Simulizi:Viganja mikononi mwangu

Asante sana mamy

Woooooooooooozeeeeeeeerr

Usaliti unanukia kwenye hii simulizi… huko mbeleni damu itamwagika…

Cc: @Mahondaw

nimefika mpenzi wangu

Sawa my honey

Ahsante sana

ooooooo

Jamani naona hii story tutaendelea nayo jf kwetu naona karibia inarudi huku kunachosha mno

Shunie endelea nayo wakati tunasubiri JF yetu irudi

Kwahiyo niendelee tu

SEHEMU YA 04

“Shoga mwenzako najuta kwa nini sikuwa nikichoma sindano za kuzuia mimba! Yaani umalaya wangu huu leo unanifanya nikose mtoto! Nimetoa mimba nyingi, mwisho wa siku leo hii nakosa mtoto! Hivi kweli mimi wa kukosa mtoto?” aliuliza Evelyne huku akimwangalia rafiki yake, Mwajuma.

“Mmh! Shoga ila na wewe ulizidi. Kila ulipopata mimba, kazi ilikuwa ni kutoa tu, ona sasa, unamfanya mume wako akose amani, alie kila siku, kwa nini lakini? Tena hata sindano za kuzuia mimba ulikataa kuchoma, ” aliuliza mwajuma.

“Wewe acha tu. Kwanza hapa ninachokitaka ni kufunga naye ndoa tu ili hata kama kuna siku mambo yataharibika basi yaharibike tukiwa kwenye ndoa ili tugawane mali manake bila hivyo naweza kuachwa kibudu,” alisema Evelyne.

“Hilo kweli Eve! Siku mumeo akigundua kwamba hata tatizo lolote ni lazima atakuacha. Umemdanganya sana! Kila nikimwangalia namuonea huruma bilionea wa watu. Wewe mwanamke mbaya sana,” alisema Mwajuma na wote kuanza kucheka.
Mwajuma alikuwa shoga pekee wa Evelyne aliyejua kilichokuwa kikiendelea.

Aliyajua maisha ya Evelyne tangu kitambo, walikua wote utotoni na kusoma pamoja. Katika maisha ya ujana waliyopitia wasichana hao yalikuwa ni maisha ya kujirusha na kila mwanaume aliyekuwa akipita mbele yao.

Waliendekeza ufuska, walitembea na kila mwanaume aliyeonekana kuwa na pesa. Walipenda maisha ya starehe kiasi kwamba wakati mwingine walikuwa wakijiuza katika mitandao ya kijamii wakitafuta pesa na kwenda nchi mbalimbali kutafuta mabwana.

Maisha yao yaliharibika, wanaume ndiyo waliokuwa wakiyaendesha maisha yao. Kutokana na kujiona mjanja zaidi, Mwajuma aliamua kujichoma sindano za kuzuia mimba ila kwa Evelyne, aliogopa kabisa kufanya hivyo.

Evelyne alipokuwa akipata mimba, kitu cha kwanza kilikuwa ni kutoa. Mpaka anakutana na bilionea kijana, Cassian, alitoa mimba zaidi ya kumi na mbili.

@Shunie maa tuendelee tu hukuhuku nyumbani huko bado hapaeleweki

Kwahiyo tuendelee tu kama kawaida nyumbani kukirudia tutaendelea napo nilivyoona jf imefunguka nikajua karibia kila kitu kitakuwa sawa

SEHEMU YA 05

Wakawa wapenzi, wakaanza kuishi pamoja. Kwa kuwa alimpata mwanaume mwenye pesa, Evelyne akatulia, akataka kujenga maisha na kutengeneza familia yake ila tatizo lilikuja pale alipogundua kwamba hatoweza kushika mimba kwa sababu mfuko wake wa uzazi (uterus) na ukuta uliokuwa ukishikilia mfuko huo (cervix) vyote vililegea na mimba isingeweza kukaa tena.
“Huwezi kushika mimba.

Mfuko wako wa uzazi umeharibika vibaya kiasi kwamba hauwezi kuruhusu kijusi kutengenezwa,” alisema daktari kwa sauti ya huruma huku akimwangalia Evelyne aliyekuwa akilia pembeni ya rafiki yake.

Hicho ndicho kitu kilichomuumiza mno, hakuamini kama tabia yake ya kutoa mimba ndiyo ingemfikisha mahali hapo. Alilia na kujuta sana huku wakati mwingine akitamani muda urudi ili arekebishe pale alipokosea lakini hakuweza kuurudisha muda huo.

Alijua kabisa kwamba kama angemwambia mumewe kuwa tatizo alikuwa nalo yeye angemuacha na kutafuta mwanamke mwingine, hivyo alichokifanya ni kutumia pesa zake, kwa kila hospitali waliyotakiwa kwenda kesho, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumtuma Mwajuma huko, alionana na daktari aliyetakiwa kuwapima siku inayofuata na kumpa kiasi kikubwa cha pesa ili aseme kwamba mwanaume ndiye aliyekuwa na tatizo.

Huo ndiyo ulikuwa mchezo wao, walifanikiwa, Cassian hakujua kilichokuwa kikiendelea, kwenye kila hospitali waliyokuwa wakiingia, majibu yalitoka na kusema kwamba yeye ndiye aliyekuwa na tatizo kitu kilichomnyima furaha katika maisha yake.

Wakati hayo yote yakiendelea, Evelyne hakutaka kuonyesha kitu chochote ndani ya nyumba, alimuonyeshea Cassian mapenzi ya dhati kwamba alikuwa akimpenda hivyohivyo kumbe dhamira yake kubwa ilikuwa ni kufunga ndoa na mwanaume huyo ili hata kama kuna siku wangeachana basi wagawane mali.

“Nakuonea huruma mke wangu,” alisema Cassian huku akimwangalia Evelyne.
“Hutakiwi kunionea huruma mume wangu! Nilikwishakwambia kwamba mimi na wewe mpaka kifo kitutenganishe,” alisema Evelyne huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Ila sina uwezo wa kumpa mimba mwanamke!”

ngoja mimi nikasome kule kwetu nilipolazoea zaidi

Kipenzi changu

Umeona eenh

mmh mbona sijaiona mpenzi

my love