Kiswahili endelevu

Hehehe…umenimulika sana. Nilikwambia kikiumana narejelea nakala yangu ya shilingi hamsini tu:D

-Squirrel…Kichakuro Naona kuna nyengine washajibu, nyengine ni kama nishagonga mwamba hata kabla ya kujaribu

millipede humaanisha jongoo

centipede humaanisha tandu

Umepata Cheetah lakini centipede na millipede si kitu kimoja ingawa jibu la jongoo liko sawa.

Hugo nyoka ako na jina lake sahihi.Umepata bung’o na duma.Hongera.

:D:DSivyo kaka!

Sivyo kaka.

Hapo umejaribu isipokuwa tu ni Kuchakuro.

[B]MAJIBU YA LEO

CHEMSHA BONGO

Elezea haya majina kwa Kiswahili:
-Millipede…jongooo/majongoo kongole @mukuna ,@dingoo_wa_ingoo
-Leech…mruba au kaka
-Centipede…tandu; hongera @mukuna Na @dingoo_wa_ingoo
-Cheetah…duma; hongera @mukuna ,@Mjuaji ,@Colombo-Combolo ,@dingoo_wa_ingoo
-Cobra…Swila @Chifu na @Mjuaji jibu ndilo hili.Hakuna aliyepata hili swali.
-Caterpillar…Kiwavi ama funza ama bungu.Hongera @mukuna
-Tsetse fly…Mbung’o wala si ‘bung’o’ kama vile @Chifu na @Mjuaji walinakili.Kongole @mukuna .
-Wasp…Nyigu. @mukuna ulikosea herufi ya ‘n’.Siyo ‘nyingu’.
-Squirrel…Kuchakuro au kuchakulo au chindi.Kongole@123tokambio kwa kupata alama kadhaa kwa jibu lako.
-Praying Mantis…Kivunja jungu. Hongera @mukuna kwa kuling’amua hili swali.

Shukran kwa wote walioshiriki hata kama hamkupata majibu sahihi. Kina @MISCHIEF , @IPDEV ,@4makind ,@Randy ,na wengineo. [/B]

Msemo wa leo ni kumbuka meli yetu ishang’oa nanga na ‘msafiri ni aliye bandarini !’

:smiley:

Cheetah - chui
Cobra - mamba

Cheetah ni duma
Leopard ni Chui
Crocodile ni Mamba kaka.