Kiswahili endelevu

Samahani nilikuwa nimesahau swali lako la pili.
Gwiji Simaro Massiya lutumba Ndomanueno bado yuko hai na anakiongoza kikundi cha Bana OK Jazz yaani watoto wa OK Jazz ile bendi ya Franco.
Ana umri was miaka sabini na saba kwa sasa.

1 Like

Kula vya mwiki ni kunyandulia dem WA mwiki Kwake.

2 Likes

:D:D:D

Zunguka mbuyu--------danganya toto jinga
-Laza damu…zembea
-Kuwa kisu butu…ambulia patupu
-Kuwa tumbo moto…patwa na waswasi
-Kata kamba…kufa, aga dunia

1 Like

Umejaribu sana. Umekosea 'Kuwa Kisu butu.

Hapo sawa kaka.

:D:D Jaribu kutumia Kiswahili. Umepata: Kupiga Chafya, Kupiga miguu, Kupiga miayo, Kuwa tumbo joto na Kata kamba japo tu tumia Kiswahili.

1 Like

Jaribio zuri. Jaribu kutumia neno moja kuelezea semi ile ya kwanza.

1 Like

:D:D:DSina cha ziada!

Hongera!! Umepata maswali uliyojaribu kaka @bababibitoto .

Kuchemua!! Shabash! Hilo ndilo jina mwafaka.

MAJIBU
[B]Elezea maana ya Semi zifuatazo
-Kupiga Chafya…Kuchemua.
-Kupiga miguu…Kutembea kwa miguu.
-Kupiga miayo…Kufungua kinywa kama dalili ya usingizi au njaa.
-Kula vya mwiki…Kula chakula kilicholala. cc @Web Dev
-Kula murututu…Kuvumiliama mambo machungu au mazito.
-Zunguka mbuyu…Kupokea hongo.
-Laza damu…Zembea au kuwa mvivu.
-Kuwa kisu butu…Kuwa mjinga.
-Kuwa tumbo moto…Kuwa na wasiwasi.
-Kata kamba…Kufa/kuiaga dunia.

Shukran kwa wote walioshiriki mtanange huu wa leo. Kila mara tujikumbushe kuwa ‘Jitihada haziondoi kudura’ na ‘Bandu bandu huisha gogo’.
Alamsiki.

[/B]

4 Likes

nina KATA MAJI

1 Like

Safi kaka

1 Like