Maalim Xuma

@introvert alienda wapi hizi streets?

Ziviona vibonzo vyake.

Tunachokora kwa mtandao…sisi ni machokora !

Bwana Xuma… Hi thredi (thread) yako imeniwacha Kwanimi mataa… Sina kamusi bana

Wewe ulifika kwa M ukamalizia hapo…

Thread…Uzi. Usijali kaka ‘mchoma mahindi’. Tupo hapa kukwamuana.

He he he :smiley:

Kukwamuana… My mind goes into overdrive…

Nakupata lakini haina maana ile unayokusudia kaka.Dhana hii imetumika kwenye Mnyambuliko wa vitenzi katika hali ya kutendeana.
Mawazo yako yamezama katika ule muktadha mwingine wa kujamiiana.

Shiet…kutendeana. You go kill me now…

Huwa inaleta hisia Kali wakati wa kufunza hili somo ukizingatia maneno yafuatayo;
Fanya…Fanyia…fanyana…fanyiana…fanywa
Tenda…tendea…tendana…tendeana…tendwa
Kula…kulia…kulana…kuliana…kulwa
Weka…wekea…wekana…wekeana…wekwa
na kadhalika. Nitashughulikia hill funzo hivi karibuni.

Sio kizingiti, ni ukomo. Ukomo wa fikra, mtazamo, uelewa tamati.

Mie Mswahili ndivyo navyoelewa

Usahihi ni ‘wenye shida ya matamshi kutokana na lahaja’

Ahsanta

googling is a verb…

Kweli @Okwonkwo

Kizingiti ni mwanzo au mwisho wa kitu fulani.
Kizingiti ina maana ya mwanzo au mwisho.Inaashiria uwili.Ilhali ‘ukomo na tamati’ huashiria mwisho pekee kakangu.

Fanya utafiti zaidi utabaini.

@Meria Mata ulikwepa mapeeema!

Usisahau kuweka hali ya kufanyiza kwa mfano fanyiza, kulisha,

Ngambwe
Verb ni nini kwa kiswahili

Niliisahau.Shukran.