Watanzania Tunamshukuru na Kumkubali Sana Rais Uhuru Kenyatta, Vipi Wenzetu Mnamkubali Rais Magufuli?

Hi Neighbour Brothers and Sisters of Kenya.
hili ni bandiko la swali ,
huu wema wa Rais Kenyatta kuturudishia dhahabu yetu,
Je Rais Uhuru Kenyatta Amethibitisha Kuwa Kenya ni Jirani Mwema?, ni Mshirika Mwema wa Ujirani
mwema wa Jumuiya ya Africa Mashariki, au bado ni mshindani baada ya kulegalega kwa “the coalition of the willing”, Uhuru ameamua kufungua the new frontiers?.

Jee Wajua Rais Magufuli, Japo Hasafiri Sana safari za overseas , Lakini ni Master Diplomat
on his own Way?.

Tuanze na Uhuru Kenyatta.
Kuna msemo wa kizungu unaosema, " you can choose your friends but you can’t choose your neighbors", ukimaanisha unaweza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua majirani.

Kitendo alichokifanya rais Uhuru Kenyatta cha kuturudishia dhahabu yetu, ni kitendo cha kustahili pongezi za dhati, na hivi ndivyo Uhuru alivyo kwa maneno na matendo.

Niliwahi kumbump Rais Uhuru Kenyatta mahali, wakati
huo hata rais Magufuli alikuwa bado hajawa rais, nilifanya nae mahojiano kidogo ya impromptu kuna kitu alikizungumza kuhusu ujirani mwema

https://www.youtube.com/watch?v=VS3dGmNY1XQ

Hivyo huku kuturudishia dhahabu yetu, japo kwa wengi itaonekana ni matokeo ya ile ziara fupi lakini muhimu ya Chatto, lakini kwa sisi wazoefu wa mambo alichokifanya rais Kenyatta ni kuyaishi tuu maneno yake na dhamira yake ya dhati kuihusu Tanzania na ujirani mwema, licha ya kumpokonya tonge la Bomba la mafuta la Uganda, toka mdomoni kwake, na kuivunja ile “the coalition of the willing” ya Kenyatta, Museveni na Kagame kwa Magufuli kufanya urafiki na ujirani mwema na Rwanda na Uganda, hivyo kuiathiri SGR ya Kenya. Alichokifanya Kenyatta ni Diplomacy ya hali ya juu sana.

Ili uweze kuishi kwa amani, ni lazima uishi vizuri na majirani zako, hata kama kuna maeneo mnatofautiana, au mlitofautiana huko nyuma, lazima muwe marafiki, befriend majirani zako wote waliokuzunguka, kiukweli katika eneo hili la kujenga ujirani mwema Rais Magufuli is doing good.

Magufuli alipoingia tuu, kati ya nchi majirani 8 zilizotuzunguka, rais Magufuli ameisha zitembelea nchi nne, amekwenda Rwanda, Kenya, Uganda na Malawi, pia alipanga kwenda Zambia, tetemeko la Bukoba likakatisha ziara yake, bado DRC, Burundi na Msumbiji, hivyo japo rais Magufuli hasafiri safiri sana ziara za nje ya nchi za mara kwa mara, lakini hizi ziara chache anazofanya, au marais wa nje wanaotembelea Tanzania ni very strategic kwa maendeleo ya Tanzania, hivyo rais Magufuli ni a master diplomat on his own way, kwa sababu, wanaomatter kwa ustawi wa Tanzania, ni majirani zetu waliotuzunguka na sio nchi mapebari na mabeberu za ulaya japo fedha za mabeberu bado tunazitegemea sana kwenye general budget support yetu.

Tanzania tukijiimarisha kikamilifu kwa ujirani mwema, Tanzania tuka take advantage ya
soko la Africa Mashariki na soko la SADC, amini usiamini, hatutazihitaji tena zile fedha nyanyasa na fedha dhalilisha za mabeberu.

Hongera rais Kenyatta kwa ujirani mwema, hongera rais Magufuli for being a master diplomat of your own way on African Diplomacy, ila pia rais wetu ni lazima aende duniani, akajichanganye na marais wenzie wakubwa kwenye International Diplomacy angalau ahudhurie UN GA, hata kama mwenyewe hapendi, apendeshwe for international diplomacy na international exposures.

P

Magufuli sasa alipie vifaranga alivyochoma na ng’ombe wa Wamaasai alio taifisha na kupiga mnada.

Tunamkubali sana rais Magufuli huku pwani.

cant relate.

Hakubaliki.

Makufuthi ni meffiakuku kwa macho zangu

Apan tambua Magu’fool!

Now Kibaki looks bad, ile gold ya Kabila ilipotelea huku kabisa

Twapenda Pombe.

Both of them can get into a clay boat and sail away. Tikteta na mlevi

Tuendeleza wema huu na ujirani mwema hata katika hili la KQ
P