Kiswahili endelevu

:eek::eek:…:D:D:D Karibu ndugu!

:D:DNimekupa alama ya upato kwa kujaribu kaka lakini sivyo.

Uko sawa lakini jina halisia ni gunzi.

Majibu ya Leo:
CHEMSHA BONGO

Tafsiri maneno haya;
i) Nauseau…kichefuchefu/kitefutefu
ii) Wink………Konyeza
iii) Mirage…Mazigaziga/Sarabi/mangazimbwe
iv) Honeymoon…Fungate
v) Elezea ‘miziki ya ala’ ni miziki aina gani?..Miziki ya ala ni miziki bila sauti za waimbaji ‘instrumentals’ kwa kiingereza.

Shukran kwa washirika wote wa leo hata wale walijaribu kama kina @uncle nyam , @aviator , @It’s Le Scumbag , @Six Thousand Blankets , @Energizer , @Colombo-Combolo , @introvert , @dabu , @Mjuaji , @4makind , @bababibitoto , @Nottybwoy .

Methali ya Leo: Mchama ago hanyeli huenda akawia papo!

@xuma methali ya Leo ina maana mtu hafanyi mabaya mahali alipo huenda akakawia sehemu ile…natumai nimepata

Umepata.Mchama ni msafiri, ago ni safari, hanyeli ni hanyi au kwenda choo, kwenye njia anayo pitia maana huenda akarudia papo hapo Siku nyingine. Kongole kaka.

Like na love zote ninatumiwa kwa kupenda lakini Luna tofauti.
Love inahusiana na kupenda kwa ndani zaidi kwa mfano aina ya mapenzi ya mahaba au huba.
Like inamaanisha penda(lakini si kwa undani kama love) au tamani.Like pia vilevile hutumiwa kama fananisho kwa mfano ’ mzuri kama mwezi’. Like pia hutumiwa kama ‘simile’ kwa kiingereza kwa mfano ‘Una nguvu mithili ya farasi’.

Kesho tutashughulikia hesabu.