Kisa Cha Kweli:Kisiwa Cha Harishi

SEHEMU YA 17

“Tutakufa kama wenzetu. Sidhani kama tutapona kwa maana tulikuwa watu saba, sasa tumebaki watatu” nikamwambia Yasmin.
“Msikate tama ndugu zangu. Kama ni kufa tutakufa sote. Hamuwezi kufa mkaniacha mimi”
Nilimuona Haji akijifuta machozi.
“Usilie ndugu yangu. Ushinde moyo. Safari yenu bado ni ndefu” akaambiwa na Yasmin.
Shazume akageuza uso na kunitazama.
“Nina tama ndogo sana kama tutapona” akaniambia.
Sikumjibu kitu. Yasmin akanyanyuka.
Nitawatayarishia japokuwa uji mchangamke” akatuambia.
“Sawa” nikamjibu.
“Naenda kuwapikia halafu nitawaletea”
“Kama tutakusumbua ninaweza kuja kuuchukua”
“Harishi hatakuja tena leo. Mnaweza hata kuja nyote”
Nikawatazama wenzangu.
“Eti mnasemaje?”
SASA ENDELEA
“Akituletea huku itakuwa bora” Haji akasema.
“Tutakuwa tunamsumbua. Tungekwenda tu kwa vile ametuhakikishia kuwa leo hakuna tatizo” nikawambia wenzangu.
“Haya twendeni ila tusikae sana” Shazume akasema.
Tukaondoka pamoja na Yasmin kuelekea katika lile jumba la Harishi.
“Tangu mmekuja nyinyi nimejisikia kuchangamka sana” Yasmin alituambia tukiwa njiani.
“Kikwazo chetu kikubwa ni huyu Harishi. Kama si yeye tungekuwa na furaha sana” nikasema.
“Roho zetu sasa zina wasiwasi. Kila siku mmoja wetu anakufa. Tulikuwa watu saba, sasa tumebaki watatu” Haji akalalamika.
“Ni kweli Haji lakini kama nyinyi mtakuwa makini mnaweza kusalimika” Yasmin akatuambia.
“Yasmin unatuambia ukweli? Tutasalimikaje? Hata kama hatutauawa na Harishi tutakaa katika kisiwa hiki hadi lini?” nikamuuliza Yasmin.
“Kwani mimi nitakaa hadi lini?” Yasmin akatuulisa. Sauti yake ilikuwa imebadilika.
“Wewe mwenyewe umeshajitolea” nikamjibu.
“Kwa sababu sijipendi?”
“Hapana, si hivyo”
“Basi mimi na nyinyi ni sawa tu. Kama mimi nimejitolea na nyinyi mjitolee kama mimi. Muwe tayari kwa lolote”
“Sisi tumeshajitolea Yasmin. Hatuna la kufanya” nikamwambia Yasmin aliyekuwa amekasirika kidogo.
“Tunaona juhudi zako Yasmin” nikaendelea kumwambia. “Kama si wewe kutupokea kwa nia moja tungekuwa tumeshakufa kwa kuhangaika na njaa.
Tulipofiak kwenye lile jumba tulipumzika ukumbini. Yasmin alituletea karata kisha tukaenda kupika uji. Uji ulipokuwa tayari Yasmin alituletea tukanywa. Huji huo ulikuwa umechanganywa na asali.
Tuliposhiba Yasmin aliondoka tena kwenda kupika chakula cha mchana. Sisi tuliendelea kucheza karata, tulipochoka tukalala hapo hapo. Yasmin ndiye aliyekuja kutuamsha.
“Wenzangu kumbe mmelala?” akatuuliza.
“Ah! tumepitiwa na usingizi bila kujijua” nikamwambia na kumuuliza “Umeshapika?”
“Nimeshapika, kwani mna njaa niwapakulie?”
“Bado kwanza. Tusubiri kidogo”
“Naona mko wachovu sana. Twendeni bahari mchangamke kidogo”
Kwa vile hatukuwa na la kufanya tukakubaliana na wazo La Yasmin la kwenda baharini. Kisiwa hicho kilikuwa na fukwe nzuri zenye mchanga mweupe.
Tukiwa kwenye fukwe za kisiwa hicho tulibuni michezombalimbali ya kujichangamsha ikiwemo kukimbizana. Mwisho tuliamua kujitosa kwenye maji na kuogelea tukiwana nguo zetu.
Yasmin alikuwa hodari wa kuogelea. Alituambia alipokuwa Comoro kila siku za jumapili alikuwa akienda kuogelea na ndugu zake.
Tulipochoka kuogelea tulikaa kwenye fukwe hadi tukakauka maji. Tukaondoka kurudi katika jumba la Harishi
Yasmin alikwenda kuoga maji baridi. Alipomaliza na sisi tulikwenda kuoga. Hatukuwa na nguo za kubadili.
Yasmin alitupa mashuka tukajifunga. Zile nguo zetu tulizifua na kwenda kuzianika nje kwenye jua.
Tulipomaliza kuanika nguo ndipo Yasmin alipotuandalia chakula, tukala. Wakati tunakula alituambia kuwa tunaweza kuendelea kushinda hapo kwake hadi jioni lakini Haji akapinga ushauri wake na kutaka tuondoke tukimaliza chakula.
Baada ya chakula tulikubaliana kuwa turudi katika ile nyumba tuliyohamia. Tukamuaga Yasmin na kuondoka.
“Sasa wenzangu mna ushauri gani, hali ya hapa ndiyo kama hii tunayoiona?” nikawauliza wenzangu mara tu baada ya kufika kwenye ile nyumba
“Kwani wewe una ushauri gani?” Haji akaniuliza.
“Nia yetu sote ni kuondoka katika kisiwa hiki. Sasa nataka tujadili njia itakayotuwezesha kuondoka. Ni vizuri kila mmoja akatoa wazo lake alilonalo” nikasema.
“Ni kweli ulivyosema lakini tunajikuta tumekwama, tusingekuwa hapa hadi leo” Shazume akatuambia.
“Kwa hiyo hatujui tutaendelea kukaa hapa na Yasmin hadi lini?” nikauliza.
“Ukweli ndio huo” Haji akanikubalia.
Nikatikisa kichwa changu kusikitika, baada ya hapo sote tukawa kimya.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 18

Yalipofika majira ya saa kumi na mbili jioni Yasmin akaja.Alikuwa ametuletea chakula cha jioni. Ulikuwa ni wali ule ule tuliokula mchana. Tukakiweka chakula hicho kusubiri usiku.
Yasmin akataka nimsindikize arudi. Nikawambia wenzangu “Namsindikiza Yasmin”
“Usije ukachelewa kurudi. Kumbuka usiku umekaribia” Shazume akaniambia.
“Sitachelewa” nikamjibu.
Tukaondoka na Yasmin. Tukiwa njiani Yasmin alinitazama machoni mwangu kisha akaniambia.”Nim
efurahi sana leo kuwa peke yetu mimi na wewe”
“Kwanini?” nikamuuliza.
“Tangu juzi hatujapata nafasi ya kuwa pamoja peke yetu. Mara nyingi unakuwa na wenzako. Jana jioni nilitaka kukwambia nisindikize lakini marehemu Masudi akawahi yeye. Sikuweza kumkatalia. Najua roho ilikuuma na mimi pia iliniuma” Yasmin akaniambia.
“Unajua jana niliwafuatilia nikawakuta mnafukuzana ndani. Kuna wakati marehemu alikushika kiuno mkaanguka chini pamoja”
Nilipomwambia hivyo Yasmin alinywea.
“Kumbe ulikuja kutuchungulia?” akaniuliza.
“Nilikuja, nilipouona mchezo wenu nikaamua kurudi”
SASA ENDELEA
“Si mchezo wetu. Masudi ndio alikuwa analazimisha. Alikuwa akinitaka kimapenzi nikamkatalia” Yasmin aliniambia.
“Basi tusimseme sana kwa sababu ameshakufa lakini nilishituka”
“Naomba unisamehe kwa hilo kama limekuudhi”
Nikanyamaza kimya.
“Umeshanisamehe?” Yasmin akaniuliza huku akinitazama machoni mwangu. Alinitazama kwa macho ya huruma sana.
“Kwani wasiwasi wako ni wa nini?”
“Nataka unisamehe!” Yasmin akasisitiza.
“Nimekusamehe”
“Sasa tusizungumze tena habari hiyo. Tuzungumze yanayotuhusu mimi na wewe. Kama tutafanikiwa kuondoka katika kisiwa hiki utanioa?”
“Wewe ndio uniambie mimi kama utakubali kuolewa na mimi”
“Mimi niko tayari hata sasa hivi”
“Unadhani wazazi wako watakubali?”
“Watakubali”
“Ujue kuwa wewe ni binti wa rais na mimi ni mtoto wa kimasikini”
“Kusema hivyo si sahihi. Sasa hapa tulipo mimi na wewe tuna tofauti gani?”
“Kwa hapa tuko sawa ila ukirudi kwenu wewe utakuwa mwana wa rais”
“Huo ni ufinyu wa mawazo ya binadamu. Binaadamu wote ni sawa. Mfano halisi ni wa hapa tulipo. Umesema tupo sawa, basi tutakuwa sawa popote. Hata kama wewe ni mtoto wa kimasikini lakini nimekupenda, utakataa?”
“Labda wewe unikatae mimi”
“Una majibu yasiyoniridhisha. Kwanini huniambii kuwa unanipenda na utanioa. Mimi nataka utamke hivyo”
“Nimekupenda na nitakuoa”
Yasmin nilipomwambia vile alitabasamu. Nilihisi alikuwa akijaribu kuufariji moyo wake uliokosa mapenzi kwa muda mrefu.
“Yasmin unaweza kusema maneno hayo hapa kwa vile hatuna matumaini ya kupona. Lakini kama tutafanikiwa kuondoka hapa unaweza kubadilika na kuniona mimi kama takataka”
“Nakuhakikishia kaka yangu mpenzi sitabadilika. Mimi si kinyonga”
“Tuombe tuokoke katika balaa hili lililotukabili”
“Ishaalah tutaokoka. Tena wewe ndio utaniokoa mimi”
“Sio wewe uniokoe mimi?”
“Mimi nataka wewe uniokoe mimi”
“Basi ishaala itakuwa hivyo unavyotaka”
“Nikuimbie nyimbo?”
“Niimbie”
Yasmin aliacha kutembea akasimama mbele yangu akiwa amenigeukia mimi. Kitendo hicho kilisababisha na mimi nisimame. Akapeleke mikono yake kwenye mabega yangu.
“Mimi ni nani wako?” akaniulza. huku akinitazama machoni mwangu.
“Wewe ni mpenzi wangu” nilijua kuwa alikuwa anataka jibu hilo.
Nilipomjibu hivyo alitabasamu na kuishusha mikono yake mabegani mwangu na kugeuka.
“Sasa ngoja nikuimbie” akaniambia huku tunaenda.
Akaimba wimbo mzuri kwa lugha ya Kikomoro. Wakati akiimba alikuwa akitingisha tingisha kichwa chake kufuatia mawimbi ya sauti yake. Wakati akiimba alikuwa akitia mziki kwa mdomo. Alionekana kuwa hodari sana wa kuimba na kutia mziki. Wimbo huo ulikuwa unavutia ingawa sikujua tafsiri yake.
Alipomaliza kuimba alinitafsiria kwa Kiswahili. Akaniambia “Ndege wawili dume na jike wamepotea juu ya bahari. Hawajui watokako wala waendako. Wanalia swi! swi! swi!”
“Wamesafiri mchana kutwa bila kupata mahali pa kutua. Sasa jua limekucwa na giza linaingia. Hawataweza kusafiri usiku. Wanalia swi! swi! swi!”
Japo niliufurahia wimbo huo tafsiri yake ilinisikitisha.
Nikahisi kama ndege wawili hao walikuwa ni mimi na yeye.
“Kumbe Yasmin unajua sana kuimba!” nikamwambia.
“Hapana, najaribu tu”
“Si kujaribu, unajua”
“Kweli eh?”
“Umeniburudisha sana”
“Ukinioa nitakuwa nakuimbia kila siku”
Tulikuwa tumeshafika kwenye lile jumba analokaa.
Nikasimama kwenye mlango.
“Mimi sitaingia ndani” nikamwambia.
“Kwanini?” Yasmin akaniuliza.
“Si nimekusindikiza tu”
“Ukinisindikiza ndio huingii ndani, mbona siku nyingine unaingia?”
“Yasije yakanikuta yaliyomkuta Masudi”
“Mimi naamini wewe huko kama Masudi lakini kama umeamua uwahi kurudi, unaweza kurudi na nakutakia usiku mwema. Tutaonana kesho.
“Asante. Usiku mwema na kwako”
Nikamuacha Yasmin amesimama akinitazama. Mimi nikarudi kule nyumbani tulikotoka. Nilirudi kwa mwendo wa haraka haraka ili kiza kisinikute njiani kwani jua lilikuwa limekuchwa sana.
Nilijikuta nikiwa na furaha na mwenye matumaini kutokana na maneno ya Yasmin. Upendo aliouonesha kwangu ulitosha kunipa hamasa ingawa tulikuwa katika hali ngumu.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 19

