Kutumia majina halisi kutaivuruga JF!

dikteta jiwe anachekesha

Hapo watanikosa na tukikaa kimya Ndio kila Mtu atachukua chake Kwenye nchi ya Kwetu wenyewe

Wewe baki huku huku jamaa yangu. Ukitaka kukirudia cheo chako cha huko jipange kupimwa mkojo.

Sio tu kuwa huna akili, hata kuandika kitu kikaeleweka hujui pia.

Majina yetu halisi yakitambulika kuna watu watatula nyama.

Nadhani TCRA wanapaswa kuendesha vipindi vya uelimishaji umma kuhusu sheria ya mtandao.

Hakuna popote watu wanapotakiwa kutumia majina halisi, bali kwenye usajili ndipo lazima wamiliki wajue majina halisi ya members wao, ili members wakifanya makosa ya kimtandao, mmiliki awajibike kuwataja.

Hili hufanyika kwa kutumia real e mail na kuweza ku log in kwa kutumia e mail, google account, FB or twitter ambazo pia zina contact details.

Members watakuwa verified kwa real phone numbers ambazo ziko registered kwa real names. Hii ni kwenye registration only, lakini members wataendelea kuwa huru kutumia pen names.

Mfano mimi jina langu ni Pascal Mayalla, kwenye registration nitaregister real name, lakini kwenye login name, nitatumia Pasco wa JF, ili siku Pasco wa JF, akivunja sheria, TCRA, Polisi or Tiss wanaelezwa huyu Pasco wa JF ni fulani na kuchukuliwa hatua.

Utaratibu huu mpya, utapunguza ladha ya majadiliano, na kutishia usalama wa whistle blowers, ila pia utapunguza uongo, uzushi, kutukana na ujinga ujinga wa mitandao.

P.

Kwa hiyo tutaenda ofis za JF na kitambulisho cha mpiga kura kujisajili? wanafikiri kila mmoja anatokea koromije!!

Maamuzi mengi yanafanyika ambayo jamii inaathiriwa na hayo maamuzi bila kupewa Elimu husika.

Wenye mamlaka ya kiuongozi bado wana tatizo sana, tatizo kubwa hawataki kushaurika mwishowe wanaharibu kila wafanyapo maamuzi.

Wakijenga tabia ya kushaurika bila kujali nani katoa ushauri, uongozi utakuwa rahisi sana

Melo atatupoteza great thinkers wa udaku gossip na umbea

Ngoja tuone…

Kwa sasa JF original unaweza kutumia PM pekee, kwa hiyo unataka kusema ukiona umeweza kupost new topic ujue taarifa zako halisi zishafahamika…

Cc: @Mahondaw

Acha utani smart watu tutakimbiana ujue tehtehteh.

hadi wewe umekuja huku?

Haitopendeza kwa kweli
Nalog off

@Pascal Mayalla hoja hapa ni kwamba huo uzushi ni nani anayesema huu ni uzushi au si uzushi, na ni kipimo gani kitakachotumika kujua huu ni ujinga jinga na huyu katukana. Kwa mfano Mkapa alisema kwamba wanaounga mkono wapinzani ni wapumbavu, lakini je mtu wa kawaida naye akisema Mkapa ni mpumbavu atasalimika?

Kama ni kweli JF ndiyo imekufa rasmi Mkuu kwani wanachama watakaoubali kutumia majina yao ya kweli hata wale ambao hawaligusi jukwaa la Siasa hawatafika hata 50.

No hauendi kujisajili na kitambulisho bali watatumia email verification or number ya simu iliyosajiliwa kwa jina lako.

Hivyo bado unaweza kujisajili kwa majina bandia kwa kufungua email kwa kutumia jina bandia mfano mimi nataka kuitwa Mashokolo Kubangashe, kabla sijajisajili jf, naanza kuirejesta e mail ya Mashokolo Kubanga, Facebook account ya Mashokolo na Twitter, kisha najiunga jf kwa jina la Mashokolo au jina lolote.

Lengo sio kuzuia majina bandia au uhuru wa maoni, bali ku establish responsible blogging, members wawe more responsible and conscious kuwa wakisema uongo, uzushi au kutukana, wanaweza kuwa pinned down.
P

Hii Sky Eclat ina gmail, what’s up nimeshindwa Facebook na instagram kwani niliosoma nao, ninaofanya nao kazi au ninao kaa nao huku kwetu Kwamtogole hawamjui Sky Eclat

Mkuu Mwifwa, hapa nakubaliana na wewe, nchi yetu, serikali yetu na viongozi wetu, wana tatizo sana la kututumia ushirikishwaji katika kupanga mipango yake.

Kuna mipango mingi mizuri serikali inapanga, lakini kutokana na ukosefu wa wa ushirikishwaji, ushirikishwaji duni na kutokuwepo kwa utoaji elimu kwa umma, wananchi na wadau wanakuwa hawajui kinachoendelea kwa sababu hawajashirikishwa, hawajaelimishwa, na sometimes wrongly informed, matokeo yake ni kuleta upinzani katika jambo hilo.

Hivyo ndivyo ilivyo hii sheria ya mitandao. TCRA ilikuwa na very effective PR department enzi za Innocent Mungy, lakini sasa sijui what happaned, kiuekweli kwa sasa PR na utoaji wa public information programs ni almost nil.

Nimezungumza na mhusika nikamshauri, kuwa japo mmechelewa lakini chelewa ufike, ili kuondoa hii mikangamano, TCRA wajitokeze sasa na kuifafanua hiyo sheria na kinachoendelea sasa ili kuondoa hii confusion.

Paskali

Umeshindwa nini ku register whatsapp, fb na Insta?. Nakukaribisha home kwangu, nikurejistie, inahusisha kukutengenezea a face ID yenye jina la Sky Eclat, kisha nakuandikishia Tin Number, nakuchukulia Driving Licence ambayo sasa ndio utaitumia as official ID yako, una register sim card mpya kwa jina hilo, unafungua fb, what’s app na insta.

Kwa vile hii kinachofanyika ni forgery, inabidi mambo haya yafanyike kwa siri, hivyo itakubidi uje nyumbani kwangu, tena chumbani, maana vifaa navihifadhia uvunguni!.

Tena hata ukitata National ID, Passport, na any official registration, ila hiyo pasport usiitumie kuombea viza ya US tuu, kama uliishawahi kuomba visa na kuingia US kwa passport nyingine, maana wao wanafanya biometric verification pale airport kabla hujaingia, hivyo utashtukiwa.

Kikawaida ingekugharimu sana, lakini wewe nitakufanyia bure… si unajua tena ila na wewe…

P

Hawamjui Sky Eclat. Lakini email yako inafahamika na namba ya simu yako inakuwa system inaijua