwa kipi cha Maana wanafunga midomo vyombo vya habari kama Jamii Forum.
Sasa ivi tupo uamishoni

Halafu unalisikia jitu zima linasema eti jiwe amemaliza rushwa kuwa sasa hakuna rushwa!!!nikamwambia kama upo shambani unalima tu hujakutana na shida ya kwenda polisi,mahakamani,hospitali na ofisi yoyote ya umma utajidanganya kuwa rushwa imekwisha ila ngoja yakukute

Rushwa kutokomezwa ni kazi sana…

Wenye dhamana ya kusimamia hizo sheria wao ndiyo wapo mstari wa mbele kuzivunja…

Cc: @Mahondaw

Ndio maajabu hayo!

Siyo Mza tu… Kila nimuonapo Polisi ni kama naiona rushwa vile!!!

!
!
Sijawahi Kuona Kituo Hakina Rushwa

Polisi nchi hii hawana tofauti kabisa na polisi wakikoloni wa enzi za kabla ya uhuru

Ila Mwanza imezidi