Nilijikuta nikiwa na furaha na mwenye matumaini kutokana na maneno ya Yasmin. Upendo aliouonesha kwangu ulitosha kunipa hamasa ingawa tulikuwa katika hali ngumu.
ENDELEA…
Nilipofika katika ile nyumba niliwakuta wenzangu tayari wameshaanza kupata wasiwasi.
“Ilibaki kidogo tu tukufuate kwa maana tuliona unachelewa” Haji akaniambia.
“Mlijua na mimi nimeshakwenda na maji?” nikawatania.
“Si ajabu. Haa tunahesabiana siku na saa tu”
“Tusikate tama kiasi hicho. sisi ni wanaume. Mmeshakula?”
“Tulikuwa tunakusubiri wewe” Shazume akaniambia.
“Mimi nimeshakuja. Toeni chakula tule”
Chakula kikatolewa. Tukakaa chini na kuanza kula.
Tulipomaliza kula tulikaa uani tukawasha moto na kuuzunguka. Kiza kilikuwa kimeshaingia na kulikuwa na baridi.
Tuliota moto hadi majira ya saa mbili usiku. Tukaingia vyumbani kulala. Usiku ule haukuwa wa mawazo sana. Nilipitiwa na usingizi mara moja.
Nilipoamka asubuhi nilishituka nilipoona mlango wa nje ulikuwa umeng’olewa mzima mzima. Palibaki uwazi mtupu. Mlango wa chumba alicholala Haji pia ulikuwa umeng’olewa. Mlango wa chumba cha Shazume ulikuwa mefungwa.
Nikaenda katika ule mlango wa chumba cha Haji na kuchungulia. Nilimkuta Haji akiwa amelala chini amekufa. Kichwa chake kilikuwa kimetobolewa kwenye utosi. Damu iliyoganda ilionekana kwenye nywele zake.
Hapo nilijua kuwa tulikuwa tumeingiliwa. Bila shaka Harishi alikuwa amekuja usiku akang’oa milango na kumuua Haji.
SASA ENDELEA
Lilikuwa tukio ambalo sikulitegemea. Katika kundi letu Haji ndiye aliyekuwa mdogo kuliko sote. Kifo chake kilinisikitisha na kunikatisha tamaa kabisa.
Nilijiambia kama Harishi ameweza kutufuata huku na kumuua Haji na sisi hatutabaki. Tilichokuwa tunasubiri ni siku na saa zetu ziwadie.
Baada ya kushangaa kwenye mlango kwa sekunde kadhaa nilikwenda kumgongea Shazume. Shazume akaamka na kufungua mlango.
“Una habari gani?” nikamuuliza nikiwa nimetaharuki.
“Sina habari yoyote” Shazume akanijibu huku akionesha kupata hofu.
“Haji ameuawa!” nikamwambia.
Shazume akagutuka.
“Haa! Haji naye ameuawa? Si tulilala naye humu ndani jana usiku?”
“Tazama ule mlango wa nje”
Nilimuonesha Haji ule mlango uliong’olewa kisha nikamwambia. “Harishi ameung’oa usiku”
Shazume aliutazama huku akitikisa kichwa.
“Ameng’oa na mlango wa chumba cha Haji” nikaendelea kumwambia.
Shazume akasogea kwenye mlango wa kilichokuwa chumba cha Haji. Alipoiona maiti ya Haji alishituka sana.
“Mimi naona hatutapona”
“Kupona tusitegemee ndugu yangu. Harishi ameshajua tupo hapa, usishangae kesho tukiamka mmoja wetu akawa hayupo!”
“Hapa nyumbani hapafai tena kukaa. Tutafute sehemu nyingine ya kujificha”
“Tutajificha wapi Shazume?”
“Popote tu, nyumba ziko nyingi”
“Sawa. Tumngoje Yasmin aje tumueleze kuwa mwenzetu ameuawa”
“Pia tumueleze kuwa tunaondoka hapa. Harishi akija tena asitukute”
“Sawa, tutamueleza”
Tukaenda kunawa uso na kusukutua maji bila kupiga mswaki. Tulikuwa tumeshachanganyikiwa. Tulipomaliza tulikaa kumsubiri Yasmin.
Yasmin alikuja majira ya saa tatu hivi. Hakuwa amechukua kitu.
Akatusalimia na kutuuliza kwanini tumeng’oa milango.
“Hebu chungulia kwenye hicho chumba” nikamwambia.
Yasmin akachungulia na kugutuka.
“Haji amepatwa na nini?”
“Haji ameuawa usiku na Harishi” nikamwambia.
“Mama yangu!” Yasmin alimaka huku akijishika kichwa. “Kumbe Harishi alipotoka usiku alikuja huku?”
“Sisi tumeona asubuhi Harishi ameuawa na milango imeng’olewa”
“Sasa tumepanga tuondoke hapa” Shazume akamwambia Yasmin.
“Muondoke muende wapi?”
“Twende mahali pengine. Tukiendelea kukaa hapa Harishi atakuja tena usiku”
“Sasa mmepanga muende wapi?’
“Mimi naona kama tunajisumbua, kama ni kufa tutakufa tu” nikasema.
“Hata kama tutakufa lakini hapa tuondoke” Shazume akasisitiza.
“Ni sawa. Sasa tufikirie hapo pa kwenda. Tutakwenda wapi?”
“Nyumba ziko nyingi”
“Yasmin unatushauri nini?”
Machozi yalikuwa yanamtoka Yasmin. Bila shaka yalimtoka kutokana na ukweli kwamba sote tutakufa. Hakunijibu.
“Yasmin usilie. Tunaomba ushauri wako” nikamwambia.
Yasmin alijifuta machozi kisha akatuambia. “Niwapeleke katika nyumba nyingine”
“Huko utakakotupeleka Harish hatafika?” nikamuuliza.
Yasmin akaguna kisha akajibu. Hatafika”
Nilijua alitujibu hivyo kututia moyo tu lakini mawazo ya Shazume yalikuwa tofauti.
“Ni mahali gani?” Shazume akamuuliza haraka.
“Kwanza twendeni mkanywe uji”
“Turudi kule tena?” Shazume akamaka.
“Mnakunywa uji tu halafu tunaondoka”
Shazume akanitazama.
“Mimi sitakwenda”
“Si tunakwenda kunywa uji tu” nikamwambia.
“Kwanza Harishi hatakuja muda huu” Yasmin akasema.
“Mimi sitaki uji”
“Utashinda hivyo hivyo na njaa?” Yasmin akamuuliza.
“Sioni njaa na ile hamu ya kula pia sina”
“Kama tumeandikiwa kuuawa tutauawa tu Shazume hata kama hutakula, ni bora ule tu” nikamwambia Shazume.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 20

Shazume akatikisa kichwa bila kusema lolote.
“Kakangu najua umepatwa na fadhaa lakini tumbo lako likipata riziki ndio akili itakuja” Yasmin akamwambia Shazume.
“Tulikuwa watu saba sasa tumebaki wawili tu bado nile? Sitakula!”
“Wewe ni mwanaume Shazume usiogope kula. Unatakiwa upambane mpaka dakika ya mwisho. Mnaweza kuokoka ndugu zangu. Msikate tama kiasi hicho. Twende ukanywe uji japo kidogo!” Yasmin alimwambia.
Shazume akakubali kwenda. Tukaondoka sote kwenda kwa Yasmin. Ile maiti ya Haji tuliiacha pale pale. Tangu wenzetu walivyoanza kuuawa hatukuzika maiti yoyote. Zote tuliziacha ziliwe na kunguru.
Kwa hisia zetu tulikuwa kama watu tuliokuwa vitani. Akifa mtu hakuna kuzika. Kuzika kuna utaratibu wake ambao kutokana na hali tuliyokuwa nayo tusingeuweza.
Tulipofika kwa Yasmin alituandalia uji tukanywa. Mimi nilikunywa vikombe viwili, Shazume alikunywa kikombe kimoja.
Wakati tumepumzika Shazume akawa anahimiza tuondoke.
“Tumeshakunywa uji sasa tunaweza kwenda”
“Tusubiri kidogo nifikirie pa kuwapeleka” Yasmin akamwambia.
SAS ENDELEA
Baada ya kusubiri kwa muda kidogo Yasmin akatuambia. “Haya twendeni tukatafute nyumba nyingine”
Tukatoka na Yasmin. Niliona wazi kuwa Yasmin alikuwa na wasiwasi. Alikuwa akitupeleka katika nyumba nyingine lakini hakuwa mtu aliyeonesha matumaini.
Tulizunguka sana kutafuta nyumba nyingine ambayo ingeweza kutufaa kumkwepa Harishi. Tulikuta nyumba moja iliyokuwa ufukweni mwa bahari iliyokuwa na hali nzuri kidogo.
“Mnaionaje nyumba hii?” Yasmin akatuuliza huku akituonesha nyumba hiyo.
“Hii inafaa” nikamwambia kisha nikamtazama Shazume ili nipate mawazo yake.
“Unaionaje Shazume?”
“Hapa pamejificha kidogo, panafaa” akaniambia ingawa sauti yake haikuwa na nguvu.
Tukaingia katika ile nyumba. Humo ndani ilikuwa kama stoo iliyosahauliwa. Vitu vilikuwa vimerundikwa ovyo. Ubuibui na vumbi vilikuwa vimetanda pande zote.
Binaadamu mwenye akili zake timamu asingeweza kukaa ndani ya nyumba ile labda waduu kama vile nyoka na matandu. Lakini sisi hatukuwa timamu. Tulikuwa tumetingwa. Tungeweza kukaa.
Kama tungehitaji kufanya usafi ili nyumba hiyo iweze kukalika tungelazimika kutoa nje vitu vyote vilivyokuwa ndani na kuanza kufagia, kupiga deki na kusafisha kuta. Ingekuwa kazi kubwa. Ingetuchukua hata kwa siku mbili.
Tuliingia katika chumba kimoja tukatenga vitu na kupata upenyu mdogo ambao tuliusafisha na kuamua kukaa hapo.
Kusema kweli siku ile sisi sote hatukuwa na furaha. Tulikaa chini pamoja na Yasmin. Tukawa kimya. Kila mtu akiwaza lake.
Mimi nilkuwa nikiomba usiku usifike kwani karibu wenzetu wote waliuawa usiku.
Sikujua Yasmin na Shazume walikuwa wakiwaza nini. Lakini kila nilivyomuangalia Shazume niliona mawazo yake yalikuwa mbali sana. Nilikisia kwamba alikuwa akikumbuka kwao Pemba, akiwakumbuka wazazi wake na ndugu zake. Pengine hakuwa na matumaini ya kuwaona tena.
Bila shaka Yasmin alikuwa akiwaza kama tutauawa atakosa wenzake wa kuzungumza nao na ataendelea kuwa mkiwa.
Mimi licha ya kuwa na hofu nlishajitolea kufa kupona. Sikupenda kujipa tama moja kwa moja kuwa nitapona na sikutaka kujikatia tama.
Ghafla Shazume akaanza kuimba kwa sauti ya huzuni. Ulikuwa wimbo maarufu uliokuwa unaimbwa na vikundi vya ngoma za kiasili.
“We Yauledi we niletee mashua twende Unguja!. We Yauledi niletee mashua twende Unguja!”
Na mimi nikamuitikia. “Ukipamba mke nawe ujipambe ndio suna. Usipojipamba watu hukwambia umtumwa! We Yauledi niletee mashua twende Unguja!”
Shazume aliendelea kuimba ubeti wake kwa kughani huku na mimi nikimuitikia.
Sauti ya wimbo huo ilikuwa ya huzuni lakini ilituchangamsha. Yasmin alikuwa akitutazama. Wakati ninamuitikia Shazume, Yasmin alikuwa akinifuatisha ninavyoimba.
Pengine tulikuwa tunajifariji kwa siku yetu ya mwisho kwani tangu tufike katika kisiwa kile, kila siku mwenzetu mmoja aliuawa na Harishi. Hakukuwa na siku yoyote ambayo hakukutokea kifo.
Kwa hiyo hatukujua usiku wa siku ile atakufa nani kati yangu na Shazume.
Shazume aliendelea kuimba kwa huzuni. Mimi nilikuwa nimenyamaza. Yasmin akawa anamuitikia.
Shazume alipoona mimi nimenyamaza na yeye akaacha kuimba tukawa kimya. Baada ya muda kidogo nilipata wazo.
“Tuombeni dua” nikawambia wenzangu.
“Tulikuwa tumejisahau kidogo” Shazume akasema
Nikasoma dua ndefu. Shazume na Yasmin wakawa wanaitikia “Amin”
Nilipomaliza nilimwambia Shazume aombe na yeye. Shazume akaomba dua ndefu, sisi tukamuitikia “Amin”
Alipomaliza nikamwambia Yasmin. “Omba na wewe”
ITAENDELEA

