Lengo la waasisi wa EAC linatimia..

Acha upotoshaji hapa ukimbizini hata ww upo vinginevyo tuonyeshe hiyo forum yako huko nyumbani iliyolipia leseni mkiwa mnachangia. Tatizo sio kulipa kodi bali ni nia ovu ya sheria ya kuwalinda watawala kwa kutaka kuwajua wachangiaji humu mitandaoni, ili wale waweze kuwadhuru.

Ni kweli kuwa kuna wafanyabiashara ambao wametoa fedha na kuzificha nchi jirani; lakini je ni sahihi kukwepa kulipa kodi stahiki? Je wapinzani mtaweza kuendesha nchi bila kodi??

Narudia usitake kupotosha, kila mtu anakubali kulipa kodi kwani ndio msingi wa nchi kujiendesha na kupata maendeleo. Lakini kodi inapotumika kama silaha ya kudhuru wenye mitazamo tofauti, ndio hayo hata ww unayeunga mkono hiyo sheria uko huku uhamishoni.

Ni hulka ya kila mtu kupenda kupata faida kubwa; ila tujifunze kuchangia maendeleo kwa kulipa kodi; najua ni very painful ila inabidi tufanye hivyo; swala hapa ni kuchagua watu sahihi wa kuisimamia Serikali( wabunge) ila kwa bahati mbaya sana hapa tunafeli kwa kuchagua watu kwa mihemko na upinzani wanaongoza kwa Hilo.

Unaongea nini mjomba? Wabunge wa upinzani ni chini ya 30%, hata kama wapinzani wawe na hoja vipi ni nadra kupita kama hayaakisi matamanio ya ccm kuendelea kubaki madarakani. Kibaya zaidi hata huo mfumo wa kuchagua hao wabunge nao una walakini mkubwa, ndio maana unaona mengi ya maamuzi sio matakwa ya wananchi bali matakwa ya kikundi kinachohodhi madaraka. Hivyo unapokuwa na bunge lenye wabunge wengi waliopata ubunge kwa njia zisizo halali ni lazima watasimamia wale waliowapa hizo nafasi.

Hilo la kwamba kulipa kodi kunaauma ni kama unalazimisha hoja yako ya kutokulipa kodi. Lakini ukweli unabaki jamii forums haina tatizo la kulipa kodi bali ni masharti ya watawala kutaka kujua wachangiaji ni akina nani ili wenye mtazamo tofauti wawadhuru na hatimaye kuunga nguvu ya kuhoji ibaki ya kusifia tu.

Hoja kwamba mfumo wa uchaguzi hauruhusu kukua kwa upinzani hiyo ni hoja dhaifu naikataa;

Toka 1992 kuanzishwa kwa vyama vingi na uchaguzi wa 1995 upinzani umekua; Chadema pekee wana wabunge zaidi ya 30 wa kuchaguliwa;

Kilichopo sasa ni upinzani dhaifu usio na hoja unaotafuta kivuli cha Magufuli na Serikali yake kuficha madhaifu yake.

Kama kodi sio tatizo kwa JF si walipe tu;

Swala la kuwa identity za watu zitafahamika ili wadhuriwe ni uongo kwani hata kule JF tulikua tunafahamika sana tu; na Hakuna aliyedhurika kwa post ya JF

Sitarajii kama unaweza kukubaliana na hoja ya mazingira kutokuwa sawa ya ushindani kati ya upinzani na chama tawala. Hakuna namna unaweza kukubaliana na ukweli huu lakini habari ndio hiyo. Ni kweli upinzani umekuwa ila katika mazingira magumu na sasa mazingira hayo yamegeuka hatarishi kuliko ilivyokuwa hapo mwanzo.

Wewe kama mwanaccm sitegemei useme upinzani una hoja za msingi kama ambavyo mimi sioni kwama ccm wanahoja za msingi, lakini kipimo cha kupimia uzito wa hoja ni uchaguzi ambao hauko katika mizania sawa hadi kuelekea kupata viongozi wengi bila ridhaa ya wananchi na hilo lipo wazi. Na ule uchaguzi wa juzi wa marudio uliondoa shaka ya hilo mpaka viongozi wa dini kutoa nyaraka kuhusu ushenzi ule.

JF hawana tatizo la kulipa kodi na wala haitokaa itokee, shida ni masharti ya kutaka kujua wachangiaji humu ndani ni akina nani. Kama wachangiaji humu ndani wanafahamika kwanini serekali inamlazimisha Mello awape details za wachangiaji humu ndani? Mfano ili kesi inayoikabili jf kuhusu sakata la mafuta bandarini. Ni kwanini serekali haikumkamata mtoa taarifa mpaka ikapeleka kesi mahakamani kulazimisha hali hiyo na mpaka sasa bado inalazimisha hilo. Juzi nimemsikia Mello akihojiwa na chombo cha habari cha nje akasema ndani ya miezi kumi na 12 sasa amekuwa akipata shinikizo kubwa kuwasilisha details za watumiaji wa humu jf.

Nimekushauri wewe na wengine ambao mnasema Magufuli na serekali yake wanakubalika sana, kwanini msifungue forum yenu mkawa na verified id mkasifia mpendavyo? Mbona hata wewe umehamia huku mafichoni tena kwa fake Id?

Narudia usitake kupotosha, kila mtu anakubali kulipa kodi kwani ndio msingi wa nchi kujiendesha na kupata maendeleo. Lakini kodi inapotumika kama silaha ya kudhuru wenye mitazamo tofauti, ndio hayo hata ww unayeunga mkono hiyo sheria uko huku uhamishoni.