Wale watoto wa mtaani ni nani anawafundisha maadili?

Ni jukumu letu kama wazazi kuwafundisha watoto maadili, dini, na ustaarabu utakao wawezesha kuishi na kushirikiana na wenzao kama binadamu waliostaarabika. Kuna tabia kama kutokuongea wakati wa kula, mtoto kutomuongelesha mkubwa mpaka aulizwe swali au awe anataka kufahamu kitu aulize swali, kwenda msalani si kwa haja ndogo na kubwa tu hata kujamba unatakiwa ujambie msalani. Kunawa mikono unapotoka msalani, kabla ya kula, baada ya kucheza na wanyama kama mbwa na paka, kutandika kitanda. kufua nguo zako hasa za ndani.

Watoto wa kike hasa wanapopevuka hutakiwa kufunzwa usafi na taratibu za kubadilisha mataulo, jinsi ya kuyahifadhi na mambo kama haya. Ni nani mwenye jukumbu la kuwafundisha haya wale watoto wa mtaani?

Sky Eclat kwenye ubora wako… ikiwa hata pa kulala hawana hayo maadili watayafanyia wapi?

Hilo ndiyo tatizo kubwa, kama hatujaweza kuwatatulia yale mahitaji makubwa ya binadamu ambayo ni
Chakula
Malazi
Mavazi
Hewa na maji safi ya kunywa
Matibabu
Elimu.

Hapo kwenye hewa sijaafiki…

Mkuu… Naomba utambue kwamba kwajinsi mabadiliko ya Dunia yanavyo pelekea/sababisha uchafuzi wa hewa Safi… Moja kwa moja, nijukumu la mzazi/mlezi/serikali kuhakikisha mtoto anapata/vuta hewa ilio safi.
Kumbuka hili sio jukumu ama sio mpango wa Mungu kwamba watoto wale wavute hewa chafu ama ilio haribiwa na binadamu.

Inamaana unaafiki mlundikano wa watoto kwenye chumba kimoja bila kuzingatia ukubwa wa madirisha na idadi ya watoto?

Tabia nzuri ni kitu cha asili kwa binadamu,upendo,hofu ,kujali nk. Shida ni kwamba mazingira wanayoishi yana waongezea na tabia hasi kwa wingi.

Jamii ina changamoto nyingi sana na kola mmoja wetu anatakiwa asaidie kwa kadri anvyoweza japo hatuwezi maliza changamoto zote.Nakumbuka kisa cha YESU alipokwenda kwenye kisima ambacho watu walikua wakitumbukia kila malaika alipotibua maji, alimponya mtu mmoja tu kati ya mamia.

Kuna limits katika hatua tunazoweza kuchukua kutatua changamoto za jamii iwe umasikini,maradhi, watoto wa mitaani nk.

Mtaani its survival for the fittest, hakuna kuremba remba. Ukipata msosi ni kula kabla tu, tena upesi kabla haujakwapukiwa. Ustaarabu na maadili yanawekwa pembeni. One has to be completely ruthless.

Lipo tatizo Mie naenda direct kwa jawabu mmbadala ,Kila mkoa pawe na shule ya kijeshi,kupokea watoto wa kawaida na wa mazingira magumu ( Yatima na watukutu.Tuwe na sheria ngumu za malezi,watu tunawazalisha wadada na kuwatelekeza.Tunafanya dhambi kubwa kulea tatizo hili.

Ni jukumu letu sote

Hapo ni Mungu tu ndio anayejua.

Wengine wanakujaga kuwa waadilifu ila wengine ndio hivyo.

Ulimwengu utakua unawafunza maana wanasemaga “asiyefunzwa na mama hufunzwa na Ulimwengu”

Mimi kama mlimwengu sishauri mwanao afunzwe na sisi vile hatutoi nafasi ya pili, hatuna msamaha wala aibu bora afunzwe na wazazi wake, sisi ni sheria mkononi otherwise FALSE

Hahah!! Nikweli walimwengu hamna maana kabisa

Hakika mkuu walimwengu sisi ni vitendo hatuna maswali sisi ni hukumu Only. hatuna muda wa kukufundisha

Hua najiuliza Wizara yetu inayohusika na maendeleo ya jamii jinsia na watoto pamoja na kua na budget kubwa tu kuliko wizara nyingi kazi zao ni zipi hasa kama hawawaangalii hawa watoto ambao kwakweli ni jeshi la hatari sana likiachwa kukua katika hali hiyo ya kukosa maadili. Wanakosa maadili ya kijamii(manners),ya kinchi, kidini na kiutu(human values) kwa ujumla. Waweza kutana na mtoto wa mtaani anavyoishi katika mazingira magumu na ya hatari halafu ukamlinganisha na mwanao, dah! roho inauma sana kwakweli

Kwanza kabisa ile wizara ni kubwa sana, pili afya inapewa kipaumbele kuliko ustawi wa jamii.
Tatu wale wahitimu wa Kijitonyama kila mwaka huwa wanaajiriwa na nani?

Wizara kweli ni kubwa maana hiyo idara ya maendeleo ya jamii pekeyake majukumu yake ni makubwa. Kama watunga sera wangekua na vision na focus wangetafuta solution kwanza ya kulipa muongozo wa kimaadili jeshi hili la watoto lakini pia kufanya juhudi za makusudi za kuhakikisha wanapunguza kama sio kuondoa kabisa sababu zinazopelekea watoto kujikuta katika mazingira hayo. Kwa mtazamo wangu Sky serikali haikupaswa kuliacha jukumu hili kwa wazazi wasiowajibika peke yao maana wenyewe(wazazi) ndio chanzo cha tatizo. Ingechukua hatua kama ambavyo sasa wanachukua hatua kushughulika na kupamabana na UKIMWI kwa kuhakikisha watu wengi zaidi wanapima kujua status za afya zao

Hufunzwa na walimwengu… the tough way…

Cc: @Mahondaw