SEHEMU YA 21

Yasmin naye akaomba dua.
Kwa muda wa nusu saa hivi mahali hapo pakawa kama madarasa kutokana na kurindima visomo vyetu vya dua.
“Pia tungekuwa tunaswali” Shazume akatukumbusha.
Sikuzote binaadamu humkumbuka sana mola wake pale anapofikwa na matatizo. Siku zote hizo tulikuwa hatukumbuki kuswali ila ni kwa siku ile ambayo tuliona tutamalizika.
“Pia ilitakiwa leo tufunge” na mimi nikawakumbusha.
“Ni kweli” Shazume akanikubalia na kuongeza “Lakini tumeshakunywa uji”
“Kama tutanusurika leo tutafunga kesho. Umesikia Yasmin?”
“Nimesikia” Yasmin akanijibu.
“Sasa sisi hatuko tohara, tutaswali vipi?’ nikawauliza wenzangu.
“Twendeni tukaoge baharini tujitoharishe” Shazume akasema.
“Hizi nguo zetu pia hazina tohara”
“Tuoge na nguo zetu ziweze kutoharika, zikikauka tutaswali”
Tukakubaliana.
SASA ENDELEA
Tukaamua sasa twende baharini tukaoge. Tukaenda sote watatu, mimi, Shazume na Yasmin. Yasmin alipotuona sisi tunajitosa kwenye maji na yeye akajitosa. Tukawa tunaoga na kuogelea pamoja.
Tuliendelea kukaa kwenye maji kwa muda kidogo ili kujisahaulisha matatizo yaliyokuwa yanatukabili.
Asubuhi ile maji yalikuwa matamu kwa mtu ambaye alikusudia aogelee kwa starehe ila kwa sisi ilikuwa starehe ya kujilazimisha. Mawazo mabaya yalituepuka kwa muda yakitusubiri tumalize kuogelea.
Tulitamani tusitoke ndani ya maji lakini nilipomuona Yasmin aliyekuwa akiogelea karibu yangu anarudi ufukweni na mimi nikaamua kurudi.
Tukakaa ufukweni na kumsubiri Shazume. Naye alipotuona tumerudi ufukweni akatufuata.
Tukakaa kuota jua. Nguo zetu zilikuwa zimetota. Kitendo cha kuogelea na nguo zetu hakikuwa cha maana sana kwani mzizimo ungeweza kutuletea madhara ya kiafya lakini hatukuwa na la kufanya.
Yasmin ambaye alikuwa na nguo za kubadili alizokuwa akiletewa na Harishi alikuwa akifuata mkumbo tu, haikumpasaaloweshe nguo zake ila alipotuona sisi tunaoga na yeye akajitosa.
Tulikaa kwa muda kwenye ufukwe tukiangalia bahri na ndege waliokuwa wakiruka ruka. Ili miiliyetu isisinyae tuliamua kufanya mazoezi ya kukimbizana.
Tulikimbizana mpaka tulipochoka tukarudi kwenye ile nyumba. Tukapanga kwamba itakapofika sa saba tuanze kuswali swala ya adhuhuri. Yasmin alituaga akatuambia kuwa anakwenda kupika chakula cha mchana.
Kwa mustakabali wetu tatizo la chakula halikuwepo. Chakula kilikuwepo kwa Yasmin. Tatizo lilikuwa ni la kuuliwa na Harishi. Kama si tatizo hilo mahali pale pangekuwa ni pazuri pa kuishi. Sikuvutika na kisiwa hicho pekee bali pia nilivutika na Yasmin. Nilifarijika sana kuona jinsi alivyokuwa akitupa moyo na matumaini japokuwa hali ilikuwa tete.
Baada ya Yasmin kuondoka tuliendelea kukaa, hatimaye tukapitiwa na usingizi.
Tulipokuja kuamka yalikuwa majira ya saa nane. Tukaenda kutawadha kwenye maji ya bahari na kuswali swala ya adhuhuri.
Yasmin alikuja saa tisa akiwa amechukua kapu la chakula. Alikuwa amebadili nguo zake na kuvaa mavazi mengine.
“Mmepauka kwa chumvi. Mnasikitisha sana kaka zangu” akatuambia.
“Ndiyo hivyo, tutafanyaje sasa” nikamwambia huku nikimpokea lile kapu.
“Mmeshaswali?” akatuuliza.
“Tumeswali na wewe umeswali?” Na mimi nikamuuliza.
“Mimi naswali kila siku kuomba nusura na kuwaombea na nyinyi. Sijui kama nyinyi mmekumbuka kuniombea”
“Tumekuombea” nikamdanganya. Tulikuwa tumemsahau.
“Mngesema mmesahau kuniombea ningejua hamnipendi”
“Tunakupenda sana. Umetuletea chakula gani?”
“Wali”
“Roho zetu zimekinai, hatutamani hata kula” Shazume akasema.
“Shazume unaanza maneno yako!” Yasmin akamwambia Shazume.
“Unafikiri nakudanganya, mimi sina hamu ya kula kabisa”
“Mbona juzi na jana ulikuwa unakula?”
“Nilikuwa na matumaini”
“Si vizuri hivyo. kuleni japokuwa kidogo mpate nguvu. Mkiacha kula mtakuwa mnajitesa wenyewe. Mimi pia sikula. Nimekuja huku nile na nyinyi”
Yasmin alitoa kile chakula akakiweka chini. Akatoa tasa la maji tukaosha mikono kisha tukaanza kula.
Mimi pia sikuwa na hamu ya kula lakini nilikula kumridhisha Yasmin.
Tuliendelea kula kidogo kidogo hadi Shazume alipomuuliza Yasmin.
“Yasmin ukibaki peke yako itakuwaje?”
“Hatuombei hivyo, tuombee tubaki sote. Ukiomba dua uweke matumaini, isiwe unakata tama”
“Ni kweli Yasmin huwezi kuomba kitu bila kukiwekea matumaini. Kama huna matumaini na kitu hicho kwanini unakiomba?” nikasema.
Shazume akaguna.
“Pamoja na kuomba kwetu bado naona wakati wetu umekaribia sana” Shazume akasema kwa hali ile ile ya kukata tama.
“Shazume usiseme hivyo, mnaweza kunusurika. Harishi ni kiumbe kama nyinyi”
“Lakini mwenzetu amepewa uwezo”
yasmin naye akaguna. Pakawa kimya. Yasmin ndiye aliyeutanzua ukimya huo alipotuambia. “ Jamani tukinusurika nitawachukua Comoro. Nitamwambia baba yangu nyinyi ni ndugu zangu wa damu. Mtaenziwa kama watoto wa rais”
ITAENDELEA

SEHEMU YA 22

“Sidhani kama hapa ni karibu na kwenu Comoro. Mimi nadhani kama tutapata msaada wa kuokolewa tutapelekwa kwanza Zanzibar” nikasema.
“Si vibaya Zanzibar pia ni nyumbani lakini baba akipata habari atatuma ndege siku hiyo hiyo ituchukue pamoja na nyinyi”
“Itakuwa raha sana tukienda Comoro na kupokewa na rais” nikasema.
Shazume alikuwa kimya akitusikiliza. Bila shaka alikuwa anaona tunajidanganya kujifariji. Kwa mawazo yake sisi tulikuwa ni wa kufa tu.
“Si unajua mzazi aliyekwishamkatia tamaa mwanawe halafu anaambiwa amepatikana, atafurahije?” Yasmin akaniuiza.
“Atafurahi sana”
Iliwezekana tulikuwa tulikuwa tunajidanganya kweli kama alivyowaza Shazume lakini tulifarijika. Saa zikapita.
Tulipomaliza kula Yasmin alileta storitofauti tofauti kutuondoa katika mawazo mabaya. Tukawa tunazungumza.
Aliondoka jioni sana. Tukamsindikizakwa pamoja hadi nusu ya njia, tukarudi. Tukakaa kwenye kile kisehemu chetu kusubiri usiku. Hatukujua nini kitatokea kati yetu usiku huo.
SASA ENDELEA
Usiku ule tulikesha macho kwa sababu ya hofu. Tulikuwa tumejilaza chini kila mmoja upande wake lakini hakukuwa na aliyelala usingizi. Mara kwa mara nilimuona Shazume akijigeuza kila upande.
Ilikuwa kati kati ya usiku Shazume aliposhika mguu wangu. Sikujua kama alikuwa anataka kuniamsha au alitaka kujua nilikuwa macho lakini aliponishika nilishituka nikarusha mguu wangu.
“Nini?” nikamuuliza nikiizuia sauti yangu isisikike sana.
“Nimebanwa na haja ndogo” akaniambia.
“Sasa?” nikamuuliza.
“Tunaweza kutoka nikajisaidie”
“Haya tutoke” nikamwambia.
Shazume akainuka na mimi nikainuka. Akatangulia kutoka kwenye mlango. Kulikuwa giza sana. Hatukuweza kuona kwa mbali.
“Twende nje au uani?” Shazume akaniuliza.
“Naona tutoke uani” nikamjibu.
Shazume akaelekea upande wa uani. Mimi nilikuwa nikimfuata nyuma. Alifungua mlango akachungulia uani. Mwezi ulikuwa unaangaza, ua ulikuwa mweupe. Baada ya kuchungulia kwa tahadhari Shazume alivuka kizingiti cha mlango akatoka uani na mimi nikatoka.
Yeye alikwenda upande wake na miminilikwenda upande wangu tukachutama na kujisaidia. Mimi sikuwa na haja ndogo lakini baada ya mwenzangu kuniambiana mimi nikaisikia.
Tulipomaliza haja zetu tulirudi ndani tukajilaza tena. Safari hii tulipojilaza tu usingizi ulitupitia tukalala.
Wakati nipo usingizini niliota Harishi anatufukuza baada ya kutufuma tukiwa na Yasmin kwenye lile jumba lake. Tukaingia katika chumba kimoja kujificha chini ya mvungu wa kitanda. Muda si muda Harishi akafungua mlango na kuingia mle chumbani kututafuta.
Akaona mguu wa Shazume umetokeza chini ya mvungu. Akaushika na kuuvuta. Shazume akawa anapiga kelele kuniita.
Kelele hizo ndizo zilizoniamsha. Nikaamka na kuangaza macho. Nikasikia Shazume akiendelea kupiga kelele kuniita lakini sauti yake ilitokea kwa juu, sio pale chini tulipolala. Nikashituka sana kwa kujua kuwa haikuwa ndoto.
Nikatazama juu. Kwanza niliona kanzu nyeupe halafu nikaona upanga uking’aa. Nilipoona hivyo nilijisogeza zaidi ndani ya makorokoro na kuendelea kuchungulia.
Nilimuona Shazume ameinuliwa juu juu na Harishi. Nikajiambia kumbe ile ndoto ilikuwa ni kweli. Shazume alitolewa mle chumbani. Sikuweza kujua Harishi aliwasili muda gani na kumkamata Shazume.
Bila shaka kilichokuwa kimeninusuru mimi, ni kuwa nililala nyuma ya mlango. Harishi alipoingia alimuona Shazume na kumkamata yeye.
Ile ndoto niliyoota ilikuwa ya kweli. Harishi alikuwa ametuingilia!
Jitihada zetu za kujaribu kumkwepa zilikuwa za bure kwani Harishi alikuwa akitugundua kila tulipokwenda kujificha na sababu ni kuwa alikuwa akifuata harufu zetu kama vile m’bwa.
Harishi alipomtoa Shazume ukumbini, nilimsikia Shazume akipiga ukulele mmoja tu “Nakufa!”. Halafu sikusikia kitu tena.
Moyo ulikuwa ukinienda mbio na nilikuwa nikihema kwa nguvu kama niliyekuwa nafukuzwa. Tukio hilo lilikuwa la ghafla sana kiasi kwamba nililazimika kujiuliza, kama bado nilikuwa kwenye ile ndoto au kilichokuwa kinatokea kilikuwa kweli.
Hofu yangu sasa ilikuwa kwangu. Nilijiua Harishi akimaliza kumuua Shazume ataniingilia na mimi kwani alipoingia humo chumbani alituona tukiwa wawili.
Wazo hilo likanifanya nizidi kujisogeza kwenye makorokoro ili Harishi akiingia tena asinione. Lakini muda ulipita. Sikumuona tena Harishi.
Nikaendelea kukaa hapo hapo hadi nikaona kunakucha. Nikahisi kwa muda ule Harishi atakuwa ameshaondoka. Nikajiburuza kujitoa kwenye yale makorokoro nilikojiingiza.
Nilinyata hadi kwenye mlango nikaufungua na kuchungulia ukumbini. Nilichungulia upande wa mbele na upande wa uani. Niliiona maiti ya Shazume imelala chini kando ya mlango wa chumba tulichokuwemo. Harishi mwenyewe hakuwepo.
Nikatoka nje na kuangalia kila upande. Sikuona kitu. Kando ya ile nyumba palikuwa na mti. Nikapata wazo kuwa nipande juu ya ule mti kujificha. Nikaenda kwenye mti huo nikaupanda na kukaa kwenye tawi mahali ambapo nisingeweza kuonekana.
Wakati nipo juu ya ule mti nilimuona Yasmin kwa mbali akija. Nikajiambia tuliobaki katika kisiwa kile tulikuwa watu wawili tu, mimi na Yasmin.
Sikupenda kujisifu kuwa nilikuwa nina bahati kwa sababu nimenusurika. Nilijua kuwa wakati wangu ulikuwa haujafika. Pengine niliandikiwa niwe wa mwisho kufa.
Historia ya kisiwa hicho tangu tulipofika kila siku alikufa mtu. Leo nimeishuhudia maiti ya Shazume, huenda kesho Yasmin ataishuhudia maiti yangu.
Yasmin alipofika pale nilimuacha aingie mle ndani. Mara moja nikamuona ametoka akiwa amechanganyikiwa. Bila shaka alikuwa ameshitushwa na maiti ya Shazume.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 23

