Watapata tabu sana

Nimekuwa nikiisikia kauli hii siku kadhaa na inapendwa kutumiwa na watu wengi sana.
Naombeni kujuzwa chanzo cha msemo au kauli hii
#WATAPATA_TABU_SANA

  1. Wakati ule “dada mkubwa” wa USA kakinukisha! Kuna kamanda RPC, nadhani wa central zone, alipiga mkwara waandamanaji na kuahidi “WATAPATA TABU SANA!”

  2. Mpk Hapo kauli ilikuja na kupotea. Siku za hivi Karibuni, wala jamaa wa CHILA WAA DUU akina BROUWN SOUD! Wakaja tena na kauli ile ile: WATAPATA TABU SANA!

Muasisi ni kamanda Muroto wa Dodoma

Rejea yale matamko mbalimbali ya maandamano ya April 26

Hajasikika muda huyo kamanda sijui ataibuka na kiki gani

Kwani hukumsikia week iliyopita kamdaka chid benz na dawa za kulevya

Na kweli ile ilikuwa kiki maana kila mtu anajua kuwa chid benz ni teja na muda wote ukimhitaji kumkamata na kete ni rahisi tu

Wanaoipigia chapuo wanajua what does it mean. Something big is about to happen, I believe. Huenda yajayo yanafurahisha kweli

:):):slight_smile: Yajayo yanafurahisha…

pia kuna clip moja wakati wa uefa ilikazia kaulihiyo nanukuu

'mkuu unazungumziaje Liverpool, nasema watapata tabu sana kipigo chake kitakua cha mbwa koko"

hahaha ‘watapata tabu sanaaaa sana’

Aiseee hii kauli nmeona inapendwa sana na wadada yan kdogo tu unaskia
Na Bado utapata tabu sana

Wew hufuatilii jambo vizuri, kaulu hii ilirudshw n kuchekesho cha mechi ya Liverpool vs Real Madrid, kwamba Liverpool watapata tabu sana …

Unawachokoza THE REDS

Hahah!! Mkuu adi huko wanaitumia?

Mkuu huko fb ndo kauli yao iko moto
Sana Kwa sasa

Hahah!! Kila kitu na muda wake mkuu