Mabadiliko ya uongozi TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki)

Askofu hupatikana kwa mapendekezo yanayofanywa na maaskofu waliopo. Mapdri wenye uwezo hupendekezwa na na hatimaye papa hiwateua nafasi inapopatikana. Jina la kitima lingekuwa Roma nahisi angekuwa ashateuliwa kitambo sana kwa sifa na uwezo wake. Inawezekana jina lake bado halijaenda, ila inawezekana pia lishaenda.

Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi wako japo nahitaji ufafanuzi zaidi ya huu ulioutoa kama sintokukwaza. Uwezo wa padri unapimwa kwa kuangalia nini? Kuhubiri au kusimamia maendeleo kwa kanisa au jimbo lake?

Nina mfano halisi, Arusha kulikuwa na padri mmoja alifariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 100 alikuwa akiitwa Padre Joseph Babu. Padri huyu alileta maendeleo ya dhahiri kwa kanisa na jimbo lake. Alijenga kanisa la katoliki Ngarenaro, alijenga hospital kubwa tu hapo parokiani na ni hospitali maarufu hapo Arusha mjini kwa jina hospital ya padre Babu. Alijenga shule ya sekondari na sasa imetoa tawi la chuo kikuu cha St. Augustino. Hayo ni baadhi achia mbali shule na zahanati na hosptali mbalimbali alizofungua mpaka mauti yanamkuta.

Kwa jumla amekuwa padri zaidi ya miaka 60 huku akifanya maendeleo makubwa tena kuliko maaskofu wengi. Sasa mtu mwenye uwezo huu hajawa askofu, najiuliza ni uwezo upo unahitajika mpaka ukasema huyo wako alipaswa kuwa askofu na sio padri tu?

Sawa sawa

Hahaha kama kauli ya Dr Shoo jana huko Njombe nashangaa haijapata kiki

Huyo huyo

Dr Charles Kitima,hope aliwahi kuwa VC wa SAUT

Siyo Kila mtu anaweza kuwa Rais wengine wanafaa tu kuwa Mawaziri wa Ujenzi,ukiwapa Urais wanaharibu

Sawa naona mnasema jembe jembe… Tunashukuru sana kwa hayo majembe sasa yako shambani twasubiri mavuno yake. asante Mungu

Mkuu nimekusoma, basi inabidi tukubaliane pia pamoja na uwezo na mapendekezo, bado pia kuna swala la bahati pia.

Ni kipimo gani unatumia kupima uwezo wa rais? Hakuna mtu mwenye akili timamu atashindwa kuwa rais wa Tanzania. Urais wa nchi yetu sio lazima uongoze kwa ubora bali ni ili siku ziende.

Hapo ni sawa sasa.

Ha ha ha ha nimecheka,2020 na Mie nagombea