Kiswahili endelevu

Umeelezea kwa uzuri kabisa.

Nimeishi pwani miaka nne pale mtaa inaitwa Ukunda

CHEMSHA BONGO

Tafsiri maneno yafuatayo:-
i) Yardstick…Kigezo . Kongole @mukuna
ii) Ethics…Maadili. kongole @mukuna
iii) Doll(child’s toy)…Mwanasesere au Sesere. kongole @mukuna
iv) Remote Controller(the gadget)…Kitanzambali ama Kitenzambali. Kongole @123tokambio
V) Bainisha kati ya Moyo na Roho…Moyo ni sehemu ya mwili inayopiga damu mwilini: Roho ni nafsi iliyomo ndani ya mwanadamu ambayo haionekani kwa macho lakini ina uhai wake. Kongole @MISCHIEF na @Colombo-Combolo
Vi)[B]Maana tatu au zaidi ya neno ‘chungu’.-Chungu: mdudu
-Chungu: chombo cha kupikia mfano wa nyungu
-Chungu; Ladha kali mdomoni
-Chungu; wingi wa vitu; Kwa mfano -Xuma ana pesa chungu nzima. Kongole @mukuna ,@Okiya

Shukrana kwa wote walioshiriki bila kuwasau kina @Young na @coldpilsner .

Msemo wa leo: Ukijua hu, na hu hujui!
[/B]