While in exile....

Unapokuwa ukimbizini huwezi kuwa huru kama ulivyo kwenyu ama nyumbani kwako… Kuna hali fulani ya kujiona kabisa hapa si pako na mazingira ni mapya na mageni kabisa… Watu pia ni wapya…
Lakini cha kutia moyo na faraja pia ni ile company unayoipata toka kwa home pals… Mnajikuta wote mmekutana ughaibuni… Ukimbizini… Mnaanza kukumbushana mengi na jinsi mnavyoihamu nyumbani
Tuko huku ukimbizini hatujui tutakaa huku mpaka lini na tukirudi nyumbani kutakuwaje… La muhimu sana na la kukumbushana kila wakati ni kuwa tuwe makini sana na maandiko yetu… Kuna siku tutarejea nyumbani… Wamekuja hata huku pia kimya kimya wanatusoma na kutuchambua. Wanatuweka kwenye mafungu na makundi yao… Tumakinike… Kuna siku tutarudi nyumbani

Mungu ibariki Tanzania… Na watu wake

Kumakinika kukoje mghothi? Watu wana hasira sana ndiyo maana wanaandika kila kinachowajia kichwani!!

Msata mojaaaa shukran mkuu

Kwamba na huku ukimbizini mmewafata???

Kweli kiongozi jr

Hilo la kumakinika na maandiko yetu ndo jambo la msingi

Tunatishana au?

Hahahaaa… Inshallah ipo siku tutarejea kwetu pazuri tunapopakumbuka sana

Mmh

Hapana huo ndio ukweli

Tumepigwa exile, nakumbuka jinsi Okonkwo katika Things Fall apart alivyopelekwa exile kutoka Umuofia, when he came back he found things had fallen apart, wakumbusheni kina tcra wasituweke sana exile

Nitarejea kule na ID mpya kabisa

Hivi katika kufuatiliwa wanawezaje kukukamata jamani? Kwa mfano umetumia e-mail kujiunga Kenyatalk, jamaa hawewezi kufuatilia kuwa kutumia hiyo e-mail yako?

Wakati nakimbilia nchi jirani nikapita maeneo ya Msata, nakumbuka kuona sura kama hii, bilashaka ndio wewe mkuu. Karibu sana, we are in exile na hatujui lini tutarejea kwetu, jambo la muhimu ni kuendeleza mshikamano na kuruhusu hoja za kupingana bila kupigana, kukubali tofauti zetu za kila aina kuanzia jinsia, dini, kabila, rangi au eneo mtu anapotoka lakini bila kubaguana

Amen

Hakuna ka dawa ka kumtoa mtu mshipa mkuu.

IP address ndo mchawi mkuu, waki track inaonyesha aina ya device pamoja na location uliopo. Ndo mana JF wao katka detail zao wameondoa IP address zetu kwa usalama wetu ndo ile juzi juzi wali update terms nd conditions

Hatuna namna mkuu, mzee wa msata!

Serikali ya TZ ilipotaifisha mifugo na kuchoma vifaranga toka hawa jirani zetu, VP wao alisema ‘paraphrased’: kiongozi wao ndiye mbaya wetu, lakini wananchi ni ndugu zetu.

Hilo halina ubishi…

Cc: @Mahondaw

Mkuu sijui unamaaninsha nini. Huku jukwaani hakuna anayetukanwa bali anaambiwa ukweli mchungu. Hivyo hata wakija huku hakuna namna tutaacha kuongea ukweli. Tukirudi huko nyumbani wanaweza kufanya chochote kama kinachowakwaza ni ukweli.