KUWA MACHO NA FORUMS ZINAZOANZISHWA USIJE KUWA MTEGO WA JIWE

Kama ingekuwa hivyo basi wengi ndani ya JF wangeshakamatwa, lakini hakuna hata mmoja aliyekamatwa na hili genge la wahuni na wauaji wanaojiita Serikali.

Ongeza na sura ya huyo mnyamulenge Mkuu aliyefoji kabila na kujifanya ni Mkoromije.

Picha moja nimeiacha makusudi, time ikifika nitaiweka

Tupe elimu location on unaionaje kwenye window ninapofungua JF

Stuka sana Mkuu. Kule Bongoforums nilikuwa nataka kujiandikisha nilivyomuona Mwanakijiji tu yuko kule machale yakanicheza.

Mkuu hizo forums sio za kujisajili, ni za kuziangalia kama guest na kuwaacha wenyewe. Ukiwa na madini yako unakuja kuyatemea huku kwenye uhuru wa kweli.

Kabisa Mkuu, kwa sasa mpaka JF itakaporudi hewani kama itarudi nimeamua ni bora kubaki hapa ukimbizini badala ya kuhangaika na hizo forums nyingine ambazo zinaweza kabisa kuwa zinatumika na wauaji wanaojiita watu wasiojulikana.

Washindi huwa tunashinda kwanza halafu ndipo tunakwenda vitani, wakati wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndipo wanatafuta ushindi…tehteehhh

Mimi wakinikamata labda wakichemshe supu waninywe maana ni mifupa mitupu.

Na BAK unavyokuwaga unanyoosha goti sipati picha wakikumata, unaweza kuwa mkuu wa mkoa wa wale waliofia kwenye viroba.

Hakuna online platform ilio bongo ikawa free kukosoa utendaji wa sirikali ikachekewa,
Labda kama unapenda umbea

Acha kabisa Mkuu. Kuna kisa kimoja nikajua jamaa leo wamenipata lakini Mwenyezi Mungu si Athumani. Hawawezi kutuharibia nchi yetu huku tukiendelea kukaa kimya dhidi ya uhuni wao na mauaji.

hahahaha lumumba wanahangaika sns nchi imewashinda wanavamia hadi bungeni na rula kupima samaki

tena watamtundika pale posta mpya kwenye mnara wa askari ili awe wa mfano kila mtu amuone.

Wapumbavu sana hawa jamaa. Mambo yenye maslahi kwa Watanzania wanakaa kimya huku wakihangaika na yasiyo na kichwa wala miguu. Tanzania ya Viwonder!

Internet ni kama uko ndani ya nyumba ya kioo halafu usiku,ukiwasha taa tu watu waliopo nje wanakuona,iko hivi; hakuna usalama wa 100%
Nalog off

Asante kwa tahadhari @kyekomakubi. Mimi nakomaa huku KT mpaka JF itakaporudi.

wanacho weza kufanikisha ni kufika bei na hawa mods wa humu kisha wana reveal your IP address ambayo nadhani kila simu ina ya kwake na wakisha ipata wanaanza kuifanyia kazi… location inatumika na line gani n.k

kama sio kufika bei ni kuishambulia hii kt na kuiba data za wateja

Cha ajabu hiyo wanayoipigia promo ilianzishwa punde Tu baada ya Jf kuzimwa wakijua member wengi watakimbilia humo …everyone be careful