mobile network companies in tanzania should pull up their socks, bakhresa is coming to invest in same sector.

vodacom ndio mtandao ninaoutumia kwa kuduma za Internet, ila bado sijaridhika na huduma zao.
juzi kati niliunga WiFi ya halotel, mzigo ulikuwa faster sana mpaka nikashangaa.

Mkuu labda tuanzie hapo umeifahamu dstv toka lini?,kwa anaye jua ubora lazima aijue dstv,kwa hiyo mtu akitumia njia ya PA,ni tatizo kwa sasa ameongeza huduma kulingana na aina ya wateja anao wahitaji,je kuwa na media ambayo unachopata hakilingani na unachokiingiza ndio ujanja??unachukua pesa toka kwingine kulipa wafanyakazi wa chombo chako cha habari ndio ujanja!!azam sawa anajitahidi lakini bado hajafikia huko unakotaka kutuaminisha.

kwahiyo zile ndege za nini?

baki na unachokiamini na mimi nibaki na ninachokiamini.

karibu katika ulimwengu wa “azamtel”. hahahaha

kuwa na ndege ndio kuingia katika aviation business?.

Jamani mnakosea mnapo jumuisha tu !!yaani mitandao ya tz ,kila sehemu kuna mbambe wake,utakuta hapa voda ndiyo yupo vizuri,pale hakuna kitu,labda kama hiyo tathimini yako unaifanyia posta/upanga dsm,na pale karibu mitandao yote iko vizuri!!lakini kwingine kila mtu atakuwa na jibu lake tofauti tofauti.

Pesa kidogo GB za kumwaga…

Mimi ninatumia mitandao yote. Lakini ukweli kila mara najikuta ni lazima nirudi kutumia airtel tu.
Hawa jamaa mtandao wao una kasi ileile wakati wote.

Voda kuna wakati mchana inakuwa ovyo sana.

Halotel zamani wakiwa wageni walikuwa uhakika. Sasa majanga tu.

Wacha waje tuwe na uchaguzi wenye wigo mpana zaidi

Uko sahihi kabisa kulingana na ushindani wa Azam umefanya hata Dstv kujishusha na kuwafuata wananchi wa kawaida.

Zamani nilikuwa nahisi Dstv ni anasa, ila toka nifunge naona kawaida sana japo vipindi vyao ni vya viwango vya juu, kwa kweli unachokilipia kinaendena na thamani ya fedha zako.

Azam wasiachie VPL maana ndio inayowabeba…Japo nasikia Dstv nao wanaimendea mara baada ya makataba kumalizika.

Kwa mimi mpenzi wa soka na michezo mbalimbali Dstv haina mpinzani.

Wabongo tunavyopenda mteremko hapo watu wanasubiri waambiwe kupiga Simu itakua bure

Pale mnaposema na kujisifia kabisa cherehani nne ni kiwanda Bhakresa anawatizama na kuwacheka kwa dharaaaau sana…

Ukitaka real definition ya kiwanda/viwanda huyu jamaa ndiyo case study…

Tuone nani ataenda kuzindua kiwanda cha ATTL…

Cc: @Mahondaw

Sisi tunataka ubora na unaafuu wa Internet.

Hili eneo ndio linalotumika sana siku hizi, watu hawataki mavifurushi ya voice.

H

hiyo voda kwenye swala la internet wamezidiwa,before walikuwa vizuri sana but now nahisi uchakavu wa mitamba na wingi wa watumiaji wa huduma hiyo,kuna baadhi ya maeneo wana speed ya konokono.

Kweli kabisa mkuu, mimi natumia internet ya Vodacoma na Halotel, lakini Voda wako vizuri zaidi, ila sijui kama labda inategemea na eneo husika ndio linaamua ubora wa internet yake kutokana na ubora wa mitambo yake

Swadacta! Umenena vema mkuu!

Upambe katika kiwango cha juu Sana… Hongera

haina ubishi kuwa VPL ndio backbone ya azam tv the same kwa dstv na league ya uingereza.

ukiondoa ubora wa channel na vipindi vyake, dstv bila FA ni sawa na kazi bure.

nina hakika azamtv hawatakubari kuona vpl ikichukuliwa na washindani wao, wataweka dau lolote katika tenda ili iwe vigumu kwa wapinzani wao kulifikia.

ni sawa na kilichotokea three years ago pale
board ya league ilipotangaza tender ya kuonyesha vpl, bakhresa aliweka mezani tsh 23 billion, mpinzani wake wa mwisho alikuwa ni startime, yeye aliishia kwenye 18 bilioni na hakuweza kupanda zaidi ya hapo.

so nina hakika next time, bakhresa hataona hasara kuweka mezani hata 30 bilioni ili tu ashinde tender ya vpl.uwezo wa kufanya hivyo anao. let’s wait,2020 sio mbali.

siku si nyingi tutakuwa tunapishana kwenye kibanda cha “azampesa” tukifanya miamala.
hahahaha

[ATTACH=full]179378[/ATTACH][ATTACH=full]179379[/ATTACH]