Hivi Mambo Ndio Yamefikia Hivi?

@Raynavero duh…haya bhana…

Halafu wanasema nchi Ni yetu sote Pamoja na raslimali zilizopo wananchi watanufaika nazo mbaya zaidi Eti mtetezi wa wanyonge ptuuuuu

sio kwamba wamekosa kazi ya kufanya. Hizo ni mbinu za wanaccm ili kututoa kwenye mjadala wa bajeti kuu, hasa baada ya kuona bajeti ya upinzani imeshawafikia asilimia kubwa ya wananchi wenye uelewa

Hahaa!karibu tz nchi yenye maajabu ya kila aina

Mambo ya kipuuzi kama haya ndio wanayaweza sana hawa viongozi wa awamu hii

Ngoja wakawadhalilishe huko huko ndani ya mgahawa wa wabunge labda nao wataelewa hawa jamaa wanavyotuvua nguo mbele za watu uraiani. Ukiona chakula cha mbunge kinapimwa kwa rula, bikari na kipima pembe tena jikoni kwao kabisa anza kumuomba Mungu atuepushie kikombe hiki.

Niliwahi kusema bunge letu linazoeana sana na mbwa na ipo siku watawafuata msikitini… Leo yametimia ndio naibu spika anaomba maelezo ya serikali. Kwani hakusikia kuna watu wamepigwa na kuumizwa na udhalilishaji mwingine mwingi tu? Hakuamini? Leo watu wametinga bungeni hadi jikoni na rula zao za kupimia jinsia ya samaki, bila hata ruhusa ndio muongozo umeombwa! Kweli? Ama kweli mkuki kwa mchungu, kwa binadamu nguruwe!

Haya ngoja tuone. Ila naamini msimu wa mvua ukiisha adha ya mbu nayo itapungua!

Umesema jambo la kweli kabisa! Watu wamehamasishwa kuchimba mabwawa na kufuga samaki. Sasa hata samaki nifugao napaswa kutumia rula kabla ya kuwavuna? Hii no aibu kubwa sana kwa maamuzi ya kijinga

Hii wizara ndio ambayo haikupata hata shilingi kumi bajeti iliyopita?

A very good and a valid point mkuu. Common sense is never common they say.

Kina stroke watakuambia serikali yao ya ccm haijatoa passports kwa sato walioko huku kwa hiyo hawawezi kwenda Kenya au Uganda.

Akili hiyo ccm hawana. Alijisemea mtu mmoja kuwa akili zao ni za kuvukia barabara tu.

Nchi ya kusadikika hii mkuu, mambo yake yanachekesha sana kama siyo kufurahisha

[ATTACH]177845[/ATTACH]

Inachukiza sana kama mtu anashindwa kuzitoa maelezo yaliyonyooka shilingi trilion 1.5, lakini anapata ujasiri wa kutoka ofisini kwenda kupima urefu wa vidagaa kwenye migahawa na mama ntilie.

Hapa hata kama serikali iliwakopesha hawa walioendesha hilo zoezi wakasoma hadi vyuo hizo hela zilipotea tu bure. Lakini nisiwalaumu sana maana wamesema waliagizwa na waziri wakavipime hivyo vidagaa.

Watanzania jamani tuwaombee viongozi wetu ili Mwenyezi Mungu awape hekima kwenye kila walitendalo lilete tija kwa manufaa ya nchi. Au sala zetu zimejaa manung’uniko ndio maana kila siku tunavuna matunda yanayotufaa?

Ila kwa kweli sato akiwa mdogo ana miba mingi