Wakitubana Tz tuhamie hii Yetu ya Kenyatalk tupeane updates za Uchaguzi.

Ule muda umewadia watanzania wenzangu. Tuje huku KenyaTalk na kuendelea kupeana Updates maana huko Kwetu hawataki tena tupate mawasiliano.

Watanzania tuhamie Kenyan talk kupata update uchaguzi.JF ipo slow sana nadhani ni sehemu mkakati wao wakoloni weusi

Huku JF Tz wameibana toka jana mchana, lengo ni kutuzuia watu kupeana habari za huu uchaguzi uliokuwa unafanyika. Lakini kwa bahati mbaya uchaguzi wenyewe umekuwa na wapiga kura wachache sana. Ni uchaguzi ambao wananchi wameonyesha kutokuridhishwa na mambo, lakini hawana la kufanya, huku wakilizimishwa kuishi kwa amani ya shuruti.

Mkuu tetesi za matokeo ya ubunge kwa baadhi ya majimbo zipoje?

Mbeya Mjini Tulia
Mbowe Chali

Arusha Udiwani Wote umeenda CCM

Ccm wameshinda kote mpaka sasa kwa matokeo yanayoendelea kutangazwa. Kilichofanyika ni idadi ndogo sana ya wapiga kura, huku wapiga kura wengi wa upinzani ndio hawakupiga kura, kutokana na kupoteza imani kabisa na zoezi zima la uchaguzi. Sehemu zote wanazotangaza kwenye vituo vyenye wapiga kura 400+ hakuna popote wamefika wapiga kura 170! Mbowe ni mmoja ya waliopoteza jimbo. In short hakuna mpinzani hata mmoja aliyeshinda so far.

Kwa idadi ya wapiga kura wachache waliojitokeza, sioni mpinzani yoyote akishinda, maana kwenye hao wachache, wengi ni wapiga kura wa ccm. Ile idadi ya wapiga kura 29m+ nilifahamu fika ni fake, na uchaguzi huu umedhirisha hilo.

Du! Tanzania yetu inarudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Kama hakuna upinzani wa nguvu bungeni chama chetu pendwa kitajiamulia kitakavyo bila kujali maslahi ya wananchi

Ni jambo la hatari kabisa, maana nchi imeshurutishwa kurejeshwa kwenye utawala wa chama kimoja bila ridhaa ya wananchi walio wengi, ila kwa utashi wa rais aliye madarakani! Hii imetokana na katiba iliyo na mapungufu ya wazi. Inawezekana kuonekana ni jambo la sifa kwa watakaotangazwa washindi, lakini ni jambo la hatari na litakaloigharimu sana nchi yetu kwa siku zijazo. Muda utakuwa muamuzi wa hili.

Ila hili la kuzimiwa huduma za mitandao ya kijamii linakera sana.

Lengo la kuzima mitandao ni ili kutekeleza hujuma bila jamii kuhamasishana kupinga hujuma hiyo.

Wafanye wafanyayo gizani lakini mwisho wa siku yatakuwa nuruni na historian watayaandika katika vizazi vjavyo

They don’t care as long as wako madarakani.

lakini watanzania na waganda wamekaliwa…

Yani ni hatari.

Kweli kabisa boss, tumerudi kama wakati wa Moi huko Kenya.

Nisafishe macho dada. Huko kwenu ukipata magumu, njoo huku kwangu Nairobi. Nitakuhosti.

Jamani tupeane VPN apk huku maana tumefungiwa

Kuna iitwayo Proton VPN, hata hivyo huwezi kudownload na kuinstall maana wamebana kufanya verification.

Nchi yetu imekua ya kipumbavu sana.

Namchukia sana the so called jiwe.

Kuiba liibe na mitandao liiandame.

Jamaa mshamba sana .