Nimegundua JF ilitufundisha ustaarabu mkubwa sana.

Safi sana. Mbona ni kama nakujua wewe? Jitabulishe chap chap ngamia hii. :smiley: Hahaa aiseee huku ni kuzuri buana tunajiachilia hadi raha. :smiley:

Ntolilo ila JF ya mwanzo kulikuwa na ustaarabu mkubwa sana watu walishindana kwa nguvu ya hoja bila kuitana haya mshenzi au mpumbavu.

Tatizo lilianza pale MACCM walipostuka na kuanza kuiona JF ni tishio kwa hoja zilikuwa zikijengwa za maovu yao mbali mbali hasa ufisadi na pia waliona kwamba idadi ya wanachama ilikuwa inakuwa kwa kasi.

Yule Mwigulu katika kikao kimoja cha MACCM akaweza kuwashawishi MACCM kuweka bajeti ya kuwalipa buku 7 na pia kuwapa laptop kuja humu ili kuvuruga mijadala kwa namna yoyote ile ikiwemo kutumia matusi ya nguoni.

Walipoingia tu ndiyo tatizo la urushaji matusi likashamiri sana. Buku 7 hawakujali kufungiwa kwani walikuwa wana IDs chungu nzima hivyo kufungiwa kwao hakukuwa tatizo kwani ikifungiwa ID moja anahamia nyingine na kuendelea kurusha matusi. Walikuwa hawana hoja zenye nguvu kwani ni kazi mno kujenga kuwa na hoja nzito huku reality ikionyesha MACCM na Serikali yao yananuka rushwa na ufisadi uliokithiri.

Duh JF ikageuka kiwanda cha ajira aiseee. Hapo hapo imetumika nguvu kubwa kuua hizo ajira sijui wahusika wanajisikiaje huko walipo kwa kukosa pesa za bure

Naam kun awatu ambao labda kwa sasa hawana ajira kisa dikteta kutotaka kukosolewa kwa maovu yake mbali mbali. Na si ajira za JF tu bali blogs nyingi nyingine ambazo hawakuweza kumudu masharti makubwa ya kujiandikisha hasa kutokana na bei kubwa.

Daah kuna blog zilikua na matirio ya akili sana aiseee utawala huu umeua vipaji vingi.

Ntolilo ndo Numbisa??? Nimemiss sana vile vibwanga vya cheka na Numby.

Ndio mkuu ni mie. Daah JF ipo vizuri

Hapo sawa, Jf noma aisee ila Pogba hana utu kabisa. :smiley:

Yaan katuzima ghafla

Acha tu aisee. Yaani alivotusambaratisha ghafla bila notisi, haina budi itabidi tushike adabu zetu. :smiley: Btw umeuona @Nalendwa humu?

Bado hajafika au kama kafika atakua anatumia ID nyingine ambayo hatujaigundua

Dah namngoja sana. Nimemmiss kishenzi.

Bila hata JF sisi watanzania automatic ni wastaarabu na wakarimu sana…

Though kuna wachache wanataka to take advantage of that na kutufanya sisi ni wapumbavu…

Cc: @Mahondaw