Jamaniiii, hapa nishavuta kumbukumbu hadi masikio yanaenda upande… nakumbuka ofa ya mwisho nilipewa ilikuwa kwenda kufuturu, na ile ofa niliikubalia. Je ndo hiyo? ni wewe maana hapa uko na jina jipya sijajua kule JF ulikuwa unatumia jina gani.
Sikukumbikia jamanii, nilikukubalia ila nikawa nasubiri maelekezo ya eneo husika ni wapi… sikuona PM wala maelezo zaidi nikawa mpole.
Hivo eeeh, basi itabidi niokae macho uchaguzi au uteuzi ukianza tuu nujitokeze nami nichaguliwe niwe balozi kabisa kama sio katibu tarafa au katibu kata hahahahha.
Haki ya Mungu ukiwa na mwanamke mwenye kumbukumbu kama kassie huna haja ya kuwa na kompyuta…haswaa ndiyo ile futari…nikawa bize kuwasiliana na waandari wa ile futari kurudi tayari tushawekewa mapadiloku…nilipoingia nilikuta notifications tu sikuweza kuzisoma tena…anyway kesho…nasema kesho…ukuje hapa karipu na afisi ya gavana wa hii county ya nbi tusherehekee eid pamoja na mafriends zangu pia unawesa kuja na mafriends sako.
Hhehehehehehe kwahiyoooo, kwakifupi ni kuwa unaandaa pati ya kusherehekea Eid… na mie ni mmoja wa waalikwa…
Basi Inshallah, panapo maajaaliwa Eid pili ntakuwa available. Nimekuja nyumbani mara moja, ule msiba wa wanafunzi wa chuo waliopata ajali wkenye ambulance mmoja wapo ni binamu yangu. Hivo kesho siku ya Eid ntakuwa msibani ila jumamosi nipo na jumapili nageuza kurudi kazini. Count me in on Saturday.
Pambana ndugu yangu, mapambano ndo yameanza hivo hakuna kulaza damu. Ni mwendo wa mchaka mchaka hadi Mzee Baba nae atu join kwenye hii jogging hahahahaa.
Oooh poleni sana…wape pole ukweni huko…ooh yaeh I saw that picture taken on the scene… Dah so sad…
Party ni nzuri kwa kujiliwaza na kuongeza network… J3 ukinikuta kny tractor shambani utadhani siyo Mimi…