Kile kitendo cha kutoniona mimi inawezekana kilimpa hisia kuwa na mimi nilikuwa nimeuawa kama Shazume. Tatizo ni kuwa mwili wangu hakuuona. Bila shaka alitoka nje kuutafuta mwili wangu.
Alisimama mbele ya ile nyumba akaangalia kila upande kisha akarudi tena mle ndani. Mimi nikashuka kwenye ule mti.
Yasmin alipotoka tena akanikuta nimesimama mbele ya mlango. Akashituka na kuniuliza. “Ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa nimepanda juu ya huu mti” nikamjibu.
Akaja kunikumbatia kifuani kwangu. Kumbe alikuwa analia. Nilipoona analia na mimi nikaanza kulia. Kama Yasmin alikuwa anaona uchungu jinsi tulivyokuwa tunauliwa na Harishi, mimi niliona uchungu nilipowaza nitakavyouliwa na Harishi hapo kesho.
“Buriani Yasmin, ndio tunaagana. Kesho hatutakuwa pamoja tena. Shazume ametutangulia leo” nikamwambia Yasmin.
Yasmin akajifuta machozi yake na kunitazama.
“Wewe hutaniacha, kama ni kufa tutakufa sote. Mwili wangu utalala juu ya mwili wako” Yasmin akaniambia kwa sauti nzito lakini ya kijasiri.
Akaongeza. “Ili uamini kuwa wewe utakufa na mimi turudi kule kule kwenye lile jumba,hatuna sababu yoyote ya kujificha. Akija Harishi nitamwambia atuue sote, Anitangulize mimi kisha wewe”
SASA ENDELEA
“Twende!” nikamwambia Yasmin bila kusita.
Yasmin akanishika mkono tukatembea kuelekea katikalile jumba. Hatukuzungumza kitu tena mpaka tulipofika katika jumba hilo Yasmin aliniuliza.
“Utakunywa uji?”
“Sitakunywa” nikamjibu kwa mkato
“Kwanini?”
“Roho yangu imefadhaika sana”
“Hata roho yangu imefadhaika lakini kama wanipenda tunywe kidogo”
Ilikumridhisha Yasmin nilimkubalia. Yasmin aliniacha ukumbini akaenda jikoni. Baaada ya muda kidogo alikuja na vikombe viwili vilivyojaa uji wa ngano uliotiwa asali.
Alinipa kikombe kimoja kisha aliketi nami.
“Yasmin kweli tumeshindwa kuondoka kwenye kisiwa hiki cha mauti” nikamuuliza Yasmin
“Tutaondokaje wakati tumezungukwa na bahari na hatuna chombo!”
“Nashangaa kwamba hakuna wavuvi wanaokuja katika kisiwa hiki!”
“Hiki kisiwa kiko mbali na pia kinajulikana. Hakuna wavuvi wanaoweza kufika hapa”
“Chombo chetu kilipotuharibikia tulipokiona kisiwa hiki tulidhani tumeokoka kumbe tumekuja kuangamia”
“Hata kama msingekiona hiki kisiwa pia mngeangamia. Mngekula nini? Mngekufa kwa njaa”
“Mimi naona bora kufa kwa njaa kwa sababu njaa itakuwa imekulevya, hutajijua. Kuliko kusubiri….” sikumalizia sentensi yangu.
Niliona nilikuwa najikumbusha kifo kibaya cha kutobolewa utosi kwa ncha ya upanga na kufyonzwa damu na ubongo1.
Siku zote tulizokaa hapa kisiwani niliweza kujikaza na kuondoa hofu licha ya wenzangu kuendelea kuuawa lakini kwa siku ile ambayo nilibakimimi na Yasmin peke yetu, sikuweza kuzuia hofu yangu.
Mawazo ya kifo cha kutobolewa utosi kwa ncha ya upanga na kufyonzwa damu na ubongo yalikuwa yametawala akili yangu.
“Harishi ni kiumbe na sisi ni viumbe. Huwezi kujua Mungu amepanga nini” Yasmin akaniambia.
“Namuamini Mungu na simkatii tamaa”
“Hapo umezungumza kitu cha maana sana. Haifai kukata tama. Nimeshakwambia kama ni kufa leo tutakufa sote. Na mimi ndio nitakufa kwanza”
“Unataka tuendelee kukaa humu hadi usiku”
“Ndiyo. Unafikiri utakwenda wapi?”
“Sioni pa kwenda”
“Basi tukae tu humu”
“Harishi akija atukute pamoja?”
“Ndiyo”
“Aniue mbele yako!”
“Hapana. Ataniua mimi kwanza”
“Mimi sipendi nikusababishie kifo, niache nife mwenyewe”
“Na mimi sitapenda nikusababishie kifo”
“Wewe hutanisababishia kifo, ni Harishi”
“Sikiliza kaka yangu. Sisi tukae hapa hadi usiku.Litakalotokea lolote na litokee lakini kama ni kufa nitatangulia mimi”
Nilimuangalia tu Yasmin, sikumjibu kitu tena. Nikaendelea kunywa uji huku nikiwaza kama ni kweli alikuwa amejitolea nafsi yake kwa ajili yangu.
Maneno yake yalionesha alichokuwa akisema kilikuwa na udhati.
Hata hivyo niliwaza kuwa msimamo wa Yasmin haukuwa na msaada wowote kwangu zaidi ya kuonesha upendo. Ulikuwa msimamo wa kukata tamaa na haukuwana maana.
Atangulie yeye kufa halafu nifuatie mimi? Maana yake ni kuwa sote tutafikwa na mauti. Jambo hilo kwangu lilikuwa tishio ingawa yeye aliona lilikuwa la kijasiri.
Jambo la maana lilikuwa kupata wazo la kutunusuru sote na sio tufe sote.
Tulibaki kimya tukinywa uji. Uji huo niliunywa kwa kujilazimisha ili kumridhisha Yasmin. Kama ningekuwa peke yangu ningebaki na njaa hadi mauti yatakaponikuta.
Nilipomaliza kikombe changu cha uji Yasmin aliniuliza.
“Nikutilie tena?”
“Umetosha’ nikamjibu.
Yeye pia alikuwa amemaliza uji wake akaniambia.
“Basi nenda ukaoge, umeshatia nguvu kidogo”
Pamoja na kukabiliwa na tishio hilo la kifo kusema kweli nilihitajika sana kuusafisha mwili wangu. Nilikuwa nimechafuka sana na nilikuwa sijaoga kwa siku tatu.
Niliona aibu kumwambia Yasmin kuwa sitaoga. Nikainuka.
Yasmin akanipeleka bafuni kisha akaondoka. Nilioga haraka haraka. Nilipomaliza niliondoka bafuni na kumbishia Yasmin mlango.
Yasmin alinifungulia mlango na kuniambia.
“Karibu”
Niliingia mle chumbani alimokuwa. Hamkuwa na kiti. Akaniambia.
Kaa kitandani”
Nikakaa.
“Unajisikia vizuri kidogo?” akaniuliza.
Nilijaribu kutabasamu bila kufanikiwa. Niliishia kubenua midomo tu, uso haukukunjuka.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 24

Yasmin akanipeleka bafuni kisha akaondoka. Nilioga haraka haraka. Nilipomaliza niliondoka bafuni na kumbishia Yasmin mlango.
Yasmin alinifungulia mlango na kuniambia.
“Karibu”
Niliingia mle chumbani alimokuwa. Hamkuwa na kiti. Akaniambia.
Kaa kitandani”
Nikakaa.
“Unajisikia vizuri kidogo?” akaniuliza.
Nilijaribu kutabasamu bila kufanikiwa. Niliishia kubenua midomo tu, uso haukukunjuka.
Endelea sasa
Yasmin akaja kukaa kando yangu.
“Unajua maisha?” akaniuliza. Sikujua alikuwa na maana gani.
“Maisha ni nini?” nikamuuliza.
“Maisha ya mwanaadamu ni mtihani. Lolote linalokufika liwe zuri au baya ni mtihani kwako. Kama wewe ni muumini unatakiwa ulijue hilo”
“Ndio ninalijua”
“Mungu hashindwi kutuokoa sisi waja zake tunaomtegemea yeye ila anatupa mitihani kuona ni kwa kiasi gani tunaweza kuweka matumaini kwake na kwa jinsi gani tunaweza kumuomba kwa unyenyekevu katika siku hii ambayo mimi na wewe tunahitaji sana msaada wake”
Ndani ya moyo wangu nilikiri kuwa Yasmin alikuwa amenieleza maneno ya maana kuliko aliyowahi kunieleza wakati wowote. Nilifarijika kuona juhudi zake za kunitia moyo zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuamsha imani yangu.
Nikajiambia laiti kama ningekuwa na mke kama Yasmin nisingeshindwa kimaisha hata itokee shida ya kiasi gani
Hatimaye jua lilikuchwa. Giza lilianza kuingia. Yasmin aliwasha taa za nyumba nzima. Alikuwa ameniacha mle chumbani mwake, akanifuata na kuniuliza. “Utakula chakula?”
Nikatikisa kichwa.
“Sitakula”
“Hutakula hata kidogo”
Nikaendelea kutikisa kichwa.
“Sitakula”
Yasmin akakaa karibu yangu.
“Usiku ndio huu” akaniambia.
“Kwani Harishi atakuja muda huu?”
“Anaweza kuja wakati wowote kutoka sasa hadi alfajiri”
“Anakujaje?” nikamuuliza Yasmin huku nikiitazama ile chupa iliyokuwa juu ya kabati.
“Anakuja kama moshi. Unajaa ndani ya ile chupa kisha unatoka. Unapotoka unabadilika na kuwa jini”
“Na ni kwanini anakuja hivyo?”
Yasmin akabetua mabega yake
“Sijui lakini ondoa hofu. Mwisho wa mateso yetu utakuwa leo”
Sikusema kitu tena nikanyamaza kimya. Tulikaa kimya kwa muda mrefu. Ile shauku ya kuzungumza ilikuwa imetuishia. Tukaamua kukaa tu kusubiri muda wetu.
Tulikuwa tumekaa chini tumeelekezana migongo. Kila mmoja alielekea upande wake. Yasmin alipochoka au kuhisi kusinzia aliuegemeza mgongo wake kwenye mgongo wangu.
Kitu gani kilimfanya Yasmin asipande kitandani na kulala?
Alikuwa amejitolea kufa na mimi. Alikuwa ameamua akae na mimi pale chini hadi Harishi atakapokuja.
Ilikuwa kama saa saba usiku nywele zangu zilipoanza kunisisimka. Nikayapeleka macho yangu kwenye ile chupa ya Harishi iliyokuwa juu ya kabati. Moyo wangu ulishituka nilipoiona chupa inaingia moshi kwa ndani. Nikamgutusha Yasmin aliyekuwa anasinzia.
“Yasmin!”
“Abee!” Yasmin akaniitikia.
“Tazama ile chupa!”
Yasmin akageuza uso wake na kuitazama chupa hiyo.
“Usimuogope kiumbe aliyeghulukiwa kama wewe. Muogope aliyeghuluku” Ndilo neno aliloniambia Yasmin.
Ule moshi uliendelea kujaa ndani ya ile chupa. Kifiniko cha chupa hiyo kilikuwa pembeni. Moyo haukunipa. Mara moja nikanyanyuka na kwenda kando ya lile kabati. Niisubiri ule moshi ujae kabisa kisha nikakichukua kile kifiniko na kukifunga kwenye mdomo wa ile chupa.
Baada ya sekunde chache nilisikia sauti ya Harishi kutoka kwenye ile chupa.
“Nani amefunga kizibo?”
Sote tukanyamaza kimya.
Ile sauti ikasikika tena.
“We Yasmin si nilikwambia usifunge hiki kizibo?”
Tukaendelea kunyamaza lakini moyo wangu ulikuwa ukienda mbio.
“Fungua sasa!” ile sauti sasa ilifoka.
“Usifungue!” Yasmin akaniambia huku akinifuata.
“Ahaa! kumbe uko na hawara yako! Sasa mtanitambua”
“Sifungui!” Yasmin akasema kwa jazba.
“Nimekwambia fungua, nataka nitoke!” Sauti ikafoka.
“Toka mwenyewe!” Yasmin akajibu.
“Yasmin umechoka kuishi? Nakwambia nitakuua wewe na hawara yako!” Sauti ya Harishi iliendelea kuunguruma kwa hasira.
“Ndio tunavyotaka utuue. Tuue sasa hivi!” Yasmin aliendelea kujibu.
“Wewe kijana nani amekuruhusu ufunge hiki kizibo, hujui kuwa hii ni nyumba yangu?” Sauti ya Harishi ikaniuliza.
“Nimemruhusu mimi akifunge. Nimeshachoka na wewe. Kama unaweza kutoka toka mwenyewe utuue. Sisi tunasubiri kufa tu”
“Yasmin umeamua kunigeuka leo?” Sauti ya Harishi sasa ilukuwa imerudi chini. “Nifungulie mke wangu. Nimekuletea zawadi nzuri”
“Sitaki zawadi yako. Njoo utuue!”
“Nani amekwambia kama nataka kuwaua?”
“Si ndio kazi yako kuua watu. Watu wote wa kisiwa hiki si umewamaliza wewe!”
“He he he!” Harishi alitoa kicheko kilichoonesha wazi kuwa ni cha uongo. Kisha akauliza kwa ukali.
“Sasa utakifungua kizibo au hufungui?”
“Sifungui!” Yasmin akamjibu.
“Wewe kijana fungua kizibo hicho?’ Sauti ya Harishi ikanigeukia mimi.
“Usifungue. Mwache atoke mwenyewe. Sisi tumeshajitolea, liwalo na liwe!” Yasmin akaniambia.
Wakati wote nilikuwa najiuliza kama Harishi alikuwa hawezi kutoka mwenyewe kwenye ile chupa mpaka atuombe sisi tufungue kizibo. Nikataka kupata uhakika kama kweli Harishi alikuwa amenasa na asingeweza kutoka bila msaada wetu.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 25

