Waislamu na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

WAISLAMU NI NDUGU.

1)Alisha amuru Mungu,tunapaswa kuungana
Tena tuwe na uchungu,pale tukikwaruzana
Na tuyaache majungu,tusije pata laana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.

2)Na dini yetu ni moja,kwanini tunatengana
Maadui watungoja,sisi tuanze zozana
Wavunje wetu umoja,wao wazidi shikana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.

3)Kwanini Shia na Suni,Arabuni mwauana
Mnapigana kwanini,wenyewe mwamalizana
Wapi yasema Qurani,mlipaswa kuchinjana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.

4)Tusomeshaneni dini tupate kusikizana
Turejee vitabuni,huko tutaelewana
Tuingie darasani,na kwa hoja kushindana
Yatupasa kuungana,waisilamu ni ndugu.

5)Na Dua tuombeane,tuache kuchukiana
Na wala tusigombane,Bali kuelimishana
Mapungufu tujuane,daawa tukipeana
Yatupa kuungana,waisilamu ni ndugu.

SHAIRI-WAISLAMU NI NDUGU.
MTUNZI-Idd Ninga,wa Tengeru Arusha.
+255624010160
[email protected]

tamaa zao na kusalitiana ndio vinawaangamiza

achaneni na ujinga wa dini waafrika nyinyi
maandiko ya kwenye vitabu vya dini ni moral teachings na sio maneno ya mungu
acheni kupoteza muda

Hili ni jambo muhimu

Hmm!..

Ata martin Luther naye alikuwa na tamaa, na ndio maana alihasi ukatoliki.

wengi wA dini hiyo hawana elimu wApo busy Kuwaza bikra 73 akhera na mito ya pombe isiokauka

Duh! Umeongeza idadi si wanasema ni 72 au ni typing error.

ila hawapigani wao kwa wao

Umewakumbusha vema

ni ,73 mkuu
yaan kukosa elimu ni janga,eti kufuga ndevu ni Baraka,Kuvaa kanzu pia ni Baraka

Wakristo kama kawaida yenu.

Hamuwezi kuficha hisia zenu za chuki kwa waislamu.

Mpo ugenini lakini mnachanua makucha na kuonyesha tabia zenu za chokochoko dhidi ya waislamu.

Sijaona waislamu wakianzisha uzi kuwasema wakristo au hata kukosoa.

Tatizo siku zote linaanzia kwenu,waislamu wakiwajibu mnasema wakorofi.

Bhahahaaaa

Hahaha mi simo.

msema kweli hukimbiwA na rafiki zake,nikipatwa na ajali kama hiyo ctaona haya"_hayati shaban Robert

Aisaee