Ni hivi, JF si kwamba walikataa, ila wanachosema ni kuwa wanaopaswa kusajiliwa kama Online Content Providers, sasa JF wao wanamiliki platform tu na content providers ni sisi wanachama, na endapo wangejisajili kirahisi ni kwamba wangetakiwa kukubaliana na vigezo vifuatavyo
Mmiliki wa blog/forum atawajibika kwa chochote kitakachowekwa kwenye site yake.
Pale itakapo hitajika mmiliki atatakiwa kutoa taarifa za watumiaji wake.
Hayo ndo yamefanya wasite kujisajili mkuu, mimi nina blog na nimefuata taratibu zilizowekwa bila tabu lakini kwakuwa nafahamu namna JF inavyofanya kazi naelewa nikwanini wamesita kujisajili hata ingekuwa wewe usingethubutu unless umeamua kuwauza watumiaji wako wakapate kipigo cha mbwa koko.
Jombaa unapigana sana na keyboard, Fanya utafiti mzuri kabla ya kuvamia keyborad
Hivi Kina Mexence Mellow wamekosa hiyi milioni Moja ya usajili na ada?
Iko hivi, Moja ya kipengele cha usajili ni issue ya kutoa information za watu endapo zitatakiwa na serikali hapo ndipo kwenye utata man.
Wewe mwenyewe hapo inajiita MAGUFULI 4 CHANGE IN BLOOD. mbona usijiite jina lako halisi ambalo nalijua mimi,
Nadhani dhulma kubwa ni kutumia nguvu nyingi kuunyima umma uhuru wa habari, kufanya hivyo kunazidisha hofu ya kujiandalia mazingira ya kuwa dikteta, kama una nia njema kwanini hutaki kusikia usiyopenda kuyasikia? Watanzania wanafiki aina yako ndio chimbuko la madhila haya. Nguvu unayoitumia kumsakama Max ungeitumia kuwaeleza waliokutuma kuwa jamii ya sasa inahitaji zaidi teknolojia kuliko kurudishwa nyuma kwa namna wanavyofanya.