Wabongo na vihere here vya visivyowahusu!

Wanajamii walio wakimbizi walio wanavijiji!
Nawasalimu sana!

Mada tajwa hapo juu inahusika sana!
Naomba niende katika Mifano halisi!

Mfano wa Kwanza!
Kuna siku nikiwa katika mishe mishe za kutafuta Mkate wa kila siku, nikawa na mchongo flani wa hela ambao wadau walitaka tukutane maeneo ya Ubungo, pale UDSM Hostel nyuma ya NBC Ubungo! (Safari iliontoa home haikuwa ya Kwenda Ubungo) Wadau wa mchongo ule walikuwa mmoja –ke na mwingine –me! Ikatokea wa kwanza kufika eneo la tukio ni -ke! Tukiwa tunavuta muda huku tukiwa na Coca na story za hapa na pale, ili column itimie, simu yangu ikaita, kucheck wife! Kupokea anauliza uko wapi? Nikamjibu Ubungo! Uko na nani? Nikamjibu niko na Stellah! Mnafanya nini? Nikamjibu niliekaa nae umemuona lakini tunachofanya hukioni? Basi kama upo karibu unatuona, njoo tujumuike ote hapa, huwezi endelea tu kutuona mpk mwisho wetu, km kuna dish umeset liambie dish lako likamate matukio yote mpk mwisho! Mshkaji akaja, tukaweka mipango vizuri, tukatawanyika!

Mfano wa Pili!
Nina mshkaji wangu anafanya kazi SIDO HQ pale kona ya kwenda Mzumbe Univ na jirani na Mzizima School (nadhani)! Huyu mwana huwa ananipa sana connections, kuna siku akaniita pale ofisini kwake, nikawa natembea mdogo mdogo kutokea DIT kupitia REGENCY Hosp (sifanyi kazi Regency Hosp) kuelekea pale SIDO, nikiwa maeneo ya Regency Hospital nikamuona Old school friend, mdada! Wakati nabadilishana nae maneno mawili matatu, simu inaita! Kucheki wife! Slim5 nani mgonjwa hapo Regency? Nikachoka!

Moral of the story:
[ol]
[li]Wake zetu muelewe kuwa, hii mikate tunayoleta nyumbani, inatoka njia nyingi na sio lazima njia zote mzifahamu, kwanza baadhi ya njia hizo ni temporary, zingine tunakuwa tumebet![/li]
[li]Kuna michongo mingine tunaiset humu mitaani, haina uhakika kama KARATA 3 ama Chafu 3! Kuna kula na kuliwa, ikitokea tunabutua, tunasema, tukiliwa tunakufa na maumivu yetu![/li]
[li]Wake zetu mjua huwezi kuambiwa mitego isiyo na uhakika wa kupiga hela! Hamkawii kutibua coz baadhi yenu ni roporopo! Kuna baadhi ya deals ukiwa roporopo zinabuma![/li][/ol]

Na nyie mnaowapa wake zetu taarifa za matukio yanayoendelea mitaani, nani kawapa authority hiyo? Ni lini tulikuteua kuwa PRO wa ndoa yetu?
Nyie maojifanya wema sana wa kuwapa taarifa wake zetu juu ya misele yetu, muwe mnawapa taarifa kamili ili kuwasaidia, msiwape nusu nusu!

Naomba kujua, kwa utoaji wenu huu wa taarifa za kiuchochezi ambazo hata TCRA wanakataza, huwa mnatarajia Malipo gani? Kama hamna Malipo nini hasa huwa mnakitafuta?

Nimewasilisha tu!

aiseee ndo nimejiunga leo nina mchecheto hatari,ngoja nikazurure nitakuja kusoma hii yako

Binadamu ndivyo tulivyo, ila wife wako ako na mCID mob sana! Na wewe jirani kila makutano ni ke tuu unanipa wasiwasi ujue!

Ninahamu ya kujua kilicho kuwa kimeandikwa kwenye paragraph # 2&4

Take Care! Kwa watu huku!

Nakutafuta. Tukutane. Tuongee ile biashara.

Mkeo ako na wivu mbaya

Ila binadamu ni wambeya sana kutwa kushughulika na ya watu sijui wanafaidika nini

Pole sana mkuu

Viumbe wazito!

Ya dunia na malimwengu!

Mkeo akijua je???

Ntamubia hii biashara ndio ule mkate anaonipokeaga!

Mkeo ni mtata sana…
Wacha lile dili liyeyuke tuu

Daah. Kashaniponza

Mkeo atakuwa anakusaliti sana mkuu.

Mwizi hakuna kitu hapendi kama kuibiwa.

Yajayo yanafurahisha sana:D:D:D

Kama nimekuelewa, ni kwamba mkeo ndio mwenye kihere here, kakuwekea PI …
lazima ulikosea mahali ndio maana anakufuatilia…

Mkeo anajipa stress sana

Inaonekana ana muda mwingi bila kazi ya kufanya.

Hahahaha… mleta mada.