Walioishi Uswazi Vs Ushuani tukutane hapa

Hi,

Najua hapa wapo watu waliokulia maisha ya Kiswazi.

Pia wapo waliokulia Ushuani, mageti karee wapo pia.

Mje hapa mtueleze maisha ya ushuani na uswazi, vyakula vyao na vituko vyote vya uswahilini na ushuani.

Mi naanza na Uswazi…ukifua nguo inabidi uilinde mpaka ikauke…ha ha haaa…ukichomoka tu…inaibiwa.

Tiririka na wewe…

Ushuani nimeishi udogoni, uswazi ukubwani kwa sana…
Ushuani kuna akili za darasani, uswazi ni chuo cha maisha
Watoto wa uswazi ni more creative linapokuja suala la maisha kuliko ushuani

Kweli kabisa mkuu…

Uswazi watu hawafanyi kazi lakini wanaishi, asubuhi ukitoka unawapita kijiweni kinamama vibarazani na jioni ukirudi wako palepale. Halaf uswazi tunafuatiliana sana.

Ushuani hatuna vituko kama uswazi sema huku tuna miss ule ushirikiano kama wenu huko kwamba mnaweza kushare vitu na jirani, huku kila mtu na lake ata jirani humjui labda unajua gari lake tu

Nilipokua mdogo ndo niliishi ‘ushuani’ kuhusu msos nilikua nachagua sana chakula, maharage nakunywa mchuzi tu mchuzi ukipika nachambua vitunguu natoa nilikua nikiona pilipili hoho kwenye mchuzi nishashiba, mihogo sikua nakula viaz sili yan nilikua kama fito nilipokuja kuishi maisha bila ya baba ndio nilipojua uswaz kukoje sikuchagua tena nabugia tu

Kijijini ni ushuani au uswazi? Maana nimeishi bukililo

Sawa wa ushunani

I second you Bro

Hivi upo?

Hahah!! Sawa sawa

Wewe uko upande gani lakini?

Hahah!! Nipo aisee, vipi?

Mm mswazi maa

Salama kabisa

Kumbe wewe wa kiembe mbuzi kama mimi haha

Mm kwa mtogole uku kwa tumbo najuaga we ni wa ushuani ujue

Ushuani wapi wewe mie wa kiembe mbuzi