Kiswahili endelevu

Neno lililopigiwa nguvu.

Kitabu cha majilio au matukio.

MAJIBU
CHEMSHA BONGO

-Andika majina sahihi ya maelezo yafuatayo;
i) Aina ya kofia yenye sehemu inayotokelezea mbele(cap) huitwa…Chepeo
ii) Aina ya kizibo cha kufungia na kufungulia maji huitwa…Bilula
iii) Mahali maalum palipochimbwa ukutani ili kuhifadhia nguo ni…Shubaka
iv) Kiti cha kukalia chenye miguu mitatu na kisichokuwa na kiegemeo huitwa…Kigoda
v) Kifaa maalum kwa ajili ya kuleta ubaridi wakati wa joto(fan) huitwa…Panka au upepeo au kipepesi kongole @123tokambio
vi) Bainisha kati salamu za Masalkheri na Sabalkheri.
-Masalkheri hutumiwa asubuhi na Sabalkheri hutmiwa jioni. Kongole @dingoo_wa_ingoo ,na @ziga
vi) Ukisalimiwa Masalkheri au Sabalkheri, mtu hujibu…Alkheri
vi) Air conditioner kwa kiswahili ni…Kiyoyozi kongole @123tokambio
vi) Carpet kwa kiswahili ni…Zulia. Kongole @Bingi

vii) Bill of exchange/Treasury bills kwa kiswahili ni…Hawala @Okiya ungefaa kujua hili.

Shukran kwa wote walioshiriki bila kusau @It’s Le Scumbag , @wheelz , @duad ,@Young , @ziga ,@123tokambio ,@Bingi , @dingoo_wa_ingoo ,na @coldpilsner na @jumabekavu kwa kupitia. @gashwin, @Meria Mata , @introvert , @Mjuaji ,@mukuna ‘msicheze mbali’.

Msemo wa Leo; Mchimba kisima huingia mwenyewe.
Jumapili njema.