Wakimbizi wa mtandaoni!!

Ahaaaa

Usijali najisogeza mdogo mdogo

Wengine wabaguzi wanatutusi wazi wazi kabisa sio jambo zuri hata kidogo.

Malipo hapa hapa duniani,tuliwapokea wengine nasi leo tunapokelewa,ahsante Mungu
Nalog off

Hii ni Sifa mbaya sana kwa jamii ya Africa mashariki

afadhali nimepata hifadhi.

Tatizo la ukimbizi ule Uhuru na hisia ya ubinadamu hupungua, na ukitoka nje ya kambi lazima utaitwa mhamiaji haramu.

Account yangu ya hili jukwaa ilikuwa in active for so long. Ngoja nikamwite Faiza naye aje huku maana ameshamaliza mfungo.

Hivi Yule bibi Yupo mrengo gani

Ombi langu watuletee na app kabisa ili tupate na uraia wa kudumu

Ndo hivyo tushakuwa wakimbizi

Sasa hivi mambo yalivyovurugika watu hawaeleweki. Ila Kwakuwa jiwe anawaponda KKKT na TEC live akiwa na Masjid, bila shaka Kikongwe atamkubali tu.

Bi Mkubwa ni mtu wa mtambani hata kama hawapendi CHADEMA. Yeye ni mzee wake Mohamed Said hawaipendi CCM lakini pia hawaipendi CHADEMA na kila wanaesimama nae mstari mmoja huwaangusha!

Dah!!

Ndiyo shida ya monopoly. Jukwaa la mtandaoni (electronic social platform) linalotoa fursa kwa jamii kupeana habari na kujadili masuala mbali mbali, halikupaswa kuwa moja tu kama ilivyokuwa huko Tz kwa Jf. Yalipaswa kuwa mengi ili kama mmoja akizengua au akapatwa na matatizo kama aliyoyapata Jf, wananchi hawataathirika na kubidi baadhi wawe wakimbizi wa kimtandao kwenye nchi jirani.

Hili liwe funzo kwa watanzania. Na kwa wanahabari kama akina Pasco Mayalla waone hii kama fursa ya kuanzisha majukwaa yao ya aina hii kwani ni dhahiri kuwa huduma hii inahitajika and it is good buisiness - inalipa na hakuna sababu kwa nini isisajiliwe rasmu na wamiliki kulipa kodi stahiki kama ilivyowekwa na sheria. Na hakuna sababu ya kukaidi kufuata maadili ya habari kwenye maudhui ya habari za mtandaoni. Kutumia fake name isiwe ndiyo kinga ya kuropoka ovyo na kuvunja sheria za nchi. Anayefanya hivyo mmiliki wa mtandao husika asikatae ku reveal the real ID ya mhusika kwa mamlaka husika kwa utaratibu uliowekwa na sheria na kanuni zake. Haya yataifanya mitandao hii kuwa bora zaidi.

Kurudi sio shida, usalama wa wakosoaji utakuwepo? Sioni Mello akihimili shinikizo la wasiojulikana. Humu wameshajaa wasijulikana kusems tumehamia huku maana wiki hii serekali imelala unono.

Ukizingatia bajeti ndio ipo mezani, hapo mambo yao yanenda vyema maana hawapati kelele nyingi za JF

Hebu ninaomba unipe tafsiri ya neno kuropoka. Maana kuna tafsiri tofauti ya kuropoka kwa watawala. Niweke vizuri ili nikupe ukweli wa hii hoja yako.

@Tindo nimefurahi kukuona! Malizana na huyo jamaa @Sungura !

Ndiyo shida ya monopoly. Jukwaa la mtandaoni (electronic social platform) linalotoa fursa kwa jamii kupeana habari na kujadili masuala mbali mbali, halikupaswa kuwa moja tu kama ilivyokuwa huko Tz kwa Jf. Yalipaswa kuwa mengi ili kama mmoja akizengua au akapatwa na matatizo kama aliyoyapata Jf, wananchi hawataathirika na kubidi baadhi wawe wakimbizi wa kimtandao kwenye nchi jirani.

Hili liwe funzo kwa watanzania. Na kwa wanahabari kama akina Pasco Mayalla waone hii kama fursa ya kuanzisha majukwaa yao ya aina hii kwani ni dhahiri kuwa huduma hii inahitajika and it is good buisiness - inalipa na hakuna sababu kwa nini isisajiliwe rasmu na wamiliki kulipa kodi stahiki kama ilivyowekwa na sheria. Na hakuna sababu ya kukaidi kufuata maadili ya habari kwenye maudhui ya habari za mtandaoni. Kutumia fake name isiwe ndiyo kinga ya kuropoka ovyo na kuvunja sheria za nchi. Anayefanya hivyo mmiliki wa mtandao husika asikatae ku reveal the real ID ya mhusika kwa mamlaka husika kwa utaratibu uliowekwa na sheria na kanuni zake. Haya yataifanya mitandao hii kuwa bora zaidi.

Kuongea maneno ya kuudhi wenzako, kutukana, kudhalilisha, kubagazana, kutoa siri za wenzako au za nchi, kuchonganisha au kugombanisha wenzako, kufanya uchochezi wa wananchi dhidi ya serikali yao halali nk nk.

Nipo mkuu. Huyo Mello anashinikizwa mwezi wa 12 sasa atoe taarifa za wakosoaji. Hamna namna ya kujiongeza zaidi ya hivi.