ILIPOISHIA…
“Wewe kijana fungua kizibo hicho?’ Sauti ya Harishi ikanigeukia mimi.
“Usifungue. Mwache atoke mwenyewe. Sisi tumeshajitolea, liwalo na liwe!” Yasmin akaniambia.
Wakati wote nilikuwa najiuliza kama Harishi alikuwa hawezi kutoka mwenyewe kwenye ile chupa mpaka atuombe sisi tufungue kizibo. Nikataka kupata uhakika kama kweli Harishi alikuwa amenasa na asingeweza kutoka bila msaada wetu.
SASA ENDELEA…
Nikamwambia Yasmin “Tusifungue hii chupa tuone nini kitatokea”
“Wewe achana naye, kama akitoka mwenyewe na atoke, potelea mbali!”
Nilikuwa nimesimama kando ya lile kabati. Yasmin alisimama karibu na kitanda. Macho yetu sote yalikuwa kwenye ile chupa.
Ingawa nilikuwa nimejikaza kiume, hofu ilikuwa ikitambaa kwenye mishipa yangu. Yasmin hakuonesha kuwa na hofu hata chembe. Nilishangaa kuona msichana ambaye siku zote nilimuona dhaifu, siku ile alikuwa amejaa ujasiri usio kifani. Hapo niliamini kweli kuwa Yasmin alikuwa amejitolea kufa kupona.
Ile sauti ya Harishi iliyokuwa ikitoka kwenye chupa ilipotea lakini ule moshi uliendelea kuonekana. Kwanza ulionekana moshi wa rangi nyeusi kisha ukabadilika na kuwa wa rangi nyeupe. Baada ya muda kidogo ulibadilika tena na kuwa wa rangi nyeusi.
Mawazo yangu yote yalikuwa kwenye kifo kibaya kilichokuwa kinatungoja.
. Nilijua kuwa Harishi angekizibua mwenyewe kile kizibo na kutoka. Hapo hasira zake zisingekuwa na kifani. Nilipata wazo la kumwambia Yasmin tukimbie lakini nikajiuliza tutakimbilia wapi usiku ule? Na ni wapi ambapo Harishi hataweza kufika?
Muda uliendelea kupita. Tuliona Harishi hatoki kwenye ile chupa kama ilivyo kawaida yake. Aliendelea kututaka tukifungue kizibo kwa sauti ya upole akiahidi kwamba hatamuua yeyote.
Nikahisi inawezekana kwamba kitendo kile cha kuwahi kukifunga kile kizibo cha cha chupa wakati Harishi yumo ndani ya chupa ile akiwa katika umbile la moshi, kilikuwa kimemzuia kutoka na hakuwa na uwezo tena wa kutoka mwenyewe.
Hapo hapo nikazikumbuka simulizi za wazee wa zamani ziizosema kwamba majini walikuwa wakifungiwa ndani ya chupa na kutoswa baharini pindi wanapofanya makosa.
Kumbe ni kitu kinachowezekana kweli, nikajiambia.
“Sisi tunaiondoa hii chupa!” nikasema kwa sauti ili kusikia Harishi atajibu nini.
“Usiiondoe. Nataka mnifungulie niende zangu” Sauti ya Harishi ikasikika kutoka kwenye ile chupa.
“Hakuna atakayekufungulia muuaji wewe”Yasmin akamwambia.
“Nifungulie nitakurudisha kwenu”
“Mbona siku zote hukunirudisha?”
“Nakwambia kweli kabisa. Ukinifungulia nitakurudisha kwenu Comoro”
“Kwenda zako, mimi si mjinga wa kukufungulia wewe… Bora ubaki humo humo. Siku zako zimeshafika”
Yasmin akanigeukia mimi na kuniambia.
“Twende tukaizike hii chupa”
“Hapana… hapana. Msiizike!” Sauti ya Harishi ikalalamika.
“Mimi naona tukaizike baharini” nikamwambia Yasmin.
“Hapana…hapana. Msiitose baharini!” Ilikuwa sauti ya Harishi lakini hatukuipatiliza.
“Niliwahi kusikiakule kwetu kwamba majini wanafungiwa kwenye chupa na kutoswa baharini” nikamwambia Yasmin.
“Tukiitosa baharini itaelea na kisha itarudishwa ufukweni na mawimbi”
“Labda tuifunge kamba na jiwe ili izame chini”
“Nyinyi msifanye hivyo. Mimi nimeshwambia sitawaua. Nifungulieni niende zangu” Harishi akatuambia.
“Basi tutaifunga na jiwe tizamishe” Yasmin akasema.
“Hamsikii hivi ninavyowambia. Nyinyi mnataka mfe?” Sauti ya Harishi ikasikika kutoka kwenye chupa.
“Utakufa wewe, mbona huwezi kutoka !” Yasmin akamwambia.
“Tusubiri kuche” nilimwambia Yasmin.
“Linaweza likatoka!”
“Usiku huu hatutaweza kwenda baharini”
“Basi tusubiri”
Tukasubiri. Harishi sasa alikuwa amenyamaza. Sauti yake haikusikika tena. Lakini ule moshi uliendelea kuonekana ndani ya ile chupa. Ulikuwa unabadilika rangi kila mara.
Nipoona kunaanza kupambazuka nilijaribu kuishika ile chupa. Ilikuwa nyepesi kama chupa tupu.
Yasmin alileta kapu. Akaniambia tuitie kwenye kapu.
“Tutapata wapi kamba?” nikamuuliza.
“Twende nayo, tutapata kamba huko huko”
Tukatoka nje ya lile jumba. Mimi ndiye niliyeshika lile kapu. Kulikuwa na baridi kali lakini tulijikaza hivyo hivyo. Wakati tunaelekea baharini tuliokota kipande cha kamba na jiwe tukavitia kwenye kapu.
Tulipofika ufukweni mwa bahari tuliitoa ile kamba tukaifunga kamba kisha ile kamba tukaifunga na jiwe.
Tulimsikia Harishi akisema maneno ndani ya ile chupa lakini sauti yake ilikuwa ya chini kiasi kwamba hatukuelewa anasema nini.
Mimi na Yasmin tulijitosa kwenye maji. Tukatembea kwa miguu hadi tulipofika kwenye maji mengi tukaanza kuogelea kwenda mbali zaidi tukiwa na ile chupa tuliyoifunga jiwe.
“Tuizamishe hapa hapa” Yasmin akaniambia.
Nikaiachia ile chupa, ikazama ndani ya maji taratibu. Hatukuiona tena.
“Sasa turudi. Zama za Harishi zimekwisha” Yasmin akaniambia.
Tukaogelea kurudi ufukweni. Tulipofika ufukweni nilimwambia Yasmin.
“Sidhani kama atatoka tena”
“Hawezi kutoka. Labda atokee mtu aifungue ile chupa”
“Na huyo mtu atatokea wapi?”
“Labda wavuvi”
“Wavuvi ni watu wanaojua. Wakiona chupa chini ya bahari hawaifungui. Na pia hakuna wavuvi wanaofika huku”
“Lakini ni kitu cha ajabu. Ujanja wote ule alionao ameshindwa kujitoa kwenye chupa!”
“Ndio maana tunaambiwa kiumbe hakukamilika kwa maumbile wala kwa ujuzi. Mkamilifu ni Mungu peke yake”
“Tungejua mapema tungemfungia tangu tulipofika, tungesalimika sote”
“Hatukujua. Hata mimi ningeweza kumfungia. Sasa nimeshajua sababu ya kunisisitiza kila siku kuwa niweke mbali kile kizibo na nisiifunge hata siku moja”
ITAENDELEA

SEHEMU YA 26

“Lakini ni kitu cha ajabu. Ujanja wote ule alionao ameshindwa kujitoa kwenye chupa!”
“Ndio maana tunaambiwa kiumbe hakukamilika kwa maumbile wala kwa ujuzi. Mkamilifu ni Mungu peke yake”
“Tungejua mapema tungemfungia tangu tulipofika, tungesalimika sote”
“Hatukujua. Hata mimi ningeweza kumfungia. Sasa nimeshajua sababu ya kunisisitiza kila siku kuwa niweke mbali kile kizibo na nisiifunge hata siku moja”
SASA ENDELEA…
“Yasmin tumeepuka kifo cha aina moja, sasa tunakabiliwa na kifo cha aina nyingine” nikamwambia Yasmin.
“Kifo gani tena?”
“Tutaondokaje kwenye kisiwa hiki?”
“Usijali. Mungu mkubwa”
Tukarudi katika lile jumba. Tulipofika tulioga maji baridi. Yasmin alinitolea “Ni kwa nguo za kiume alizokuwa akiletewa na Harishi, akaniambia nivae.
Kwa vile kulikuwa kumeshakucha alipikauji aliouchanganya na asali, tukanywa. Kwa sababu moyo wangu ulikuwa umetulia nilikunywa vikombe vitatu.
Wakati nakunywa kikombe cha tatu Yasmin akaniambia.
“Leo umekunywa uji mwingi kuliko siku zote!”
sababu nina njaa na roho yangu imetulia”
“Yasmin akacheka.
“Jana hukutaka kula kabisa!” akaniambia.
“Ni kwa sababu ya yule mshenzi, alinisababishia hofu sana”
“Sijui ulipata wapi akili ya kufunga kile kizibo?”
“Niiona tu akili yangu ikinituma nikifunge nilipoona ule moshi”
“Pengine ni kwa sababu ya zile dua ulizokuwa ukiomba tangu juzi”
“Pengine”
Wakati tunajadiliana na Yasmin tulishituka tulipoona wazungu wawili wanaume namtu mweusi mmoja wakiingia ndani ya ile nyumba.
Nguo zao zilikuwa zimeroa maji. Walionekana walikuwa wamatoka baharini.
Tukapatwa na uoga kwa vile hakukuwa na watu waliokuwa wakifika katika kisiwa kile.
Tulikuwa tumekaa pale ukumbini Yasmin akanyanyuka na kuwauliza kwa Kiswahili.
“Nyinyi ni kina nani”
“Samahani jamani. Tumekuja kuomba msaada” Yule mtu mweusiakatuambia.
“Mnatoka wapi?”
“Tunatoka Zanzibar. Chombo chetu kilipigwa na dharuba kimepinduka. Tumeogelea hadi tumetokea katika kisiwa hiki”
“Nyinyi ni kina nani” Yasmin akawauliza tena.
“Hawa wenzangu ni watalii wanatoka Ufaransa. Mimi ni Mzanzibari. Nilikuwa nawatembeza kwa boti kwenye Bahari ya Hinndi ndio tukapatwa na ajali”
“Mimi pia najua Kifaransa, ngoja niwaulize” Yasmin akasema na kuwageukia wale wazungu. Aliwauliza maswali kwa kutumia lugha ya Kifaransa. Wazungu hao walimjibu na kufurahi kuona Yasmin alikuwa akizungumza lugha yao.
“Karibuni make” Yasmin akawambia kwa Kifaransa.
Watu hao watatu wakakaa chini.
“Kwanza tunawapa pole sana kutokana na mkasa uliowafika. Mmesema kuwa mnaomba msaada, mtufahamishe mnaomba msaada gani?” Yasmin aliwauliza.
Msaada wowote tu unaostahili kwa binaadamu kwani tumezunguka sana katika kisiwa hiki hatukuona mtu yeyote. Tulichoona ni nyumba tupu na kwingine tulikuta mafuvu na mifupa ya bianaadamu” Mzanzibari alisema.
“Ni kweli” Yasmin alimjibu.
“Ni kwanini?”
“Kwanza mlitakiwa mshukuru kuwa mmefika katika kisiwa hiki katika muda mzuri, vinginevyo na nyinyi mngekuwa kama yale mafuvu mliyoyaona”
“Kwa niaba ya wenzangu nasema kuwa tumeshukuru lakini tuna shauku ya kutaka kujua kilichotokea mpaka mkabaki nyinyi peke yenu”
“Nitawaeleza”
Ndipo Yasmin alipoanza kuwaeleza kisa cha kisiwa hicho. Alianza kwa kujitambulisha kuwa yeye ni binti wa Rais wa Comoro na jina lake ni Yasmin. Akawambia kwamba alisoma elimu yake nchini Ufaransa na ndiyo sababu akawa anajua kuzungumza Kifaransa.
Akaeleza alivyoposwa na mwana wa mkuu wa majeshi nchini mwao lakini siku ile ya harusi akakumbwa na jini anayeitwa Harishi ambaye alimpeleka katika kisiwa hicho na kumgeuza mke wake.
“Sikujua nilivyofika katika kisiwa hiki. Nilijishitukia tu nikiwa ndani ya jumba hili nikiwa sijielewi” Akasema.
Watu hao watatu, wazungu wawili na Mzanzibari mmoja walishikwa na mshangao mkubwa kusikia habari ile.
Yasmin aliendelea kuwaeleza kuwa jini aliyemkumba ndiye aliyekuwa akiua watu katika kisiwa hicho kwa kuwafyonza damu na kula ubongo wao.
“Aliwamaliza watu wote waliokuwa katika kisiwa hiki na kuacha majumba yakiwa matupu. Niliishi peke yangu kwa karibu mwaka mzima” Yasmin alieleza.
Aliendelea kuwaeleza jinsi tulivyofika katika kisiwa hicho na kumkuta yeye ndani ya jumba hilo na jinsi tulivyoanza kuuawa na Harishi mmoja mmoja hadi nikabaki peke yangu.
Ni dhahiri kuwa maelezo ya Yasmin yalikuwa yamewatia hofu watu hao kwani nyuso zao zilizidi kupata fadhaa.
“Mungu ni mkubwa” Yasmin alisema kabla ya kueleza jinsi walivyofanikiwa kumfungia Harishi kwenye chupa na kwenda kuizamisha baharini asubuhi ile.
“Hiki ni kisa cha ajabu kweli kweli. Je tunaweza kwenda kuiona hiyo chupa? mzungu mmoja akauliza.
“Hatuwezi kujua tumeizamisha wapi lakini kwa sasa Harishi yuko chini ya Bahari”
“Je hao watu waliouawa tunaweza kuwaona?”
“Hao mnaweza kuwaona”
“Tunaomba mtupeleke tukawaone kama hamtajali”
Yasmin akanitazama.
“Umeridhika twende tukawaoneshe hawa wageni miili ya ndugu zako?” akaniuliza.
“Nimeridhika” nikamjibu.
Yasmin akawambia wale watu “Twendeni”
Tukaondoka sote watu wanne. Yasmin alianza kuwaonesha miili ya wenzetu waliouawa ambayo ilikuwa karibu na lile jumba. Walikuwa ni wale wenzangu waliouawa mwanzo mwanzo.
Yasmin alikuwa akieleza jinsi watu hao walivyokuwa wakiuawa kila siku mmoja baada ya mwingine.
Tukaenda mbali zaidi katika ile nyumba aliyouawa Haji. Wazungu hao pamoja na Mzanzibari waliyekuwa naye wakauona mwili wa Haji.
Mimi nilitakiwa kueleza alivyouawa Haji. Nikaeleza kwa Kiswahili huku Yasmin akitafsiri kwa kKifaransa.
Baada ya hapo tulikwenda katika nyumba aliyouawa Shazume.
Tuliwaonesha mwili wa Shazume na nikawaeleza jinsi Shazume alivyouawa.
“Hapa ndipo nilipokata tamaa kabisa. Nilijua na mimi ningeuawa leo” nilisema.
Yasmin akaeleza kuwa nay eye alikuwa ameshajitolea kufa kwa ajili yangu.
“Nilisema kama atauawa basi tuuawe sote” akasema na kuongeza.
“Niliona Hakuna haja ya kuendelea kujificha. Nilimwambia mwenzangu twende kule ninakoishi. Harishi akija atukute sote”
Wazungu hao walimsifu Yasmin kuwa alikuwa msichana jasiri na mwenye moyo.
“Kumbe na sisi tungekuja kufa!” Mzanzibari naye aling’aka.
“Ndiyo maana niliwambia mwanzo kuwa mshukuru kwa kufika katika kisiwa hiki katika kipindi cha usalama” Yasmin akawambia.
“Sasa kule nyumbani Comoro wanajua uko wapi?” Yule Mzanzibari alendelea kumuuliza Yasmin.
“Wao hawajui niko wapi na kwa sasa wanaamini kuwa nimeshakufa”
“Je wakikuona tena itakuwaje?”
“Itakuwa mshangao mkubwa. Wazazi wangu hawataamini”
“Ni mkasa wa kutisha kweli na unastahili kuandikwa katika historia ya Comoro”
“Hapo ni kama tutanusurika na nitarudi kwetu kwani kama niivyowambia mwanzo hapa hatutarajii kupata msaada wowote. Hatima yetu tumemwachia Mwenyezi Mungu”
ITAENDELEA

