kwa muktadha Wa kibiashara, import Na export zaitwaje
Nina swali moja mwalimu,
Wheelbarrow yaitwaje kwa kiswahili?
toroli au rukwama
Asante, toroli nikaa imetoka kwa trolley, rukwama nimeskia Leo
niliambiwa hata pia mkokoteni unafaa kuitwa rukwama, basically any type of cart can be a toroli or rukwama
Ni kweli. Hata ‘handcart’ huitwa rukwama na siyo ‘mkokoteni’ kama tunavyojua katika lugha ya kawaida.
[U][B]
MAJIBU
ZOEZI
Nyambua maneno yafuatayo katika hali zote tano.[/B][/U]
[B]-Kula-Kuliwa,kulwa,kulia,kulana.
-Kunywa-Kunywiwa,Kunywa,Kunywia/kunywea,kunywiana/kunyweana
-Piga-Pigiwa, Pigwa, Pigia, Pigana.
-Pika-Pikiwa, Pikwa, Pikia, Pikiana.
-Lala-Laliwa, Lazwa, Lalia, Laliana.
-Tembea-Tembelewa, Tembezwa, Tembelea, Tembeleana.
-Ingiza-Ingiziwa, Ingizwa, Ingizia, Ingizana.
-Andika-Andikiwa, Andikwa, Andikia, Andikiana.
-Tega-Tegewa, Tegwa, Tegea, Tegana.
-Lia-Liliwa, Lizwa, Lilia, Lizana.
-Bana-Baniwa, Banwa, Bania, Baniana.
-Kaza-Kaziwa, Kazwa, Kazia, Kazana.
Kongole kwa kina @Mjuaji , @Okwonkwo , @123tokambio , @introvert , @Eng’iti , @Meria Mata , kwa juhudi zenu. @Yule Karis Black hata nawe kongole kwa kushiriki. @Eng’iti , @Mjuaji na @Okwonkwo wamezoa alama za juu kenye hili zoezi.
Tunapolala tukumbuke kuwa ‘tusilolijua ni usiku wa giza tu’.
Alamsiki![/B]
:D:D:D:D:DUbunifu wako umenichekesha. Hata hivyo umejaribu sana.