Kikao na wastaafu ni changa la macho kwa huyu anayetapatapa?

Nani atampenda na anafanya mambo ya kijingajinga!! Ndiyo maana ka JK kamamkaushia pamoja na kujipendekeza kwa wastaafu!! Hivi umeona lilivyokuwa linajishebedua wakati linaongea? Watu wamekaushia ile mbaya mpaka nikamwona Jaji Augustino Ramadhan ameshika tama!!

Kawapotezea muda wao tu ili aongee pumba zake katika jitihada zake uchwara za kupamba na zile nyaraka mbili za Viongozi wa dini wa Kikatoliki na Kilutheri.

Anataka kutuonyesha Watanzania mnaniona!!! Wastaafu wote wananiunga mkono hivyo zile nyaraka mbili za Viongozi wa dini hazina maana. Ana ufinyu wa akili kudhani kwamba Watanzania wote ni wapumbavu hivyo kukubali hadaa zake.

Exactly, hakuna aliyemchekea ukiacha wapuuzi wachache wa Ukerewe

Kama JK yuko Bongo na akaamua kumpotezea itamuuma sana huyo dikteta.

Sijui wastaafu wako comfortable kiasi gani wanaposhiriki hicho kikao. Frankly, if I were in their position I would certainly have a bone to pick with our current rulers. Tumeshuhudia hadharani wastaafu wakitakiwa kukaa kimya bila kutoa maoni hadharani kuhusu masuala ya kisiasa na kijamii. Nikawaza, hivi Baba wa Taifa angekuwa hai, angechukuliaje! Tumeona juhudi za kuaminisha umma kuwa tawala zilizopita hazikuwa na uzalendo wa kutosha hivyo nchi ilikuwa kama shamba la bibi! Tumeona harakati na mchakato wa kurekebisha sheria za madini ukiendeshwa kwa namna ambayo kwa uhakika uliwaumiza sana wastaafu wa awamu ya 3 na 4. Aidha uliendeshwa kana kwamba iliyoko madarakani ni serikali ya Ukawa! Sera za maendeleo zilizowekwa na baada ya mashauriano ya kina sasa zinatupiliwa mbali bila maelezo ya kutosha.

Mkuu msikilize Baba wa Taifa hapa.

https://www.youtube.com/watch?v=UFIkjSqXTUQ

Kicheko chake cha kinafiki

https://www.youtube.com/watch?v=PNAEeJUg-Ec

https://www.youtube.com/watch?v=0hLjxxDElpM

Sasa kama hawa majaji wastaafu walitoa kauli kama hizi inakuwaje Msigwa kwenye ripoti yake ya Ikulu kuhusu kikao cha jana kauli za hawa wastaafu aliziminya? KULIKONI? Au ndiyo katika kuendeleza uongo kama wa mkulu wake wa kazi AKA dikteta!?

Hawa Wastaafu wamenishangaza sana. Warioba kimyaaaa kuhusu katiba mpya ya rasimu ya Warioba

Lowassa na Sumaye kimya kuhusu manyanyaso yote ya vyama vya upinzani, kudai katiba mpya, na kukanyangwa kanyagwa kwa katiba ya sasa, Bunge kudharauliwa, Mahakama kudharauliwa, watanzania kutekwa na kuuwawa bila uchunguzi wowote.

Lissu kapigwa risasi 38 miezi 11 iliyopita hadi leo hii hakuna uchunguzi na hajalipwa haki yake. Sumaye na Lowassa hawakutia neno (labda walisema tumefichwa) Mwinyi na Mkapa kimyaaaa kabisa kuhusua kauli zao za gari kuendeshwa kama gari bovu na mjadala wa Kitaifa kuhusu kuanguka kwa Elimu.

Wastaafu hawa ni WANAFIKI wakubwa sana ukiondoa Jaji Samatta na Augustino Ramadhani.

https://www.youtube.com/watch?v=kNqXPgPSleE

https://www.youtube.com/watch?v=fTUjMVSP7dI

Huyu Mzee mpuuzi sana mamamaye yaani anazungumza pumba tupu bila woga wala aibu!!!

https://www.youtube.com/watch?v=mjt-EVmu1Bc

[MEDIA=instagram]BkzLH-FHr6Y[/MEDIA]

Washukuriwe majaji wastaafu kama mzee Samatta kwa kumchana. Maendeleo na sheria kandamizi wapi na wapi.

daah ahsante mkuu lkn hv yule mzee anadawa au, kila mtu akikutana nae ht kam anampinga atabak kumsifia tu…
kwel upele humpata asiye na kucha…

Kuna msemo kuwa " Hata wapumbavu huzeeka" na ndio maana hatumii busara iliyopo kwa baadhi ya wazee wetu, wameshindwa kumwambia ukweli in a politely way na msg ikafika.

Mi naona angewaandalia kikao au waandae wenyewe kikao wakiwa free wazungumze then wampelekee ripoti ya kikao cha hao viongozi wastaafu nafikiri atapata picha tofauti na aliyoipata siku hiyo!

Hivi hakuwakumbusha kuacha tabia yao ya kuwashwa washwa?

Kati ya majitu niliyoyapuuza hili linaongoza!! Watu mimi niliwakatalia tangu zamani kwamba jitu halina busara ya kushika ofisi kubwa!!

Kabisa Mkuu mie sikutegemea kabisa MACCM yamteue huyu mtu eti aiongoze nchi wakati nyadhifa zake zote kwa zaidi ya miaka 20 ni madudu matupu ambayo yameigharimu Tanzania trillions za shillingi pesa za walipa kodi. Barabara zake zote alizojenga akiwa Ujenzi ni hovyo kabisa kwani baada ya mvua kubwa lami yote ilisombwa na mvua na madudu mengine chungu nzima.

Kiburi chake cha kulewa madaraka alithubutu kuwatusi wastaafu kwamba wanawashwa washwa. Sasa kagundua kila analogusa ni madudu tu anajifanya ana unyenyekevu wa hali ya juu! Jamaa ni MNAFIKI mkubwa sana.