SEHEMU YA 27

“Sasa kule nyumbani Comoro wanajua uko wapi?” Yule Mzanzibari alendelea kumuuliza Yasmin.
“Wao hawajui niko wapi na kwa sasa wanaamini kuwa nimeshakufa”
“Je wakikuona tena itakuwaje?”
“Itakuwa mshangao mkubwa. Wazazi wangu hawataamini”
“Ni mkasa wa kutisha kweli na unastahili kuandikwa katika historia ya Comoro”
“Hapo ni kama tutanusurika na nitarudi kwetu kwani kama niivyowambia mwanzo hapa hatutarajii kupata msaada wowote. Hatima yetu tumemwachia Mwenyezi Mungu”
SASA ENDELEA…
Wakati tunazungumza tulikuwa tumeshaondoka katika ile nyumba aliyouawa Shazume na tulikuwa tunaelekea ufukweni mwa bahari. Tulipofika ufukweni Yasmin akataka tukae kidogo tupumzike kwani tulikuwa tumetembea mwendo mrefu.
“Tangu niletwe katika kisiwa hiki, nyinyi ni wageni wangu wa pili kufika hapa” Yasmin aliwambia wale watu wakati tumeketi.
“Wa kwanza walikuwa kina nani” Mzanzibari akamuuliza.
“Wa kwanza walikuwa ni hao watu saba ambao waliuawa na Harishi na kubaki mtu mmoja mliyenikuta naye”
Yasmin alinionesha mimi.
“Ulikuwa unakula nini?”
“Harishi alikuwa akiniletea chakula”
“yeye alikuwa anakipata wapi?”
“Anaiba kwenye masoko. Harishi ni mwizi na anatembea sehemu nyingi kuanzia kwetu Comoro hadi Afrika Mashariki”
Tulikaa pale ufukweni tukazungumza na wale wageni hadi Yasmin aliposema kuwa anhitaji kurudi nyumbani.
Wakati tunarudi yule Mzanzibari aliyekuwa pamoja na wale wazungu alituambia kuwa boti waliyokuwa wakitalii nayo ilipopigwa na dharuba waliweza kupiga simu Zanzibar kuomba msaada lakini baadaye mawasiliano yalikatika.
“Boti ya polisi wanamaji inaweza kuwa inatutafuta baharini” akatuambia.
“Lakini haitawapata, mmeshafika huku” Yasmin akamwambia.
“Ni vizuri kama tungeendelea kukaa ufukweni ili tuangalie vyombo vinavyopita. Tunaweza kuwaona”
“Sawa. Mnaweza kwenda kukaa. Tutawafuata baadaye”
Mzanzibari huyo alizungumza na wale wazungu na kukubaliana kuwa wabaki kule kule ufukweni. Tukawaacha na kurudi kwenye lile jumba.
“Unajua ni kwanini nimetaka turudi?” Yasmin akaniuliza.
“Sijui”
“Ninataka kupika”
“Ukipika tutawapelekea chakula na wale jamaa?”
“Tutawapelekea. Wameshakuwa wageni wetu”
“Nilitaka kujua hilo tu”
“Jibu umeshalipata?”
“Nimelipata”
“Sawa” Yasmin akaanza kushughulika. Baada ya masaa mawili akawa ameshaivisha wali na mboga ya uyoga.
“Unaonaje ukaenda kuwaita tuje tule nao hapa?” Yasmi akaniuliza.
“Ni sawa. Ngoja nikawaite”
Nikatoka. Wakati nachanganya mwendo kuelekea ufukweni nilisikia mlio wa helikopta. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusikia mlio kama huo tangu tulipofika katika kisiwa hicho. Nikashituka na kutazama juu. Niliona helikopta ikipita chini chini. Ilinipita ikaendelea kwenda na kupote mbele yangu.
Laiti ningekuwa na uwezo wa kuisimamisha, ningeisimamisha lakini sikujua ningeisimamishaje. Nikabaki kuikodolea macho huku nikisikitika.
Mlio wa helikopta hiyo ulikuwa bado ukisikika masikioni mwangu. Ilikuwa kama inayozunguka kwenye hicho kisiwa. Ghafla nikausikia tena mlio huo ukitokea kwa nyuma yangu. Nikageuka na kuitazama. Ilinipita tena na kuendelea kuzunguka.
Ghafla kwa mbele yangu nikasikia kelele za watu zikitokea kwenye miti. Baadaye kidogo nikawaona wale wazungu pamoja na yule mswahili wamevua mashati wakiifukuza ile helikopta huku wakiipungia mashati yao.
Ile helikopta ilirudi tena upande niliokuwa mimi. Sasa mwendo wake ulikuwa wa taratibu na ilikuwa chini chini sana. Ilitafuta sehemu iliyokuwa wazi ikatua. Kitendo cha kutua kwa helikopta hiyo kilinipa furaha na kunirudishia matumaini. Nikajua msada umeshapatikana. Nilitaka nirudi mbio nikamchukue Yasmin lakini naye alishausikia mlio wa helikopta hiyo. Alitoka na kuja mbio.
Ndani ya ile helikopta walishuka watu watatu. Moja alikuwa na mavazi ya kipolisi lakini sikuweza kujua alikuwa polisi wa wapi na pia sikuweza kujua ile helikopta ilitokea wapi na ilikuwa inatafuta nini kwenye kile kisiwa.
Watu hao waliposhuka walitutazama.Yule polisi akauliza.
“Yinyi ndio ambao mliripoti kuwa chombo chenu kinazama?” Alikuwa akimtazama yule Mzanzibar aliyevua shati pamoja na wale wazungu.
“Ndiyo sisi” Mzanzibari huyo akajibu haraka.
“Na hao wataliiwa Kifaransa ndio hawa mabwana?”
Aliwaonesha wale wazungu.
“Ndio hawa niliokuwa nao kwenye boti. Tuliogelea hadi kwenye kisiwa hiki”
“Tumezunguka sana baharini kuwatafuta bila mafanikio. Huku tulikuja kubahatisha tu, ndio tunaona watu wanatupungia. Poleni sana”
“Tunashukurusana kwa msaada wenu”
“Tuliambiwa mlikuwa watu watatu, na hawa watu wengine ni kina nani?”
“Ndio wenyeji wetu tuliowakuta hapa kisiwani, hakuna watu wengine”
“Ninachofahamu mimi ni kuwa hiki kisiwa kilihamwa na watu. Sasa hawa wametokea wapi?”
“Wametueleza habari ya kusisimua sana. Huyu msichana ni binti wa Rais wa Comoro. Aliletwa katika kisiwa hiki katika mazingira ya kutatanisha,mwe
nyewe akiwa hajifahamu. Na ameishi hapa kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa peke yake”
Watu hao watatu waliotoka kwenye helikopta walipatwa na mshangao waliposikia habari ile.
“Eti ni kweli?” Yule polisi akaniuliza.
“Ni kweli” Yasmin akamjibu.
“Wewe ni binti wa Rais wa Comoro?”
“Ndiyo”
“Ulifikaje katika kisiwa hiki kisichokuwa na watu na ulikuwa unaishije?”
Yasmin akaeleza kisa chake kuanzia alivyokumbwa na Harishi katika siku ya harusi yake hadi kuletwa katika kisiwa kile.
Akeleza jinsi alivyokuwa anaishi.
“Wageni wangu wa kwanza kufika katika kisiwa hiki ni huyu kaka na wenzake”
Alinionesha mimi.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 28

“Wametueleza habari ya kusisimua sana. Huyu msichana ni binti wa Rais wa Comoro. Aliletwa katika kisiwa hiki katika mazingira ya kutatanisha,mwe
nyewe akiwa hajifahamu. Na ameishi hapa kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa peke yake”
Watu hao watatu waliotoka kwenye helikopta walipatwa na mshangao waliposikia habari ile.
“Eti ni kweli?” Yule polisi akaniuliza.
“Ni kweli” Yasmin akamjibu.
“Wewe ni binti wa Rais wa Comoro?”
“Ndiyo”
“Ulifikaje katika kisiwa hiki kisichokuwa na watu na ulikuwa unaishije?”
Yasmin akaeleza kisa chake kuanzia alivyokumbwa na Harishi katika siku ya harusi yake hadi kuletwa katika kisiwa kile.
Akeleza jinsi alivyokuwa anaishi.
“Wageni wangu wa kwanza kufika katika kisiwa hiki ni huyu kaka na wenzake”
Alinionesha mimi.
SASA ENDELEA…
“Wenzake wote waliuawa na Harishi na kubaki yeye peke yake. Siku yake ya kuuawa ilikuwa ni leo lakini Mungu mkubwa, amenusurika” Yasmin akaeleza.
Alilieleza tukio zima la kumfungia Harishi kwenye chupa lililotokea usiku uliopita.
“Hatukudhani kuwa ungekuwa mwisho wake. Sisi sote tulikuwa tumeshapanga kufa”
“Sasa ikawaje?” Polisi aliendelea kumuuliza kwa shauku.
“Harishi alishindwa kutoka ndani ya chupa na leo asubuhi tukaenda kuizamisha baharini”
“Ni habari kubwa nay a kushangaza kwa kweli. Unaweza kwenda kutuonesha nyumba uliyokuwa unaishi?”
“Ninaweza. Twendeni”
Yasmin akaliongoza kundi hilo la watu kuelekea katika lile jumba alilokuwa anakaa.
Watu hao waliingia ndani na kujionea jumba hilo lilivyokuwa. Yasmin aliwatembeza sehemu zote za jumba hilo hadi katika chumba alichokuwa analala.
Watu hao walimpa pole na kumsifu kuwa alikuwa msichana jasiri aliyeweza kuishi katika mazingira kama yale.
“Leo imekuwa ni siku yako ya uokozi, wewe na mwenzako” polisi aliyetoka kwenye helikopta alimwambia na kuongeza.
“Washukuru hawa watalii ambao chombo chao kilizama kwani wao ndio sababu ya sisi kufika hapa na kuwagundua nyinyi”
“Nawashukuru nyote kwa jumla, hawa watalii na nyinyi mliokuja kutuokoa” Yasmin akawambia watu hao huku akitabasamu.
“Sasa twendeni tukajipakie tuondoke” Polisi huyo akatuambia.
Yasmin akanitazama.
“Hatutakula tena?” akaniuliza.
“Hata njaa yenyewe siioni, kwaniwewe unahitaji tena kula?”
‘Basi ningojeni nibadili hizi nguo zangu”
Yasmin akaingia chumbani kwake haraka. Yule polisi akawambia wenzake.
“Unaona kama alikuwa anaishi maisha ya kawaida kumbe alikuwa katika mazingira magumu”
“Ameyazoea” Yule Mzanzibari akasema.
“Na pia ni jasiri sana” na mimi nikati akauli. “Mimi nimekaa hapa kwa siku chache tu lakini nimeshachoka. Inakuwaje kwa yeye aliyekaa kwa zaidi ya mwaka?”
Wote wakatikisa vichwa.
Baadaya robo saa hivi Yasmin alitoka. Alikuwa amebadili nguo na kuvaa vazi jingine lililokuwa limempendeza na kufanya aonekane kama malkia. Vazi hilo lilikuwa ni moja ya mavazi aliyokuwa akiletewa na Harishi. Alikuwa amejitia manukato yaliyokuwa yakinukia vizuri na nywele zake aliziweka katika mtindo wa Kikomoro.
Alikuwa ameshika mkoba wa kike mkono mmoja na mkono mwingine alishika begi kama msafiri.
“Hili vazi umelipata wapi?” Yule polisi akamuuliza.
“Nililipata kutoka kwa huyo jini. Alikuwa akiniletea nguo”
“Na hilo begi na huo mkoba?”
“Vyote”
Watu wote wakatazamana kwa mshangao.
Tulitoka katika lile jumba. Wakati tunatoka Yasmin aligeuka juma akalitazama jumba hilo kwa mara ya mwisho. Sikujua alikuwa akiwaza nini. Baada ya kulitazama kwa sekunde chache aligeuka mbele na kuendelea na safari.
“Lete begi nikusaidie” nikamwambia.
Nilimpokea begi. Lilikuwa zito kiasi.
“Umetia nini?” nikamuuliza.
“Mna vitu vyangu”
“Umeamua kuondoka navyo”
“Nataka wazazi wangu wakavione”
“Naamini watafurahi kukuona”
“Na mimi nitafurahi kuwaona”
“Tulifika mahali ilipoachwa helikopta. Rubani akatufundisha jinsi ya kujipakia kwenye helikopta.
“Mnapotaka kupanda helikopta mnainama namna hii ili kukwepa mapangaboi na hata wakati wa kushuka mnainama” akatuambia huku akituonesha jinsi ya kuinama.
Yasmin ndiye aliyetakiwa ajipakie kwanza. Baada ya Yasmin kujipakia tulifuatia sisi.
Sote tulipokuwa ndani ya helikopta, helikopta ikapaa juu na kuanza safari. Nilimuona Yasmin akitazama chini kupitia kwenye vioo. Bila shaka macho yake yalikuwa yanaagana na kisiwa hicho alichokikaa kwa zaidi ya mwaka mmoja akiwa peke yake na asiye na matumaini ya kunusurika.
Kwa upande wangu nilikuwa siamini kuwa tunaondoka. Niliona kama niko kwenye ndoto.
Nasaha za Yasmin zilikuwa zimetimia siku ile. Nilikumbuka kuwa aliwahi kuniambia kuwa aliota ninamuua Harishi na kumuokoa yeye. Wakati huo niliona kama maneno ya mzaha lakini kweli yametimia. Bila kutegemea nimemzamisha Harishi chini ya bahari na hatukutegemea kama angeweza kutoka tena.
Pia nilikumbuka jinsi Yasmin alivyokuwa akinipa moyo kuwa tutaokoka. Na siku ile tukaokoka kweli.
Wakati helikopta ikizidi kuyoyoma na Yasminakiendele
a kukiangalia kisiwa hicho, pengine akikumbuka enzi zake na Harishi, nilikumbuka jambo moja tena jambo muhimu.
Niliikumbuka ahadi yetu ya kumuoa Yasmin pindi tutakaponusurika na kurudi makwetu.
Sikudhani kuwa Yasmin alikuwa angali akiikumbuka ahadi ile japokuwa alinipa siku chache tu zilizopita
Niliamini kuwa kwa vile tulikuwa tumeshaokolewa mawazo ya Yasmin yanaweza kuwa yamebadilika. Kule aliniona kama mwenza wake kwa vile tulikuwa kwenye kifungo. Sote tulikuwa sawa. Lakini tukifika huko tunakokwenda yeye atakuwa binti wa rais mwenye hadhi na heshima, na mimi nitakuwa mvuvi nisiye na thamani yoyote. Sikudhni kama nitakuwa na maana tena kwake.
Helikopta sasa ilikuwa ikipita juu ya Bahari ya Hindi. Yasmin aliacha kutazama chini, sasa akawa anatazama mbele. Kwa vile viti vyetu vilikuwa vinapakana aligeuza uso akanitazama mimi. Nilidhani alitaka kuniambia kitu. Na mimi nikamtazama. Lakini hakuniambia kitu. Nikauona uso wake ukichanua tabasamu. Na mimi nikatabasamu. Baada ya hapo aliugeuza uso wake mbele.
Sikuweza kujua alikuwa akiwaza nini au aliwazia nini aliponitazama na kutabasamu lakini vyovyote ambavyo aliwaza alikuwa ameniwazia vizuri.
Wakati helikopta ikiendelea kupasua bahari niligeuka nyuma kuangalia kwenye vioo vilivyokuwa vimeizunguka helikopta nzima. Nilikuwa naangalia kile kisiwa tulichokuwa tumekiacha kwa mbali. Tuliendelea kukiacha kadiri helikopta ilivyozidi kusonga mbele.
Hatimaye tulikuwa katikati ya bahari. Hatukuona nchi tena. Baadaye tuliona mitumbwi ya wavuvi wakivua samaki. Baada ya muda ambao sikuweza kuukadiria tuliona nchi kwa mbali. Ilianza kutokea mbele yetu kama chuguu ya rangi ya kijani iliyochukua eneo kubwa. Kadiri tulivyozidi kwenda chuguu hiyo ilizidi kuonekana kubwa.
Sasa tuliweza kuona miti kwa mbali. Kijani tulichokuwa tunakiona ilikuwa miti iliyokuwa imeenea katika ardhi. Majumba ya ghorofa na barabara sasa vilionekana waziwazi. Nikajiambia kwamba tulikuwa tumekitokea kisiwa cha Unguja.
Muda si muda tukawa tumeivuka bahari. Sasa tulikuwa tunapita juu ya kisiwa cha kwetu baada ya kukitoka kile kisiwa cha kifo. Nilishukuru sana.
Tuliona vespa, bajaji na magari yanayokokotwa na punda yakipita chini yetu. Nikawa natabasamu peke yangu.
“Yasmin unakuona kwetu?” nikamwambia Yasmin.
“Ahaa ndio hapa!” Yasmin akaniuliza.
“Hapa ni Zanzibar. Kisiwa hiki kinaitwa Unguja”
“Uliniambia wewe unatoka Pemba”
“Pemba ni kwetu na Unguja pia kwetu. Yote ni Zanzibar moja”
Yasmin akatabasamu.
“Nimefurahi kufika kwenu. Nitawaona wazazi wako na ndugu
zako”
ITAENDELEA

