tukiwanga high school kuna huyu boyz alikuanga akijiita Lemio. huyu msee alikuanga haeleweki. idhaa ya preps either umpate anamake noise, analala, ama anasoma magazine ya ngwati. hakuanga anafanya kitu constructive. siku ya results alikuanga last akijaribu sana anakuwa second last. alikuanga anakaanga kona sana na alikuanga akimulikwa sana huko. most of the night preps alikuanga akipenda kudoze sana. saa kuna day boy flani alikuwa akiitwa Gillie aliplan vile tungemhangaisha. piri naye ni wale hawakuwa watiaji saa plan ilikuwa set. tumeingia daro evening prep lemio by kitu 8.30 ashaanza kung’orota sisi nani tukatafuta tai zile zimezeeka tukamfungilia miguu na mikono kwa locker alafu tukacount @123tokambio tukatoka kijiko kutoka daro saa hio wasee wengine wamepitia juu ya locker za wengine. Lemio kuamka akacheki vile wasee wanahepa akaona huku ni kunoma pia yeye akadai kuhepa lakini wapi msee asongi. akainuka tena asongi. jamaa alipiga nduru kama dame anapigwa kuni “waaaiii mama” alipiga nduru ile ya nguvu ikabaki tumerudi daro haraka ndio tusiletee commotion saa hio daro zingine zinachungulia kwa dirisha kuona nini inaendelea. kiasi depa akaingia akauliza prefect ngori ni gani ameskia “I have heard someone screaming like a cow on heat”
“Its Lemio Sir”
saa hio lemio bado miguu yake imefungwa kwa locker ni bahati alikuwa amefunguliwa mikono. depa kumuuliza akadai ati aliona panya “embeba masagiro” (kisii - ile panya kubwa inatoshana na pussy). depa akamsho akuwe serious. uzuri akuambiwa atoke otherwise angejipata akitembea na locker hadi staffroom.
hiyo chuo bado kulikuanga na warogi walai. msee anaamka usiku saa nane alafu anakam anakuwai kibare manze alafu anahepa na blanketi yako. before ugutuke uanze kumfuata unacheki tu vile ameteremka mbio kuenda dorm za huko chini saa hio blanketi inapepea tu. Alafu huezi mfuata kwa dorm unaeza ingia alafu msee akupate akuulize unafanya nini huko usiku saa nane upigwa vita hujai ona. huyu msee kuna venye alinikulanga kibare manze niliskia ni kama nimepigwa stima. lakini nilikuwa rada nikakufa na blanketi. huyo msee akacheki siachilii blanketi akaachana nayo akatoka mbio. nikajifanya nimedoze fala akarudi tena nikamchekia akitembea nikaamka nikaanza kutembea nyuma yake saa hio kuna giza kwa dorm. nilingoja ainame akidai kupiga form one kibare nikamuwai bare moja nzito ya shingo msee alipiga chini juu ya kuloose balance vile alilose balance ilinifanya nitake kuchema lakini nikaacha.nilishindwa kumshika juu alikuanga na mwili kiasi alafu alikuwa na nguvu. vile alitoka hiyo dorm sijui. before wasee waamke nilikuwa nisharudi kudoze wasee wanaeza kukugeuzia ati ulikuwa unasanya uonwe war ile mbaya. ufala ni ati uyu msee hakuna msee alikuanga anamtambua manze.
depa wetu alikuanga mjinga sana. alikuanga anakamingi morning dorm kuamsha wasee. wasee walikuwanga kwa mlango walikuanga wanaonanga shida kweli. hao ndo walikuanga wanafanyiwanga litmus testing ya viboko before mfikiwe mko rada mbaya. kuna siku depa aliingia 4.30 saa hio bell imering lakini wasee wameignore wakaendelea kudoze. aliingianga chini ya maji alafu akaendanga kufungua bed ya jamaa alikuwa akijiita Ras. ni ile design Ras alikuwanga amecover bed yake na masheets ilikuwa inamfanya suspicious. depa alienda akamfungua blanketi saa hio ras ameamka na mahasira “We Mata” kucheki ni depa akanyamaza. depa akamuuliza alikuwa anadai kusema nini akadai alikuwa anataka kusema Matayo. depa akubuy hio vako lakini alochorea tu. alafu kuna day kifala flani kiliamka saa nane akakam pole pole kwa dorm akaanza kubonga kama depa kabisa. design wasee waliamka manze ungeeza fikiria kuna nyoka kwa hio dorm. uyo msee alisema ivo alafu akajitoa akuna msee alimuona. mafala hata hawakucheki ni saa ngapi wanataka kuenda daro kutoka nje watchie anawauliza wanaenda wapi wakadai daro. watchie akawashow ni saa nane za usiku warudi walale. wasee walikatsika sana.