SEHEMU YA 29

Tuliona vespa, bajaji na magari yanayokokotwa na punda yakipita chini yetu. Nikawa natabasamu peke yangu.
“Yasmin unakuona kwetu?” nikamwambia Yasmin.
“Ahaa ndio hapa!” Yasmin akaniuliza.
“Hapa ni Zanzibar. Kisiwa hiki kinaitwa Unguja”
“Uliniambia wewe unatoka Pemba”
“Pemba ni kwetu na Unguja pia kwetu. Yote ni Zanzibar moja”
Yasmin akatabasamu.
“Nimefurahi kufika kwenu. Nitawaona wazazi wako na ndugu
zako”
SASA ENDELEA…
Wakati nazungumza na yasmin helikopta ilikuwa inatua kwenye kiwanja cha ndege. Tukaacha mazungumzo na kuchungulia kwenye madirisha. Tuliona jingo la kiwanja cha ndege kwa mbele. Pia tuliona ndege kadhaa zikiwa zimeegeshwa huku wafanyakazi wakienda huku na huko.
Helikopta ilipotua tulishuka
Kwa vile rubani alikuwa akifanya mawasiliano tangu tukiwa juu. Tulikuta maofisa wanne wa polisi wakitusubiri. Polisi tuliyekuwa naye aliwapa maelezo ya zoezi lililofanyika. Akawaeleza pia tulivyopatikana katika kile kisiwa.
Polisi hao walituchukua katika chumba kimoja wakaanza kuwahoji wale wazungu pamoja na mwendesha boti waliyekuwa naye. Baada ya wao kutoa maelezo lilikuja gari likawachukua. Tukaanza kuhojiwa mimi na Yasmin. Maelezo yetu ndio yaliyowaacha hoi maofisa hao.
“Unasema wewe ni bini wa rais wa Comoro na ulikumbwa na jinni aliyekupeleka katika hicho kisiwa mwaka mmoja uliopita?” Afisa mmoja akamuuliza Yasmin.
“Ndiyo”
Niliposema “ndiyo” maofisa hao walitazamana kwa mshangao.
“Hebu tueleze ulivyofikishwa katika kisiwa hicho kutoka Comoro?” Afisa huyo akaendelea kumuuliza.
“Sijui. Ninachokumbuka ni kwamba nilikuwa kwenye sherehe ya harusi yangu nikaanguka na kupoteza fahamu. Nilipozinduka nikajikuta niko katika kile kisiwa ndani ya lile jumba nililokuwa ninaishi” Yasmin aliendelea kueleza.
“Ulijuaje kuwa ulikumbwa na jinni?’
“Wakati nazinduka nilimuona jinni mwenyewe. Aliniambia anaitwa Harishi na kwamba yeye ndiye aliyenikumba na kunileta pale”
“Alikuwa anataka nini kwako?”
“Alikuwa anataka niishi naye kama mke wake”
“Na ukawa unaishi naye?”
“Sikuwa na la kufanya zaidi ya kukubali”
“Ulikuwa unapata wapi chakula na mahitaji mengine?”
“Alikuwa ananiletea yeye chakula na nguo”
“Anavipata wapi?”
“Aliniambia kuwa anaiba kwenye maduka”
“Wapi?”
“Alikuwa anazunguka sehemu nyingi za Afrika Mashariki pamoja na Comoro”
Tumeambiwa kwamba kisiwa ulichokuwa unaishi wewe hakina watu isipokuwa nyumba tupu, ni kwanini?”
“Harishi alinieleza kuwa watu waliokuwa wakiishi katika kisiwa kile aliwaua yeye kwa kuwafyonza damu na kula bongo zao. chakula chake kilikuwa damu na ubongo”
Maafisa hao wakatazamana tena kwa mshangao.
“Chakula chake kilikuwa damu na ubongo wa binaadamu?” Afisa huyo akamuuliza tena Yasmin.
“Ndiyo” Yasmin alimjibu.
“Kwanini wewe hakukula?”
“Mimi alinichukulia kama mke wake”
“Na tuliambiwa kwamba kuna watu saba ambao chombo chao kiliharibika baharini na walifikakatika kile kisiwa, ni kina nani?”
“Mmojawapo ni huyu hapa” Yasmin alinionesha mimi na kuongeza.
“Walifikapale wakiwa watu saba wakauawa na Harishi akabaki yeye peke yake”
“Kwanini yeye hakuuawa?”
“Kuna kisa kirefu kimepita”
“Tunataka tukisikie”
Yasmin akawaeleza yaliyotokea hadi tukaweza kumzamisha Harishi chini ya bahari akiwa ndani ya chupa.
Baada ya Yasmin kuhojiwa nilihojiwa mimi. Nilijieleza kuwa nilikuwa Mzanzibari na kazi yangu ilikuwa uvuvi. Nikaeleza jinsi nilivyofika katika kisiwa kile na kumkuta Yasmin ndani ya lile jumba.
Nilipomaliza maelezo yangu simu zilipigwa sehemu mbalimbali. Haukupita muda mrefu maofisa usalama wa ikulu pamoja na waziri wa nchi ofisi ya raisi walifika kiwanja cha ndege.
Baada ya kupata maelezo yetu, waziri wan chi alimuuliza Yasmin kama kweli alikuwa binti wa rais wa Comoro.
Yasmin akasisitiza kuwa alikuwa binti wa rais huyo na akaomba aunganishwe naye kwenye simu.
Taarifa za Yasmin zilipofika ikulu, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi iliwasiliana na Wizara ya mambo ya nje ya Comoro.
Mpaka inafika saa kumi na moja jioni ndege ya serikali iliyotoka Comoro ikiwa imempakia kaka wa Yasmin ambaye alikuwa kanali wa jeshi pamoja na maofisa usalama wa ikulu ya Comoro ilitua kiwanja cha ndege cha Unguja.
Watu hao walipokewa na mkurugenzi wa usalama na kupelekwa kukutanishwa na Yasmin ambaye mpaka wakati huo nilikuwa pamoja naye.
Kaka wa Yasmin Kanali Umar Sharif Abdilatif alipomuona Yasmin alishituka. Na Yasmin naye alishituka. Walitazamana kwa sekunde kadhaa kabla ya kukimbiliana na kukumbatiana kwa furaha na majonzi.
Maofisa usalama waliotoka ikulu ya Comoro ambao walikuwa wakimfahamu Yasmin nao walishangaa walipomuona kwani taarifa zilizokuwa nchini mwao zilionesha kuwa Yasmin alipotea katika mazingira ya kutatanisha wakati wa harusi yake zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Baada ya maofisa hao kumsalimia Yasmin walithibitisha kwamba alikuwa binti wa Rais Sharif Abdulatif aliyepotea nchini mwao katika mazingira ya kutatanisha.
Wakati huo Yasmin alikuwa akitiriikwa na machozi kwa kumuona kaka yake.
Yasmin aliwaeleza masahibu yaliyokuwa yamemtokea, maelezo ambayo yalimshitua kaka yake pamoja na maofisa hao.
Baada ya kuthibitishwa kwamba Yasmin alikuwa binti wa Rais wa Comoro aliitwa ikulu pamoja na kaka yake. Yasmin aliomba na mimi niwemo kwenye msafara huo. Ombi lake lilikubaliwa. Nilipatiwa mavazi mengine tukapakiwa kwenye gari kupelekwa ikulu ambako tulikutana na rais wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar alimsikiliza Yasmin na kushangazwa na maelezo ya binti huyo wakati akimsimulia masahibu aliyokutana nayo.
“Hata hivyo wewe ni shujaa kwa sababu hukukata tama” Rais alimwambia Yasmin. Pia alinipongeza mimi kwa kunusurika kufa.
“Mkasa uliowakuta ni historia kubwa ya visiwa vyetu” Rais aliendelea kutuambia.
ITAENDELEA

SEHEMU YA 30

Rais wa Zanzibar alimsikiliza Yasmin na kushangazwa na maelezo ya binti huyo wakati akimsimulia masahibu aliyokutana nayo.
“Hata hivyo wewe ni shujaa kwa sababu hukukata tama” Rais alimwambia Yasmin. Pia alinipongeza mimi kwa kunusurika kufa.
“Mkasa uliowakuta ni historia kubwa ya visiwa vyetu” Rais aliendelea kutuambia.
SASA ENDELEA…
Rais wa Zanzibar akawasiliana na Rais mwenzake wa Comoro na kuzungumza naye.
“Binti yako Yasmin ninaye hapa” Rais wa Zanzibar alimwambia Rais wa Comoro.
“Nimepata habari zake na nimeshukuru sana kusikia kwamba mwanangu bado yuko hai. Sisi tulidhani ameshakufa” Rais wa Comoro alisema kwenye simu.
“Ni kweli kwamba alipotea siku ya harusi yake mwaka mmoja uliopita?”
“Nikweli. Lilikuwa tukio la kushangaza sana!”
“Ameniambia alikuwa akiishi katika kisiwa kimoja kisicho na watu na hajui alifikaje katika kisiwa hicho”
“Binti yangu alipata masahibu makubwa lakini nashukuru kuwa amenusurika”
“Huyu hapa, ongea naye”
Rais alimpa Yasmin mkono wa simu ili azungumze na baba yake.
“Asalam alaykum baba!” Yasmin alimwamkia baba yake.
“Wa alaykum salam warahmatulahi wabarakat. Hujambo mwanangu?”
“Sijambo baba. Matatizo yaliyonitokea ni kama ulivyoyasikia”
“Nimeyasikia na nimemtuma kaka yako Umar na maofisa wangu kuja kukuona. Nimeambiwa kuwa mmeshakutana”
“Tumekutana na kaka ninaye hapa”
“Nimefurahi kwamba uko naye kwa rais mwenzangu. Je wewe afya yako ikoje?”
“Afya yangu si nzuri lakini pia si mbaya sana. Nikija huko mtaniona”
“Ulikuwa unaishi vipi huko kisiwani ulikokuwa?”
“Nimeishi kwa taabu tu baba. Nikija nitawaeleza vizuri”
“Ningependa uzungumze na mama yako ili umtoe wasiwasi lakini hatapatikana kwa sasa kwa sababu mimi bado niko ikulu”
“Hakuna wasiwasi baba. Mwambie mama mimi ni mzima. Ni masahibu tu yamenikuta na ishallah nitakutana naye”
”Si mtakuja hii leo?”
“”Kama tutaruhisiwa kuondoka tutakuja leo”
“Sawa. Sasa mpe simu mheshimiwa rais”
Yasmin akampa samu rais wa Zanzibar.
“Umeshazungumza na mwanao?” Rais wa Zanzibara akamuuliza rais wa Comoro kimzaha.
“Tumezungumza kidogo. Unatarajia wataweza kuondoka leo hii kurudi Comoro”
“Kwa vile ndege iko tayari sioni cha kuwazuia kuondoka leo”
“Basi ningependa uwaruhusu kuondoka na mtupatie taarifa muda ambao wanaondoka”
Baada ya maraisi hao kumaliza kuzungumza, rais wa Zanzibar alizungumza na maofisa wake.
“Nataka mhakikishe kuwa ugeni huu unaondoka leo kurudi Comoro. Na kwa upande wa huyu binti apatiwe mahitaji yote ya kibinaadamu kwa gharama ya serikali wakati akiwa hapa nchini kwetu bila kumsahau kijana Zahrani aliyekuwa naye kule kisiwani”
Baada ya rais kutoa agizo hilo aliagana na sisi na kuwatakia safari njema akina Yasmin.
Yasmin alimuahidi rais wa Zanzibar kuwa hataisahau Zanzibar na atarudi kuitembelea tena atakapojaliwa.
Tulipotoka ikulu tulipelekwa katika hoteli ya Bwawani ambako tulipatiwa huduma mbalimbali kama vile chakula, nguo na mahali pa kupumzika. Hapo tulikutana na watu mbali mbali waliopata habari zetu na kututembelea. Walikuja maofisa wa serikali na pia mawaziri.
Kusema kweli nilipata umaarufu mkubwa kutokana na Yasmin. Kwa vile mwenzangu alikuwa binti wa rais na alikuwa akieleza mara kwa mara kuwa kama si mimi na yeye angeangamia, watu waliotutembelea walikuwa wakitupa pole pamoja na kunipongeza.
Maelezo yetu yalionekana kama kioja kikubwa kwa vile yalimuhusisha jini anayeitwa Harishi ambaye alimteka Yasmin nchini Comoro na kumpeleka katika kile kisiwa cha mauti.
Taarifa zilipowafikia waandishi nao walianza kumiminika katika hoteli ya Bwawani kutuhoji na kutupiga picha.
Baadhi ya waandishi hao baada ya kupata maelezo kutoka kwangu na kwa Yasmin, walimuhoji Yasmin kutaka kujua jinsi tulivyoishi katika kisiwa hicho tukiwa peke yetu.
Mwandishi: “Mliishije na Zaharani mkiwa watu wawili wa jinsia tofauti katika kisiwa hicho?”
Yasmin: “Tuliishi kama marafiki”
Mwandishi: “Mlitarajia kuwa mngeokoka?”
Yasmin: “Kusema kweli hatukutarajia ingawa tulikuwa tunaomba sana”
Mwandishi: “Mlikuwa mnalalaje usiku?”
Yasmin: “Usiku wa jana ndio tulilala pamoja lakini pia hatukulala usingizi kwa sababu tulijua kuwa tungeuawa”
Mwandishi: “Sasa umeshaokoka. Unadhani utaendelea kuwa karibu na Zahrani?”
Yasmin: “Bila shaka. Tulipokuwa kule kisiwani nilimpa ahadi Zahrani kuwa kama tutasalimika atanioa”
Mwandishi: “Una maana kwamba umempenda Zahrani?”
Yasmin akacheka kabla ya kujibu. “Nimempenda sana”
Mwandishi: Je sasa unadhani utatimiza ahadi uliyomuahidi?”
Yasmin: “Ndiyo nitaitimiza”
Mwandishi: “Kwa hiyo una mpango wa kuoana na Zahrani?”
Yasmin: “Mpango bado, ni mawazo tu ambayo naamini hayatabadilika”
Mwandishi: “Umetuambia kuwa kabla ya kupotelea katika kisiwa mlichokua mnaishi ulikuwa unaolewa na mwana wa mkuu wa jeshi la ulinzi la Comoro, je kijana huyo akitaka muoane tena itakuwaje wakati umeshamuahidi Zahrani kuwa mtaoana?”
Yasmin: “Nadhani atakuwa ameshaoa”
Kaka wa Yasmin Umar Sharif Abdulatif ambaye alikuwepo wakati Yasmin anahojiwa alithibitisha kuwa aliyekuwa anamuoa Yasmin kabla ya Yasmin kupotea Comoro alishaoa mke mwingine na walikuwa wanaishi Ufaransa. Visiwa vya Comoro vilikuwa koloni la Ufaransa.
Mwandishi: “Kwa hiyo unatarajia kwenda Comoro na Zaharani?”
Yasmin: “Natarajia hivyo”
Mwandishi: “Ndoa yenu itafanyika lini?’
Yasmin: “Siku yoyote wazazi wetu watakaponiidhin
isha kuolewa na Zaharani”
Mwandishi aliyekuwa akimuhoji Yasmin alinigeukia mimi.
Mwandishi: “Je umeyachukuliaje maelezo ya Yasmin?”
Zahrani: “Yamenifurahisha sana”
Mwandishi: “Uko tayari kuoana na msichana ambaye baba yake ni rais wa nchi?”
“Zahrani: “Kama wazazi wake watakubali niko tayari”
Mwandishi: “Mtakuwa mnaishi wapi
mtakapooana, Zanzibar au Comoro?’
Zahrani : “Popote tu tutakapokubaliana”
Mara tu baada ya waandishi wa habari kuondoka maofisa usalama kutoka ikulu ya Zanzibar walinitambulisha kwamba umefika wakati ambapo nitaachana na Yasmin kwa vile muda wa safari yao ya kurudi Comoro ulikuwa umefika.
Kauli ile ilinivunja moyo hasa kwa vile nilitegemea kuondoka na Yasmin. Yasmin akawaomba maofisa hao waniache niende naye Comoro.
“Hatumzuii mtu yeyote kwenda mahali popote anapotaka ila Zahrani hana hati ya kusafiria” Afisa mmoja alimwambia Yasmin.
Itaendelea.

SEHEMU YA 31

Mwandishi: “Mtakuwa mnaishi wapi
mtakapooana, Zanzibar au Comoro?’
Zahrani : “Popote tu tutakapokubaliana”
Mara tu baada ya waandishi wa habari kuondoka maofisa usalama kutoka ikulu ya Zanzibar walinitambulisha kwamba umefika wakati ambapo nitaachana na Yasmin kwa vile muda wa safari yao ya kurudi Comoro ulikuwa umefika.
Kauli ile ilinivunja moyo hasa kwa vile nilitegemea kuondoka na Yasmin. Yasmin akawaomba maofisa hao waniache niende naye Comoro.
“Hatumzuii mtu yeyote kwenda mahali popote anapotaka ila Zahrani hana hati ya kusafiria” Afisa mmoja alimwambia Yasmin.
sasa endelea…
Ilikuwa kweli sikuwa na hati ya kusafiria na hata Yasmin hakuwa nayo lakini kwa vile aliingia Zanzibar kidharura alilazimika pia kuondoka kidharura.
Yasmin akanitazama kwa butwaa.
“Hivi huna hati ya kusafiria?” akaniuliza.
“Sina” nikamjibu huku nikitikisa kichwa.
“Kuna kipindi ulikuja Comoro, ulifikaje bila ya hati?”
“Sina maana kwamba sina kabisa. Hati yangu ya kusafiria iko pemba”
“Kumbe unayo. Sasa tutafanyaje?”
“Amua wewe”
“Sasa sikiliza” Yasmin alitaka kusema kitu lakini akasita na kumtazama kaka yake. “Kaka kama una dola mia tano mpatie Zahrani zimuwezeshe kuja Comoro”
Umar alitoa dola mia tano hapo hapo na kunipa.
“Hizo zitakuwezesha kwenda Pemba kuonana na ndugu zako na kujiandaa kwa safari ya kuja Comoro siku yoyote utakayopenda” Yasmin akaniambia.
Umar akanipa namba za simu za kuwatambulisha wakati nitakapokwenda Comoro.
Nilikubaliana na Yasmin kwa shingo upande. Mwenyewe alijua kuwa sikuridhika kuniacha Zanzibar ingawa nilipatiwa nauli ya kwenda Comoro siku nitakayopenda kuondoka.
Baada ya Yasmin kuniambia hivyo aliishia kunitolea tabasamu lenye mchanganyiko wa furaha na majonzi.
Mimi sikuweza kutabasamu. Kwa siku chache nilizokuwanaye nilikuwa nimeshamzoea Yasmin. Kitu muhimu ambacho nitakikosa kwake ni ile hewa ya mwili wake. Alikuwa na hewa tamu nay a kusisimua ambayo huisikia kila ninapokuwa karibu naye.
Hewa ile ilikuwa inaniliwaza kuliko manukato ambayo hujitia mwilini mwake.
“Nitasubiri. Sina la kufanya” nikamwambia kwa sauti nzito ya huzuni.
“Tutakutana mahabuba wangu. Sitakuacha” Yasmin akaniambia kwa sauti ya chini. Hakutaka isikiwe na wengine.
Sasa msafara ulikuwa unakwenda kiwanja cha ndege. Na mimi nililazimika kuwasindikiza nikiwa pamoja na maofisa usalama.
Giza lilikuwa limeshaanza kuingia na taa za mji wa Unguja zilikuwa zimewashwa. Tulikuwa katika basi dogo ambalo liliweza kutupakia sote. Gari la maofisa usalama lilikuwa limetutangulia.
Tilipofika kiwanja cha ndege niliagana na kaka wa Yasmin kisha nikaagana na Yasmin mwenyewe. Kwa mara ya kwanza Yasmin hakuona aibu kunikumbatia mbele ya macho ya kaka yake.
Kwa mujibu wa tamaduni za Wangazija wa Comoro, kitendo hicho kwa watu wa jinsia tofauti ambao si ndugu kilikuwa ni cha faragha sana. Lakini Yasmin alikifanya kuonesha mapenzi yake kwangu.
Wakati ananiachia aliupeleka haraka mkono wake kwenye macho yake kufuta machozi yaliyoanza kumtiririka.
Kwaheri, tutaonana” akaniambia na kunisisitizia “Nitakusubiri Comoro. Usichelewa kuja. Usiwe na majonzi, tutaonana”
Yasmin alijaribu kutabasamu licha ya uso wake kujaa huzuni. Tabasamu lake lilinifariji sana.
Maofisa usalama walikuwa wakimtazama Yasmin alivyokuwa ananiaga kabla ya kugeuka na kuungana na wenzake’
Sikuondoka hapo kiwanjani hadi ndege waliyosafiri kina Yasmin iliporuka na kuanza safari.
Nilijisikia mwenye majonzi sana lakini nilijikaza.
“Wewe hujui kama yule ni binti wa rais?” Afisa usalama mmoja aliniuliza wakati tunaondoka kiwanjani hapo.
“Ninajua” nikamjibu.
“Sasa mbona unataka kututia aibu. Unataka kwenda naye wapi?”
Swali hilo lilinikera sana. Nikamtazama yule afisa usalama aliyetaka kunishushua.
“Yeye ndiye aliyeomba aondoke na mimi” nikamwambia.
“Wewe pia si ulikuwa unataka kwenda?”
Nilijua kuwa yule afisa alikua ameona donge. Nilitaka kumuuliza “Sasa kinakuuma nini?” lakini nilimstahi. Nikamwambia. “Ni baada ya yeye kutaka aondoke na mimi”
“Sasa yule ni binti wa rais, wewe huwezi kufuatana naye. Ukifika huko utasema nini?”
Niliona nisijibizane naye. Nikaamua kubaki kimya.
Maofisa hao walinipakia kwenye gari na kunirudisha kule hoteli. Wakaniambia nitalala pale na asubuhi nirudi Pemba.
“Tutakufuata asubuhi tukupeleke bandarini” Afisa mmoja akaniambia.
Nikamjibu “Sawa”
Nililala pale hoteli. Usiku kucha nilikuwa namuwaza Yasmin. Asubuhi simu iliyokuwa mle chumbani ikaita. Nilipoipokea niliambiwa nipokee simu yangu kutoka Comoro.
Hapo hapo nilisikia sauti niliyoitambua kuwa ni Yasmin ikinisalimia.
“Subalheri muadhamu (asubuhi njema mpendwa)”
“Subalnuur azizi (asubuhi yenye nuru mremo)” Kwa kutaka kuhakikisha kuwa alikuwa Yasmin nikamuuliza “Wewe ni Yasmin?”
“Naam, ndiye mimi. Nilitaka kukujulia hali”
“Nashukuru, mie sijambo. Je mlifika salama?”
“Alhamdulilahi. Tulifika salama. Nimekutana na wazazi wangu na ndugu zangu na pia wananchi wenzangu. Wamefurahi kuniona na mimi nimefurahi kuwaona. Kumbe bado uko hapo hoteli?”
“Ninaondoka hii asubuhi kwenda Pemba na mimi nikaonane na wazazi wangu pamoja na ndugu zangu. Najua wameshanikatia tama”
“Ni kweli. Basi ukifika unaweza kunipigia kwa kutumia zile namba ulizopewa na kaka”
“Sawa, nitakupigia”
“Ongea na mama yangu”
Mara nikasikia sauti nyingine ikiniuliza. “Hujambo mwanangu?”
“Sijambo mama. Habari za huko?’
“Huku ni salama. Unajisikiaje hali yako?”
“Hali yangu ni nzuri. Nashukuru”
“Pole sana kwa masahibu yaliyowafiaka”
“Tumeshapoa mama”
“Tunakusubiri kwa hamu huku. Utakuja lini?”
“Siku ya kuja nitawambia. Kwanza nataka nifike Pemba nikawaone wazazi na ndugu”
“Basi utatujulisha siku utakayokuja tukupokee”
“Asante mama. Nitawajulisha”
“Nampa simu Yasmin”
“Haya mpe”
“Hallo Zahran!” Sauti ya Yasmin ikasikika.
“Ndiyo Yasmin”
“Usijali kuwa mbali nami, ishallah tutakuwa pamoja. Nimeshamueleza mama yangu kilicho ndani ya moyo wangu kuhusu wewe”
Aliponiambia hivyo, mwili wangu ulisisimka.
“Hakuna tatizo Yasmin. Wewe pia usijali”
“I miss you” Yasmin akaniambia kwa kingreza.
“Sikujua jinsi ya kujibu, nikabaki kucheka. Yasmin naye akacheka.
“Bye bye (baibai): akaniaga.
“Bye…”
Simu ikakatwa.
Je Zahrani ambaye ni mvuvi na masikini asiye na elimu atamuoa Yasmin binti wa rais?

@Swahili Pride @Sponsor mature @Scoundrel @Meria Mata @SnazzyKenyan @Brikicho Bantureh @

so you want me to read all this swahili???
wueh.
sinitaumwa na kichwa.
nipe summary kigogo alafu nitaisoma usiku

Iendelee

[SIZE=6][FONT=book antiqua]Kutana na PSEUDEPIGRAPHAS BLOG[/FONT][/SIZE]
[SIZE=6][FONT=book antiqua]Ni blog yenye vitabu vya riwaya, simulizi , chombezo plus, hadithi zaidi ya 1000
Click link ujionee.[/FONT][/SIZE]

[ul]
[li]Home[/li][li]UCHAWI UPO SHUHUDA ZA KWELI[/li][li]SIMULIZI FUPI NA STORY ZA MAPENZI[/li][li]CHOMBEZO[/li][li]SIMULIZI ZA MAISHA[/li][li]SIMULIZI ZA KUSISIMUA[/li][li]CHOMBEZO PLUS+[/li][li]SIMULIZI ZA KICHAWI[/li][li]SIMULIZI ZA KIJASUSI[/li][/ul]